Mara zoteUkweli mchungu lazima.CCM wanune
Sio Wizi wa kura tu, ni aina zote za wizi
Mkubwa wao atakuwa jikoni anaandaa script mpyawale wakatoliki feki waende tena wakamshitaki maana amezungumzia wizi wa kura.
Hii sio ya leo.Huyu mzee si aamue tu kuingia kwenye siasa tujue kuwa ni mwanasiasa na sio mtumishi wa Mungu.
Ili anapojibiwa apate treatment ya wanasiasa wenzake,
Na sio kujificha kwenye dini na kuzua taharuki kila anapotoa statement.
Yeye ni mtumishi wa Mungu kama kuna jambo lolote uwanja wake ni kwenye madhabahu.Hii sio ya leo.
Lakini jibu hoja yake, akina Lisu mbona wanayasema hayo pia mnaishia kuwafunga.
Jibuni hoja zake, kama kweli hamuibi kura.
MKuu,Yeye ni mtumishi wa Mungu kama kuna jambo lolote uwanja wake ni kwenye madhabahu.
Hizi podiums za kisiasa ni kuchanganya mambo na kutuchanganya sisi tunawategemea viongozi wa kidini watuongoze kiimani.
Yeye anaweza akaona anatumia uhuru wake ila misimamo yake kisiasa inaeweza wakwaza kondoo wake anaowaongoza.
Wakati nakua sikuwahi sikia kiongozi wa dini anafanya siasa.
Hawa wa sasa wanaona madhabahu haziwatoshi acha wajaribu na kwingine.
Ni vyema akachagua madhabahu au podiums za kisiasa.
Akibakia hivyo analeta taharuki ambazo hazina ulazima sana.
Hayo maneno kayazungumzia akiwa wapi?MKuu,
Kwani amekiombea kura chama fulani kuwa kitaleta maendeleo.?
Amekemea wizi wa kura, ambayo ni dhambi sawa na wizi wa mali nyingine.
Kura hazipigwi kwenye siasa tu, maeneo mengi zinatumika ili kufikia maamuzi fulani ya wengi.
Sasa ukiiba huoni kuwa unatenda kosa?
Anazidi kukipokocha kidonda kibichi😀