Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mwanakijiji

Augustine Moshi

jokaKuu

Mie naona wewe ndio hujibu maswali na unapindisha hii mada kwa kurukaruka. Nimeuliza swali hili ukurasa wa 39 mpaka sasa hivi hakuna jibu. Naweka hapa kwa kifupi tena.
Fungueni macho muone jinsi mnavyofanya argument kikabila. Nimeuliza swali Mmanda anaposema tusishangae TRA twende jeshini kwanza. Ana maana gani? Mbona hamtaki kuliongelea hili? Nafikiri ni nyinyi tu ambao mtapinga kama kuna ukabila Tanzania.


http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=39

Maneno mnayotumia ni ya kutisha watu ili waogope kujadili ukabila ambao unaendekezwa na wakabila wachache tu katika baadhi ya sehemu za serikali. Je tusiongelee hili kwa sababu ni taboo? mnaogopa kitu gani ili lisiongelewe? Kwa nini mnataka ukweli ujifiche? Wanabodi wengi hawachangii hii mada kwa sababu inawagusa na wanafahamu ukweli kwamba ukabila upo lakini wale kwa njia moja au nyingine wanaona ni afadhali usijadiliwe kwa nini hasa? watu wamechomewa hata nyumba nyie hili hamlioni? Au kwa sababu aliyechomewa nyumba sio mtanzania wa kabila lenu? James Mbatia ameajiriwa bila cheti na qualification zinazotakiwa je ni mazingira yapi yalitumika au kwa vile ni mchaga?

Tatizo hili lipo na linatakiwa kufanyiwa ufumbuzi hata kama sio leo ni lazima litatuliwe. Hata nchi za ulaya na marekani na kwingineko wanaweka taratibu kuona hili halitokei. Sisi Tanzania mnataka watu tuamini kwamba ni malaika.
 
DR.who.

mimi simbishi na nimempa Facts nyingi tu. ila Phillimon uongo ni jadi yake na sasa anadai TIC ni KDF JEE Chadema ni CUF? kwa vile malengo yanafanana? vyote ni vyama vya upinzani.

amekwama vibaya, MAJINA aliyotuletea ya washika mapembe nimeyachambua yote,

naanda misamaha ya kodi na ushuru inayotolewa kwa minajili ya kikabila na kwanini Mengi amekwepa kulipa Billion 5 kama kodi na TRA.

NA deni la Mfanyabiashara mzee TANGO Billion 3 kwa TRA amezimwa kwa vile si mchagga.


Sawa lakini nadhani kuwa you can do better than kubishana naye

wewe piga mwaga issues kisha wasomaji watamake up ni nani anayesema ukweli

ulianza izuri lakini hapo kati kati ukaingilia sisa za kubishana

wewe kata issue sababu nimegundua kuwa uwezo huo unao lakini sijui saa zingine inakuwaje

ndio maana ninakuomba utuambie na Benki kuu,ikulu,fedha na usalama wa taifa kukoje?
 
[color=4]Baadhi ya wachangiaji wanaona chuki aliyonayo Mswahili kwa wachaga [/color]lakini hawaoni ukweli wa ukabila unaotumiwa na baadhi ya wachaga
 
Mwl. Augustine,

Shukran kwa mchango wako ambao kidogo umeuacha wazi. Nafikiri umeuacha wazi kwa sababu huko zako.
Bcstimes niliwahi kueleza kwa kirefu sababu za kusema serikali inatakiwa kuanzisha hizo development foums. madai yako ya kwamba hii ni kazi ya wananchi wenyewe hakuna haja ya kusubiri serikali, mzee wangu kidogo unapotosha.
Serikali ndiye mpanga policy za biashara zote na serikali lazima ivitambue hivi vyombo ambavyo vitaubdwa kwa ajili ya wananchi. Mzee wangu huu ni wakati wa mwanzo mpya kutafuta TRUTH from the FACT kama walivyosema wenzetu Wachina - To seek Truth from the Fact wakati walipoanza zoezi la mageuzi ya kiuchumi. Sijui kiswahili chake labda niseme Kutafuta 1. HAKIKA toka ktk MAMBO ya WAZI. au 2. Hakika toka ktk Ukweli.
Anyway hata sielewi, nahitaji msaada wa darasa la lugha hapo.
Kilimanjaro Development Forum ni matunda ya Economic zones na sielewi kwa kiwango gani imepata baraka za serikali ktk Umilikaji, uwekeshaji, imports na Exports, kodi, na hata matumizi ya ardhi na mipaka yake.
Wakati madini yapo chini ya wazawa mikoa ya kaskazini, dhahabu ktk mikoa ya ziwa imepewa wawekeshaji tena kwa nguvu na mabavu. Vyombo vya wachimba migodi sehemu hizo havitambuliwi na ilifikia hadi wananchi wa Bulyanhulu kuuawa. You know why? kwa sababu hakuna sheria inayowabana serikali ktk madaraka ya uchumi wa nchi!...hakuna mwongozo wa swala hili ila wenye nguvu ndani ya serikali ndio wenye maamuzi. Which bring us back kwenye hii mada.

Ndugu Augustine ni muhimu kuwepo na mwongozo wa kitaifa wenye malengo yaliyo wazi kwa wananchii wake. Uwazi wa policy na uundwaji wa vikundi kama hivi ni muhimu kuwepo na ushirikiano wa moja kwa moja na serikali kuu. Misaada inayotolewa kwa wakulima toka Benki zetu, serikali ama nchi za nje ni lazima iwe na mwakilishi kama huyu badala ya kutumia majina ya watu binafsi ambao hawana historia ya uchukuaji mikopo (Credits History). Hili moja na muhimu sana.
Mzee wangu kuna document fulani najaribu kuiandika - kazi ni kubwa sana ila tu nitakudokeza ya kwamba Tanzania tumepoteza DIRA! hatufahamu tunakokwenda kwa hiyo hata kama tutapiga kasia kwa nguvu za ajabu tutakuwa kweli tukisonga mbele lakini none of us knows where we heading! hii imekuwa kama imani ya dini ambayo malipo yake yatajulikana ukisha KUFA...None of us knows the truth!
Mzee Augustine huna dira huna safari, Lazima kuwepo na formation ya upigaji kasia sio kila mtu anapiga zake kuelekea anakotaka yeye, Nahodha lazima awe mjuzi wa kuongoza mashua na kinachotangulia yote ni kuwepo na dira ya kule mnakoenda. Tanzania na nchi zote za kiafrika hatuna dira, mashua zetu mbovu, Manahodha hawajui tunakokwenda ila inasonga mbele kwa nguvu za mkondo (current) wa maji World Trade Organization (WTO.)
Na kibaya kuliko yote sisi wote tunatazama nguvu ya maji ya WTO na kumwomba Mungu atufikishe salama huko current hii inakoishia. JK na viongozi wengine wote wanachojaribu kufanya ni kuhakikisha chombo hakipinduki...
Nachosema mimi Mkandara ni kwamba umefika wakati wa kusema - Noo stop! Hatuwezi kila siku kuwalaumu wazungu ikiwa sisi wenyewe tumeshapoteza dira ambayo ingeweza kutupeleka kule tuliko kusudia toka Uhuru wetu.
Mzee Augustine, haiwezekani hata siku moja kutegemea dira toka mashua ama meli nyingine iliyoko Pacific kuongoza mashua ama Meli iliyoko Indian Ocean hata kama vyombo vyote hivi vipo baharini, simple Logic...
 
Augustine Moshi.

sijatangaza chuki kwa wachaga wote. tizama vizuri nimekuwa nikimfagilia Tenga kama mtu makini si mara moja wala mbili.
au Tenga nae si mchagga? hakuna excuse hapa ni ukabila uliopo TRA.

Mwanakijiji.

najua wewe una lako mie siwezi kushughulika na wewe. nakuuliza vipi kuhusu mchango wa maiti wa TOBI? kijana aliyefia Brazil? tunajua wewe ni sehemu ya network hiyo ndio maana umekuwa ukitetea uovu TRA. soon tutaweka mtandao wa wauza madawa ya kulevya waliopo nje ya TZ. nitapita kote Holland, uswizi,America ya kusini, marekani, uk, uturuki,brazil tena sao paul, ugiriki na njia ya irani.
suburini zamu yako. hapa huwezi.
 
Mkandara,
Kwa maneno machache naomba nikuunge mkono kauli yako.Serikali inayo wajibu wa kuhamasisha development forums. Hivi sasa serikali yetu iko bize kuwatafuta wawekezaji kutoka kila kona ya dunia. Nguvu kama hiyo hiyo ingepaswa ielekezwe kwenye juhudi za kuleta maendeleo vijijini.
 
Mwanakijiji.

najua wewe una lako mie siwezi kushughulika na wewe. nakuuliza vipi kuhusu mchango wa maiti wa TOBI? kijana aliyefia Brazil? tunajua wewe ni sehemu ya network hiyo ndio maana umekuwa ukitetea uovu TRA. soon tutaweka mtandao wa wauza madawa ya kulevya waliopo nje ya TZ. nitapita kote Holland, uswizi,America ya kusini, marekani, uk, uturuki,brazil tena sao paul, ugiriki na njia ya irani.
suburini zamu yako. hapa huwezi.

wow.... I like your facts.. sasa mimi ni muuza madawa ya kulevya.. haya wenye kumuunga mkono Mswahili jitokezini kawapa fact!!
 
Mzee mwanakijiji,

Heee! heee hee!
Ikiwa fact zenyewe ni pamoja na picha ya shamba lako la madawa unalotangaza kila post yako!..
Kumbe ndio maana huwa unadai Ukulima ni kazi pia!
 
Nadhani watu sasa wanaanza kutafuta id za watu kwa kuwa personal au kuzusha mambo ili mtu ajianike wazi kupinga.
 
Nimeangalia tena ile picha ya shamba la Mwanakijiji. Mimi nilidhani ni mahindi, kumbe? he!he!he!
 
Mswahili, uje ulete ushahidi wa mimi kujihusisha na madawa ya kulevya ama sivyo nitake radhi! Hoja zikishindikana wanashambuliwa watu.. its not worthy it!!
 
Kwanini watu msikubali tu kukubali kutokukubalina,Huko mnaenda wapi tena?Mnazidi kupoteza muelekeo,Nilitamani ni pumzike lakini bado sijaamini kinachotaka kutokea kwenye hii Forum! Haya penye ukweli uongo hujitenga!
 
Augustine Moshi.


Mwanakijiji.

najua wewe una lako mie siwezi kushughulika na wewe. nakuuliza vipi kuhusu mchango wa maiti wa TOBI? kijana aliyefia Brazil? tunajua wewe ni sehemu ya network hiyo ndio maana umekuwa ukitetea uovu TRA. soon tutaweka mtandao wa wauza madawa ya kulevya waliopo nje ya TZ. nitapita kote Holland, uswizi,America ya kusini, marekani, uk, uturuki,brazil tena sao paul, ugiriki na njia ya irani.
suburini zamu yako. hapa huwezi.

This is not the spirit of this forum. It is 100% wrong to make such huge and yet unsubstantiated allegations. Hiyo ni mbaya sana sana, hizo ndio chuki zenyewe ati.

Mwanakijiji: Pole sana with this. Take a big heart, let it not hold you back from fulfilling your duty-the call to serve and to be the voice of voiceless!
 
Mswahili

We kweli unaweza kuchekesha watu na mwingi wa habari, hivi ulifanya kazi kwenye P.I.G. ya Tanzania? Maana hii iliyotoka Russia ilitaka kutuingiza mjini hapa lakini imekuta kuna wakali.

MKJJ

Turudi kwenye issue ndugu yangu hayo ni mazungumzo baada ya habari naona wengi tulikuwa tuko serious sana na Mswahili mwenyewe atasema hivyo.

Wanabodi

Hebu turudi kwenye serious issue ya ukabila ili tuweze kujua jinsi ya kuumaliza na kama wenzetu wanaotupinga wameona mwanga kidogo au wajibu hizo hoja hapo juu. Halafu tuendelee Ikulu, Foreign na kwingineko. nchi yetu inatunitaji.
 
Dua,
Hivi kweli watu waliamini kuwa Mwanakijiji ni muuza unga?...
Wanabodi, jamani msitufanye sasa hata sisi tunaopinga TRA kuwa wajinga. Tunajua kinachomsukuma Mswahili kusema yote yale na mimi naamini kabisa he (Mwanakijiji) has some interest kutokana na majibu yake. hatupo kortini hapa ila hoja hujibiwa kwa hoja na mara nyingi Mwanakijiji amekuwa akikwepa hoja kwa kuzusha hoja nyingine wakati anachoombwa ni kidogo sana!...

The call to serve and to be the voice of voiceless!...

Thanx Mwanasiasa.
 
Unajua hii forum tunaanza kuwa na double standard kuhusu nani amesema, Mswahili ametukanwa weee kutokana na msimamo wake lakini hakuna aliyesema kitu, sasa naona tayari ameanza kusakamwa kwa kitu ambacho sidhani hata kama ndicho alichokisema,

Sasa ninajua kwa mwendo huu, ataishiwa kutishiwa na kwamba amepewa hela na CCM, na kwamba antumiwa, nakwamba hata baba yake anafahamika ni nanni,

Mzee Admin, na moderators wa hii forum, kwa mara ya kwanza toka niiingie hii forum ninaanza kuwa na wasi wasi na hizi tabia, kuna mambo wakisema hakuna maneno lakini ukijibu tu basi mada zinafutwa, watu wanawazushia wengine hapa maneno ya kitoto lakini hakuna noma,

Je kuna agenda zipi hapa, mana huenda unaanza kufika wakati inabidi muachiwe hii forum, forum iko upande mmmoja hii WHY?
 
Hapa hoja hujibiwa kwa hoja, mapigo kwa mapigo. Mswahili katoa points zake na PM naye anatoa points zake. Sijaona uelemeaji wa upande mmoja mpaka lilipoibuka hili la Mwanakijiji na madawa ya kulevya. Tusianze kutishiana na kusingiziana mambo ya upendeleo. Anachofanya moderator, au anachopaswa kufanya ni kuhakikisha kwamba mijadala inaendelea kwa kuzingatia kanuni tulizojiwekea wenyewe. Not too personal na tuache matusi. I think that is fair na mpaka sasa let us stick to the points. Personally kuna mengi nimejifunza katika mada hii. Tuiache iendelee mpaka its own logical conclusion.
 
"Tusianze kutishiana na kusingiziana upendeleo" exactly una mmaana gani? niliyesema ni mimi siko mbali na nimesema kutokana na ninayo yaona, mana inaonekana ni vyema kwa some kwenda personal na sio sawa kwa wengine,

Sasa hiyo ndio ninayoiona, usinilazimishe nione tofauti bro!
 
Back
Top Bottom