Ujumbe muhimu: Mashabiki wenzangu wa Simba tulifeli hapa

Huyu njaakalihatari anaelekea kwenye ukichaa sasa ,jamani msichukulie mpira seriaz sana kumbukeni mna familia na mambo mengine muhimu ambayo yanawategemea.
 
Kwa bahati mbaya kwangu sikuwahi kukufuatilia miongoni mwa mashabiki wa Simba humu JF. Leo nimegundua busara na hekima ulizonazo na nakuongeza kwenye orodha yangu ya mashabiki wa Simba ndani ya JF Γ mbao ni Genta, Cocastic, Scars.
Baada ya ligi kumalizika Genta aliandika Uzi ulioshambuliwa Sana kuhusu madhaifu ya Simba. Kati ya maeneo aliyogusia na Mimi binafsi kumuunga mkono na Uongozi wa Simba pamoja na Benchi la Ufundi wameacha hivyo hivyo ni eneo la Kiungo mkabaji. Tulisema na narudia kusema Simba inashindwa kujua kuwa Mkude siyo DM? Mmemsajili V.A lakini inaonekana kocha mpya hajamkubali japokuwa Mimi namhusudu Sana mbali ya kasoro yake ya ball control.
Ukiangalia magoli aliyofungwa Simba juzi, assisters wamepita free eneo la DM wa Simba. Anayebisha aangalie upya magoli yale mawili. Ukitaka kuona umuhimu wa DM makini angalia upya tukio la Kadi ya njano ya Feitoto dhidi ya Okwa na uniambie Kwa nini aliamua kumvuta jezi Kwa gharama ya Kadi japokuwa yeye hakuwa DM.
Kumekuwa na ushabiki usio na faida na wengine wakidhani mashabiki hawana nguvu kwenye timu. Hebu angalia pale Man U Ten Hag anataka kumsajili mchezaji mashabiki wanasema akija aidha hatutakuja uwanjani au tukija tutamzomea, na hajasajiliwa. Leo humu watu wanasifia hata visivyositahaili ilimradi ni vyao, wanakosoa hata yasiyoatahili ilimradi si yao. Hao si mashabiki ni Washangiliaji, na humu JF washangiliaji ni wengi kuliko mashabiki. Pole kwako wewe unayejua soka.
 
Mngeshinda haya yote yasingekuwa na maana. Kubalini matokeo!
Hakuna sehemu alipokataa matokeo. Shabiki mzuri utamjua hata akishinda unamuona anakosoa madhaifu. Lakini humu Yanga wameshinda lakini ni Mtu mmoja tu alionyesha madhaifu machache ya Yanga.
 
Tate,
Hili la kuwekeza kwenye maneno timu zote za Kariakoo mko vizuri. Nadhani ni Kwa vile mko karibu na Soko kuu. Ukimtaja Ally usimsahau Manara.
 
Huyo wala usimfuatilie utapoteza Muda. Yuko na mwenzake ni maarufu wa kuanzisha nyuzi za matokeo lakini ni mweupe kichwani kama pamba ya Simiyu.
 
Kwahiyo washabiki wa yanga hawaisemi simba?
 
Kwahiyo washabiki wa yanga hawaisemi simba?
Simba tukikithirisha kiasi ambacho tukasahau kukosa na kurekebishwa mapungufu ya timu yetu mfano rahisi angalia sasa nyuzi za malalamiko ambazo kimsingi ushauri na napendekeza hayo yangekua yametolewa tokea awali ingesaidia.
 
Huu uzi wa kujadili kistaarabu tafadhali tumia lugha nzuri mambo ya ushangingi hayana nafasi hapa.
Mkuu tumekuwa tukipishana kauli kwenye mada mbali mbali ila kwa hili NAKUUNGA MKONO badilisha mtazamo wa mashabiki wenzio hapa jukwaani




Sema wanangu mnapuyanga sanaaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Simba SC kupoteza mchezo wake dhidi ya Yanga SC ni matokeo ya mpira, kwangu naona uwepo wa Nabi muda mrefu pale Yanga umemsaidia kuwajua vizuri wachezaji wake na awatumie vipi, ukilinganisha na kocha wa Simba SC ambaye bado ni mgeni.

Zile sub alizofanya Nabi ndio chanzo cha yote haya, anajua matumizi sahihi ya wachezaji wake, kocha wa Simba SC alikuwa kama anabahatisha kwa zile sub zake sababu ya ugeni wake.
 
Fukuza fukuza makocha imechangia Simba kudorora,kweli kabisa Nabi mechi zake nyingi zinaamuliwa na subs zake matata mfano fainali FA na nyinginezo ligi kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…