Ujumbe wa JWTZ kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba

Ujumbe wa JWTZ kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba

Status
Not open for further replies.
Amekwenda kuandaa jeshi la ukombozi wa Tanzania kutoka mikononi mwa mafisadi. Tunamshauri aanze kusajiri vijana tuko tayari

Utakuta uko norway mkuu! Si wa mipakani tumetulia kimya.
 
Ulitaka wakuambie kaondoka na taarifa nyeti?????

Huyo msemaji wa jeshi nikama ----- flani vile, mtu wa cheo kikubwa vile usema hajaondoka na taarifa yoyote?

Inamaana hata mikutano yao ya kijeshi mikakati na mambo memgine huyu mtaalam wa IT hakuwa akishiriki?

Watanzania tumekuwa watu wa kuishi kwa uwongo na propaganda siku zote, ukweli hatuwezi kuusema
 
Sasa kama hajatoroka kaenda wapi? Nyaraka sio mpaka aondoke na makaratasi. Kama mtu alikuwa IT lazima anajua siri za jeshi nyingi sana. Taka ustake IT department ndio roho ya organizani/ taasisi yoyote. IT expert, nyaraka ni ubongo wako na so makaratasi. Kwa hyo huyu msemaji wa jeshi hajui analo ongea.
 
Kiusalama nafikiri si busara JWTZ kukiri kuwa kaondoka na nyaraka muhimu, nafikiri statement waliyotoa kwa public kwa sasa ni sahihi wakati wakilifanyia kazi jambo hili, hili si jambo la kushare na public
 
Luteni kanali unatoroka jeshini. Hii hatari court marshall inamsubiri.
 
Ulitaka JWTZ watangaze tena kupitia vyombo vya habari kuwa NI KWELI SEROMBA KATOROKA NA NYARAKA? Akili za kuambiwa changanya na zako!
 
Sasa kama hajatoroka kaenda wapi? Nyaraka sio mpaka aondoke na makaratasi. Kama mtu alikuwa IT lazima anajua siri za jeshi nyingi sana. Taka ustake IT department ndio roho ya organizani/ taasisi yoyote. IT expert, nyaraka ni ubongo wako na so makaratasi. Kwa hyo huyu msemaji wa jeshi hajui analo ongea.

Ndugu yangu nji ngumu hii! Nyaraka wanadhani ni makaratasi. Mchizi nasikia kasepa na database ya kutosha.
 
Bramo unamtangazia nani sasa? kama alikufundisha monduli so what? au ndo tukujue wewe kuwa ni mjeda? au ndio wanajeshi wa dot com.nyie? Bora uje uraiani tupige siasa kuliko huko ulikopelekwa na baba ako
 
Tanzania Daima Jumapili limekariri msemaji wa JWTZ akikiri kuwa ni kweli mwanajeshi ametoroka lakini tayari alikuwa chini ya uchunguzi na alikuwa amekabidhi vitu vyote muhimu.

Pia ameongeza kuwa hakuwa kiongozi wa kitengo cha IT bali alikuwa tu mkufunzi wa computer na kwamba kama alikuwa na taarifa zozote basi alikuwa ni za taarifa tena za wanafunzi wake.

Soma zaidi: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=53169

JWTZ yakanusha ofisa wake kutoroka na nyaraka

na Abdallah Khamis

-
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi juu ya kutoroka kwa ofisa wa jeshi hilo, Luteni Kanali Colestine Serombe na kusema kuwa ofisa huyo hakufanikiwa kuondoka na nyaraka yoyote muhimu ya jeshi hilo.

Mbali na kusema Luteni Kanali Serombe hajaondoka na nyaraka muhimu za jeshi hilo, pia wamesema ofisa huyo aliyetoroka ni Mtanzania na kwamba kabla ya kuroroka alikuwa akikabiliwa na tuhuma dhidi ya makosa ya kijeshi.

Jeshi limelazimika kutoa kauli hiyo baada ya baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kusema kuwa ofisa huyo aliyetoroka ni miongoni mwa maofisa wachache walio na asili ya Rwanda ndani ya jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa jeshi hilo, Meja Erick Komba, alisema Luteni Kanali Serombe alizaliwa katika Kijiji cha Rukira kilichopo mkoani Kagera na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Rukira kabla ya kwenda sekondari za Rulenge na baadaye Minaki alikosoma kidato cha tano na sita.

“Ametoroka usiku wa Desemba 17 kuamkia 18 mwaka jana baada ya kuwa na makosa ya kijeshi …tulimuweka chini ya uchunguzi kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, sasa labda hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya kutoroka kwake, kwa kuwa suala la utoro ni uamuzi wa mtu kama ambavyo wengine wanaamua kujiua wakiwa na sababu zao,” alisema Meja Komba.

Kuhusu madai kuwa ofisa aliyetoroka alikuwa mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano, Meja Komba alisema hilo si la kweli na kwamba Luteni Kanali Serombe alikuwa ni mkufunzi wa wanafunzi wa kijeshi wanaosoma masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT).

Alisema kulingana na cheo cha Luteni Kanali Serombe na madaraka aliyokuwa nayo alikuwa na uwezo wa kusoma baadhi ya taarifa ambazo zilimfikia kwenye ofisi yake kwa ajili ya utekelezaji au kwa taarifa.

“Katika kipindi chake cha utumishi kwa muda mrefu alikuwa mkufunzi wa masomo ya kompyuta katika kituo chetu, kwa mantiki hii taarifa nyingi alizokuwa nazo zilikuwa ni zile za wanafunzi, yaani mahudhurio, matokeo na nyingine zinazomhusu mwanafunzi,” alisema Meja Komba.

Aliongeza kuwa jeshi lilipoanza uchunguzi dhidi ya makosa ya Luteni Kanali Serombe kitu cha kwanza kilichofanyika ni kuhakikisha anakabidhi vitendea kazi vyake vyote kwenye uongozi, huku akibainisha kuwa walichomwachia ni elimu aliyonayo.

“Labda sasa anaweza kuitumia elimu hiyo huko alikotorokea kufungua chuo cha kompyuta na wananchi wakapata ujuzi huo,” aliongeza Meja Komba.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Naona wanajaribu kufanya kazi yao
yaani kuuficha ukweli ili kuzuia panic na sintofahamu miongoni mwa wananchi huku wakiwa wahanga wa kuumia na ukweli ambao ni mchungu ndani ya mioyo yao
 
Hii nikama kufanya propaganda.

1. Mkufunzi - mtaalamu wa IT

2. Luteni Kanali - level ya kujadili mikakati, kuplan na kufanya maamuzi ya kimkakati.

Haya mambo mawili yanatosha kumfanya huyu jamaa kuondoka na kila aina ya taarifa nyeti alizozihitaji

Mkufunzi wa IT, hii inamaana kwamba alipokuwa akifanya kazi huyu jamaa alikuwa akifanya pia consultation.......

Kama hiyo haitoshi, katika maofisi ya wakubwa wenzake lazima alikuwa akiwasaidia pale walipokwama nk

Lt kanali

Hapa huyu jamaa lazima amehudhuria mikutano ya kimkakati kama jeshi mara kadhaa na ya malengo tofauti.

Kukanusha kwamba hajaondoka na kitu chochote nikujitekenya na kucheka wenyewe, JWTZ linamdanganya nani........!!!
 
Uongo mtupu,mtu kaondoka december wakati wote walikua wanasubiri nini kutangazia wananchi?au ndio walikua wakifikiria gear yakuingilia wananchi? inawezekana hata hizo hasira za pk zilitokana na information alizopewa na huyo kanali,kwani inajulikana tz walikua na mpango wa kuivamia rwanda wakipitia congo,mmh basi tusubiri kwani simuda mrefu ukweli utajulikana.
 
Hii nikama kufanya propaganda.

1. Mkufunzi - mtaalamu wa IT

2. Luteni Kanali - level ya kujadili mikakati, kuplan na kufanya maamuzi ya kimkakati.

Haya mambo mawili yanatosha kumfanya huyu jamaa kuondoka na kila aina ya taarifa nyeti alizozihitaji

Mkufunzi wa IT, hii inamaana kwamba alipokuwa akifanya kazi huyu jamaa alikuwa akifanya pia consultation.......

Kama hiyo haitoshi, katika maofisi ya wakubwa wenzake lazima alikuwa akiwasaidia pale walipokwama nk

Lt kanali

Hapa huyu jamaa lazima amehudhuria mikutano ya kimkakati kama jeshi mara kadhaa na ya malengo tofauti.

Kukanusha kwamba hajaondoka na kitu chochote nikujitekenya na kucheka wenyewe, JWTZ linamdanganya nani........!!!

Mkuu ulichoandika kina maana sana.

Sijui km wana jeshi wetu wana akili gani za Jeshi, za CCM au Za Chadema..au za akina Kinje...Siamini km hawajui kuwa huyo jamaa wa computer no matter what alihitaji sana access kwa computer za ndani na network, halafu access ya compound za jeshi na mwisho access to human networking.Mengine ni time.

Wanajeshi wanaamini kuwa ktk art of espionage,intelligence ni lazima upewe mkononi ndipo uweze ondoka nazo?Sasa wangezifuata kwa nini?Habarai unazitafuta,unaziifuata, una pokonya, unaiba, unakamua ,unazificha ili mwenyewe asizione tena, una futa traces zote na una una potosha intelligentia ya wengine.

Mungu ibariki Tanzania.I have all the reason to believe that my fellow Tanzanians are first degree dumb ass....baadaya kilio yatakuwa busy kulaumiana tuu ktk irriversible things.Hakuna Agency, wana mdanganya nani sasa?Kagame ambaya ana kila kitu alichokitaka au raia watakaoshuhudia kuanguka kwa nchi km maadui watafanikiwa?
 
Wanajeshi wanapokua wana siasa, haya ndio matokeo yake...
 
Kama alivyosema huyo msemaji ndiyo hivyo tu sasa kulikua na haja gani ya kuchukua muda mrefu kutoa statement?

Ukweli Mchungu ni kuwa kwenye kitengo cha propaganda za kijeshi kuna ombwe.Walichofanya ni rahisi hata kwa mtu ambaye ni illiterate kugundua upotoshaji

1:Inakuaje hata hawatangazi kumtafuta ikiwa makosa hayo yalikua serious hadi akaamua kutoroka?

2:Je,wana uhakika gani kuwa hakuiba nyaraka maana ujasusi ni kujua mipango na mikakati na uwe mwepesi wa kumeza au kufanya chochote kulinda data hata kwa code za siri.Sio kazima unyofoe faili

3:Je,wanafunzi wake aliowafundisha ambao ni watiifu kwake waliosambazwa idara mbalimbali ndani ya jeshi kwenye vitengo nyeti hawakumpa taarifa?Maana kama unajua mission yako ya kijasusi inatekelezwa step by step ni lazima ufanye maandalizi mapema na kujenga network itakayokurahishia kupata taarifa zozote unazohitaji while hiding you dangerous intentions.

4:Je wanafunzi wake wanachunguzwa maana usikute huko alipo anaendelea kupata data hapo hapo.Na pia hajaeleza nature ya wanafunzi wake maana inawezekana hata mabrigedia walikua wanafunzi wake hasa wale wanaojiendeleza wakiwa kazini hivyo kujenga nao ukaribu na pia kuwasaidia kuhifadhi ku-access data kwenye kompyuta zao au ku-install software na kupata kila kinachoendelea maana 'Mwalimu' always ana authority na command kwa wanafunzi wake.

Pia kwenye strategic plans na malengo ya idara yake specifically kwa muda murefu atakua anajua pamona na weakness na strength.SWOT Analysis anaijua.

Jeshi liache utani huu mbaya labda kama wanafanya kazi ya uhakika katika covert operation!
 
Hili jina "Colestine Seromba" ni la mkoa gani? Anaweza akawa mtanzania lakini je ni Mtanzania halisi (wa asili kabisa?) au kawa naturalized? Anaweza akawa mnyarwanda ambaye aliomba kuwa raia. Naona hapa jeshi liwe makini tu. Sisi hatulituhumu ila wawe waangalifu tu. Amani ya nchi yetu iko "at stake" hapa!!!
Hayo yamesemwa na msemaji wa JWTZ Meja Erick Komba, na kwamba askari huyo mtoro Luteni Kanali Colestine Seromba NI MTANZANIA. Wakimpata hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake!

Source: ITV habari saa 2 usiku huu!

-------------------------------
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom