Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

"From third world to first world" ni kitabu kinachoonyesha Singapore walivyopambana kujinasua kutoka katika umasikini mkubwa...naona viongozi wetu wakisome hiki kitabu kwa lazima...nani aliyeturoga Waafrika???au hatuna akili kama wanadamu wengine??miaka 57 ya Uhuru ilitosha kuwa na uchumi mkubwa kupita hata baadhi ya nchi za Asia.. tuna wasomi wa kweli au wafoji vyeti na wababaishaji tu..amini nawaambia vizazi vijavyo watafukua makaburi yenu na kudhalilisha mabaki yenu na vizazi vyenu..maana mtawaachia umasikini ambao dunia haijawahi kushuudia...
 
Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.

Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.

Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.

UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...

"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"

Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.

Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.

Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.

Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?

Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?

Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?

Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?

Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?

Karibuni kwa mjadala.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Mimi inanikera zaidi kwa hisani ya serikali ya ccm! Wakati pesa ni yangu na serikali ni lazima inunue ndege siyo hiari, eti ndege ya serikali ya ccm.
 
Tanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
Ni aibu kubwa kuendelea kupokea misaada hata ya uzazi was mpango.Tuna rasilimali nyingi name zinaporwa kwa faida ya viongozi wachache.Tumeikumbatia Ccm tangu uhuru ambayo imepoteza mwelekeo.Wanachofanya sasa ni kuua vyama vya siasa na kuua vyombo huru vya habari.Nchi imekuwa ya kidikteta.
 
Hakuna msaada usiokuwa na malengo. Ukitaka kuwa huru usiombe wala kupokea misaada kwakuwa inakufanya kuwa mnyonge
 
Tanzania imepokea misaada toka ilipopata uhuru kwa nini maneno haya yamekuja miaka hii ya karibuni?
jingalao umezaliwa lini
Marekani imetuletea unga wa buruga, maziwa, ngano, unga wa mahindi ya njano wakati wa njaa na kulikuwa na label km hizo na picha ya mikono inayoshikana (km kusalimiana) yote iliandikwa "kwa hisani ya United State sasa wewe tafsiri ya kiswahili ndio huitaki
Ukiona madaraja ya barabarani yameandikwa Made In China, UK au SA
 
Je, kuna sheria yoyote inayotaka ndege yetu iandikwe "HAPA KAZI TU"..? Je, kulikuwa na ulazima gani kuandika maneno hayo?

Wananchi wa Tz watapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?
 
Hakuna msaada usiokuwa na malengo. Ukitaka kuwa huru usiombe wala kupokea misaada kwakuwa inakufanya kuwa mnyonge
upo sawa lakini China ameweka sharti kuwa viwanda vyake vyote vilivyopo Marekani, Emirate, (Dubai) Tanzania huko Vingunguti, Kunduchi hata Bagamoyo lazima vioneshe ni watu wa China
angalia bulb na vifaa vya majumbani vimeandikwa Made in PRC (People Repulic of China) na hiyo bulb ya energy save inawaka chumbani kwako, angalia simu zetu za Nokia
lakin tunalaum misaada
si misaada jamani hata vyupi boxer na sidiria Made in PRC
 
made in china au made in USA sio mbaya kwani hilo ni tangazo la kibiashara kabisa.
sasa unapojinadi kusaidia wajawazito na kuweka maneno kwa hisani ya watu wa marekani inaleta tafakuri kuwa mama zetu ni kama vile wamebeba mimba kwa hisani ya watu wa marekani.
 
Kilwa Road waliandika maneno makubwa wale Kajima wakisema "...kodi za watu wa Japan " lengo nadhani ni kuwahamasisha wananchi walipe kodi kama wenzao hao "watu" wa Japan au Marekani ili nasi tuweze kujitegemea.
 
Unataka kutueleza kuwa baada ya kuandika hivyo kumekuwa na hamasa ya watu kulipa kodi?Huu ni uongo wa mchana kweupe.
 
Mleta uzi utakua bado mchanga sana...
Wewe utakua ata redio umeanza na FM....sio AM.
Tungu kuanza kupokea msaada kwa Afya nk maneno ayo yalikua yanatangazwa. Lakini pia ata sisi ccm tukifanya jambo mfano ..ujenzi wa bara bara katika ufunguzi tunasema kuwa imejengwa msaada wa Japan au Marekani.
Angalia ata kwenye mabango ya miradi utakuta kumeandikwa na kuchora nembo ya nchi iliyotoa msaada...mfano JICA,OXFAM,GTZ,USAID,EU nk.
 
Ni sharti linalolenga nini haswa?
Nina hakika wewe bado mtoto! Miradi yote tunayofadhiliwa ni lazima kuwe na acknowledgement kwa mfadhili!

Na hii imesaidia sana kwani ccm hawachelewi kusema uongo kuwa wametumia fedha za magufuli as if ametoa mfukoni mwake kumbe ni kodi zetu!
 
nikiitizama ID yako nikiitizama pia Avetar yko nikioanisha na maandishi yako

napata jibu kuwa nyinyi ni aina ya watu mnaopatikana Tanzania tu
 
Si kwasababu tuna mazwazwa serikalini,wewe badala ya kusaidiwa meli za uvuvi,mitambo ya kuchimba madini,matrekta ya kilimo unasaidiwa vyoo!!!
 
Ni kujidhaliisha wenyewe, unapokeaji msaada wa 5 milion huku Jiwe akililiwa shida na wapiga kura wake anawajaza minoti
 
elewa unatumia pesa isiyo ya kwako hizo ni kodi za watoa kodi wa USA!!!
 
Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.

Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.

Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.

UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...

"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"

Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.

Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.

Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.

Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?

Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?

Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?

Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?

Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?

Karibuni kwa mjadala.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Sawa lakini waambie maccm wenzio watutumie hazina ya taifa kwa vitu vyenye Tija. Unawezaje kutumia tril 1.5 kuua upinzani alafu, ukachukia msaada wa shimo La chooni kwa hisani ya watu wa marekani?
 
Back
Top Bottom