Mimi inanikera zaidi kwa hisani ya serikali ya ccm! Wakati pesa ni yangu na serikali ni lazima inunue ndege siyo hiari, eti ndege ya serikali ya ccm.Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.
Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.
Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.
UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...
"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"
Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.
Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.
Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.
Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?
Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?
Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?
Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?
Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?
Karibuni kwa mjadala.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Ni aibu kubwa kuendelea kupokea misaada hata ya uzazi was mpango.Tuna rasilimali nyingi name zinaporwa kwa faida ya viongozi wachache.Tumeikumbatia Ccm tangu uhuru ambayo imepoteza mwelekeo.Wanachofanya sasa ni kuua vyama vya siasa na kuua vyombo huru vya habari.Nchi imekuwa ya kidikteta.Tanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
jingalao umezaliwa liniTanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
upo sawa lakini China ameweka sharti kuwa viwanda vyake vyote vilivyopo Marekani, Emirate, (Dubai) Tanzania huko Vingunguti, Kunduchi hata Bagamoyo lazima vioneshe ni watu wa ChinaHakuna msaada usiokuwa na malengo. Ukitaka kuwa huru usiombe wala kupokea misaada kwakuwa inakufanya kuwa mnyonge
made in china au made in USA sio mbaya kwani hilo ni tangazo la kibiashara kabisa.upo sawa lakini China ameweka sharti kuwa viwanda vyake vyote vilivyopo Marekani, Emirate, (Dubai) Tanzania huko Vingunguti, Kunduchi hata Bagamoyo lazima vioneshe ni watu wa China
angalia bulb na vifaa vya majumbani vimeandikwa Made in PRC (People Repulic of China) na hiyo bulb ya energy save inawaka chumbani kwako, angalia simu zetu za Nokia
lakin tunalaum misaada
si misaada jamani hata vyupi boxer na sidiria Made in PRC
Unataka kutueleza kuwa baada ya kuandika hivyo kumekuwa na hamasa ya watu kulipa kodi?Huu ni uongo wa mchana kweupe.Kilwa Road waliandika maneno makubwa wale Kajima wakisema "...kodi za watu wa Japan " lengo nadhani ni kuwahamasisha wananchi walipe kodi kama wenzao hao "watu" wa Japan au Marekani ili nasi tuweze kujitegemea.
Nina hakika wewe bado mtoto! Miradi yote tunayofadhiliwa ni lazima kuwe na acknowledgement kwa mfadhili!Ni sharti linalolenga nini haswa?
Uzalilishaji wanataka wajikute wao ndio watoaji wakubwa wa misaadaTanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
Aisee Jingalao hilo siyo sharti ni ukweli na uwazi !!!!!Ni sharti linalolenga nini haswa?
Wanatofautisha misaada yao na ya Kichina .................!!Tanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
Sawa lakini waambie maccm wenzio watutumie hazina ya taifa kwa vitu vyenye Tija. Unawezaje kutumia tril 1.5 kuua upinzani alafu, ukachukia msaada wa shimo La chooni kwa hisani ya watu wa marekani?Habari za jioni wadau.