MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ni kweli wamefeli form four, wamepata four na zero.... kabla ya kuwalaumu tujiulize tulifanya jitihada gani kupunguza tatizo. Tuliwaonya walipokuwa wanakosea? Tuliwashauri? Tuliwasaidia mahitaji yao ya kishule kama Ada na mengineyo? Hatukuwatumikisha kazi zetu bila kujali umri wao na ratiba zao? Tulipambana vipi kuwaepusha na wale mafataki/shugamami? Unavyoishi wanakutazama kama kioo cha mambo mema au unawahamasisha kupotea zaidi? ..... Kila mmoja ana nafasi yake katika ufaulu wa wanafunzi. Jisikie kugusa maisha yao ili kupata Tanzania bora ya baadae.