Watanzania wapendwa,
China ilipokuwa na nia ya kuwekeza 35% katika bandari ya Hamburg ambayo ni bandari kubwa kabisa Ujerumani, bunge la Ujerumani, wizara sita za Serikali ya Ujerumani na Usalama wa Taifa (yaani Foreign Intelligence Service) ya Ujerumani na European Commission wote walikataa na kusema kwamba ni lazima kujihadhari sana na uwekezaji wa mwekezaji yeyote atokaye Ulaya katika sehemu kama bandari kwa sababu ni sehemu muhimu sana kwa usalama wa taifa - yaani: Strategic national security area.
Baraza la Mawaziri lilifanya kikao maalum na Usalama wa Taifa wa Ujerumani wakanyafanya utafiti.
Wanasiasa na wananchi wakapaza sauti sana. Nia ya wote ilikuwa kuchunguza kama ni sawa kuiruhusu China kuwekeza katika bandari la Hamburg.
Baada ya Utafiti na baada ya mazungumzo marefu, mapna na makali kama pilipili uamuzi ulitangazwa kwamba China haitaruhusiwa kuwekeza zaidi ya 25% katika bandari ya Hamburg. Nia ya China ilikuwa 35%.
Mwezi wa tano mwaka huu wa 2023, kampuni ya COSCO ya China ilitia sahihi mkataba wa uwekezaji wa 24.9 % katika bandari ile ya Hamburg.
Kwa nini 10% iliondolewa?
Ili kuondoa kabisa uwezo wa COSCO kuwa na nguvu za kupinga maamuzi yoyote yanayohusu uendeshaji wa bandari la Hamburg (yaani Veto power).Nguvu za uamuzi wa uendeshaji wa bandari na mambo yote yanayohusu bandari zimebaki na serikali la Jimbo la Hamburg na serikali ya Ujerumani.
Sio kitu kigeni kuwa na mwekezaji kutoka nje ya nchi katika bandari, ila lazima kujitahadhari kwa sababu bandari kubwa kama bandari ya Dar es Salaam ni sehemu - very strategic kwa national security.
China haijawekeza katika bandari la Hamburg tu. Imewekeza katika bandari la Rotterdam kule Netherlands, bandari la Piraeus kule Greece na pia Ubelgiji, Uispania na Italia.
Naunga mkono Mama Rais Samia Suluhu na Serikali ya Tanzania na Usalama wa Taifa wa Tanzania katika uamuzi wa kutafuta mwekezaji wa bandari la Dar es Salama. Pia, nawaunga Watanzania wote mkono wanaoomba kwamba Tanzania ijitahadhari na ihakikishe mikataba yote ya wawekezaji kutoka nje inalinda matakwa (yaani interests) za Tanzania kwanza, kwamba mikataba inaipa Tanzania nguvu zaidi ya mwekezaji yeyote kutoka nje na pia inahakikisha kwamba Tanzania inabaki na nguvu za maamuzi ya mwisho, (yaani veto power) katika bandari kama walivyofanya Wajerumani.
Dubai haiwezi kumpa mwekezaji yeyote kutoka Tanzania nguvu zaidi ya Emirati ya Dubai. China haiwezi kumpa mwekezaji yeyote kutoka Ujerumani nguvu zaidi ya China katika uwekezaji bandarini China. Waarabu wanalinda mali yao sana. Wachina wanalinda mali yao sana. Wajerumani wanalinda mali yao sana sana sana sana. Waafrika lazima tulinde mali yetu pia sana sana sana sana sana sana sana sana.
Bana e. Kiswahili changu ni cha Kenya jamani ndugu zangu nawaomba munisamehe kama nimekosea hapa na pale ila natumai mumeliewa kwa umbali jambo nililotaka kuwaambia.
Ni wajibu wetu kuilinda Afrika Mashariki pamoja. Nyie ni ndugu zangu na ninawapenda sana.
Maana nimewaandikia baruapepe hii. Nawaomba nisalimie Mama Suluhu na nawaombea awaletee suluhu na suluhu ile iwe yenye baraka. Nawaombea kher ya mwenyezi Mungu.
Mnisamehe kama nimeingilia mambo ya ndani nchi yenu, ila rafiki mwema ni yule akwambiaye ukweli kwa kukutizama machoni. Rafiki wa kweli hakusemi kichinichini hata mwenyezi Mungu hapendi hivyo.
Salamu nyingi kutoka Berlin.
Ni mie wenu awapendaye,Mwalimu John Njenga Karugia