Duuh!! Mara ya kwanza nili-give up kusoma hii thread baada ya kurasa 8 hivi. sasa nimejikongoja wee, mpaka nimemaliza. Sababu kubwa niliacha kusoma ni kwasababu niliona, ukweli ni kwamba ukabila upo (sana sana katika nyanja za mambo ya finance/pesa, ambayo ni area sensitive), kwahiyo nikaona hamna haja ya kubishana vitu ambavyo ni logic.
Tatizo linakuja ni watu kutofanya utafiti. mimi niko kempu ya Mswahili katika hii ishu. Ningependa nikubaliane na MKJJ kuhusu 'undugunisation', lakini ishu hii ni zaidi ya undugunisation. Mhe. PM kaja na list ya majina yake, lakini Mswahili alipo-rebutt, basi PM katulia. The fact is, watu wanaogopa kuongelea hii ishu ya 'ukabila' wakiogopa kuitwa 'hutus n tutsi' kiaina, kwahiyo wana-rely kwenye facts za Mswahili na PM, na nisengependa kusema zaidi, ila hapa nakubaliana na Mswahili (not only from his facts, but from my experience and what I know).
Ugawaji wa kazi upo na ulitendeka labda kutokana na legacy ya ukoloni au shortsightness ya Nyerere (au alipigwa bao? siju)? Lakini msisingizie waChagga walisoma zaidi (labda enzi hizo, lakini sio sasa kiasi kwamba watawale idara fulani fulani). Kwahiyo nina uhakika kabisa ukiangalia taasisi mbalimbali lazima utakuta kwamba makabila fulani yamejaa. So I wont waste my time kubishana ukabila haupo. Ndugu yangu PM, mimi msukuma, na nina ugonjwa na dada wa Kilimanjaro. Nategemea nikioa huko na mimi labda nitakuwa waziri wa nchi huko mbeleni hahaaa. Wewe mwenyewe PM, umesema mbona makabila mengine hayalalamiki (Sukuma, Nyamwezi etc). Ukweli ni kwamba watu wenye kisomo wapo, na sio kwamba hatuoni double standards. Sasa mimi naweza kuongea kama msukuma (lakini sina ukabila), najua kabisa Mwanza/Shinyanga (sukumaland) inachangia sana utajiri wa Tanzania, lakini maendeleo yake ni machovu, ukifananisha na mikoa ya kaskazini (na mchango wao katika taifa), na ingetakiwa tuwe-represented fairly katika nyanja muhimu (lakini kwa qualifications za mtu). Najua zamani kulikuwa na lobbysts wa nguvu sana (kina Bomani etc) na walisikilizwa sana, na kila mkoa ina lobbyst wao kwa interest zao kuvuta maendeleo (ndio mambo ya KDF hayo). Kwavile wewe ni Chadema, basi, mkileta mfumo wa majimbo, mbona mikoa ya kanda ya ziwa itawapiga bao? Sasa hii ni mfano mdogo wa kuonyesha ukabila upo katika National level mambo ya maendeleo. Mimi sio mkabila, mimi ni mtanzania, na chances are....nitaoa kabila nyingine (kama nilivyokwambia dada zenu nawapenda hahaaaaa).
Argument yangu sio kwamba kabila zingine zipewe posts undeservedly ili kupunguza kabila fulani, lakini katika mambo ya Finance TZ, pananuka fyuuu and we know it. Labda next stage, mmwulize Mswahili aende idara nyingine, kwani TRA ameshinda. Na nina uhakika akienda idara nyingine, atakutana na kabila fulani limetanda. Nasema haya kama mTanzania na kwa faida ya Tanzania, denying a problem exits is quite ignorant and potentially deadly. In the words of sijui nani........'Viongozi tupo na tumejaa teleee!!!'.
Wakati mkitafakari kutatua hili tatizo, kuna EAC inakuja. Hivi hii ishu si italeta matatizo makubwa zaidi?