Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Infwakti ningependa kujua shutma zinazoelekezwa kwa ukabila wa "Wahaya" maana za wachagga naona ziko TRA zaidi.

Enhe, wenye data za wahaya wameshikilia maeneo gani na wazimwage hapa ili tuanze kupata mwanga zaidi.

Baadae napenda kujua hao "Wanyakyusa" nao ni maeneo gani wameshikilia ***NYETI*** hadi waonekane ni 'Wakabila' au ni wachagga tu?

Yangu mie macho
 
Worm, Chuo Kikuu Dar, Wahaya wako wengi huko! tumeambiwa Jeshini wapo Wanyakyusa wengi... we have decided to break a principle and that principle will keep breaking us up!! Tukimaliza hayo matatu tuangalie Wapare wako wengi wapi...Wasukuma, n.k....
 
Worm, Chuo Kikuu Dar, Wahaya wako wengi huko! tumeambiwa Jeshini wapo Wanyakyusa wengi... we have decided to break a principle and that principle will keep breaking us up!! Tukimaliza hayo matatu tuangalie Wapare wako wengi wapi...Wasukuma, n.k....


Chuo Kikuu:

Mwanakijiji siamini; ila inawezekana kwa kuangalia orodha ya wahadhiri n.k lakini ukweli ni kuwa nina wasiwasi mkubwa wewe umeangalia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani (UDSM).

Vyuo vingine kama Muhimbili, UCLAS, DIT, Mzumbe n.k hujaviweka kwenye consideration? Ukiongea Chuo Kikuu basi huenda unamaanisha UDSM pekee. Hapo yawezekana, tukienda kwenye vyuo vingine nina wasiwasi mkubwa ukajikuta unaanza kuwabebesha Wachagga mzigo kama wa TRA.

Fuatilia hilo.

Jeshini:

Mwanakijiji are you serious? I do not believe it. Ngazi za juu tu (almost kama 10 hivi) sio? Kama ni jeshi zima basi inahitaji kutoa proof ya hicho usemacho as long as umesema Inasemekana.
 
Worm, chuo kikuu mlimani kimejaa Wahaya, Muhimbili kumejaa Wachagga... ni makabila yale yale.. it has to be conspiracy of tribalists
 
WANACHAMA WENZANGU,

binafsi sikuona huo utani katika haya madai ya KUUZA UNGA. sana sana niliyapuuza madai hayo kama yasiyokuwa na msingi wowote.

mara nyingi nimezungumzia "tone" , maudhui, na nia iliyojificha ktk mada tunayochangia.nimeeleza kwamba nia ya baadhi ya wachangiaji ni kuchonganisha baadhi ya makabila dhidi ya watanzania wenzao.

ndiyo, what is going on here ni character assasination. nitamvumilia mwanachama mwenzangu akiniita mjinga,kilaza,....lakini madai yake ni lazima yatokane na hoja na michango yangu, ktk forum hii. hili la kuuza unga lina-relate vipi na hoja tunazoongelea hapa?

vilevile ni lazima tukubaliane kwamba matani yana MIPAKA, na yanatofautiana UZITO. matani yakivuka mipaka na uzito yanakuwa MATUSI au KASHFA. yako maneno majina ambayo ukimuita mtanzania mwenzako basi moja kwa moja umemchonganisha na jamii nzima, MUUZA UNGA ni moja ya majina hayo.

PM,
wako wanaohalalisha matusi yaliyoelekezwa kwa mwanakiji kutokana majina uliyomuita mswahili. Muombe radhi mswahili kwa kumuita dish washer,....ili mwanakijiji naye atendewe haki hapa jamboforums.
 
Joka kuu !
Nia yako nzuri Lakini haya yameshapita na MKJJ AMESHASEMA LET bygones be bygones!
Huko ndiyo Kukomaa kwa wanaforum kwani wameacha tofauti zilizojitokeza na kuendelea na ukurasa mpya.
 
Ajabu sana Jokakuu kutazama wengine nia zao kisha wewe mwenyewe unarudisha vitu ambavyo vimesha patiwa ufumbuzi. Tumerudi ktk mada umeanzisha tena vagi lililokwisha tupwa kapuni.
Sielewi nini dhumuni lako kama sio kulendeleza kupotosha mwelekeo hapa!
 
Worm, chuo kikuu mlimani kimejaa Wahaya, Muhimbili kumejaa Wachagga... ni makabila yale yale.. it has to be conspiracy of tribalists


Nahitaji ushahidi wa haya, hapa kinachojadiliwa ukweli si kuleta chuki baina ya makabila bali kufikisha ujumbe kwa wakuu wa vitengo husika kuwa kabla ya kutoa ajira waweke kwenye 'consideration' mambo haya kuona hisia hizi za watanzania walio wengi.

Hii haijaanzia JF, hata Tanzania wengi wanalalamikia hili kwenye vyombo vya habari japo si huru sana. Lazima tuutafute ufumbuzi wa tatizo.

Binafsi naona kama mtu ana uwezo wa jambo flani na ana kila sifa ya kufanya kazi husika haijalishi ni mchagga wacha aajiriwe TRA.

Kuna watu wakileta CV zao zinatisha sana; wakti wa interview ndo unapogundua kuwa ni waandishi wazuri wa CV na wala hawawezi waandikacho.

Lakini lisemwalo lipo; lawama nyingi si za kupuuzia hata kidogo. Yes, nadhani tusiseme ukabila bali 'udugu' wa kupitiliza. TANROADS je pako shwari kweli? Hiki nacho ni kitengo kinachoibeba hela yetu walala hoi sana!

Soon tutapata data za kutosha na kufikiria kwa pamoja nini kifanyike ili kuondoa KERO hii ya 'udugu' uliokithiri katika utoaji kazi.

Bado nalia na wahindi/wachina wanaoleta 'ndugu zao' kujenga tofali Tanzania wakati tuna watanzania lukuki wanaoweza kazi hii. Hapa namaanisha na kazi anuwai zinazoshabihiana na hii.
 
Mkandara,
1.kumuita mtu muuza unga si sawa na kumuita dishwasher. inasikitisha unavyojidai ati huoni tofauti hapo.

2.ningekuwa nataka kuanzisha vagi basi nisingesubiri mpaka mwanakijiji mwenyewe alalamike.

3.Mimi nadhani hii atmosphere inayojengwa hapa ya kujenga chuki, na kuwachonganisha wachaga dhidi ya watanzania wenzao inakufurahisha.

4.Tofauti na wewe "mpenda amani" uliyehalalisha mwanakijiji kutukanwa, mimi nimependekeza SULUHU kwa mswahili na mwanakijiji kuombwa radhi.

5.Kama mambo yamekwisha kiutu uzima basi tuendelee na mjadala--wewe ukishamirisha chuki dhidi ya wachaga, na sisi wengine tukipinga chuki hizo kwa hoja.
 
jokakuu

Mswahili
Augustine Moshi.

sijatangaza chuki kwa wachaga wote. tizama vizuri nimekuwa nikimfagilia Tenga kama mtu makini si mara moja wala mbili.
au Tenga nae si mchagga? hakuna excuse hapa ni ukabila uliopo TRA.

Mwanakijiji.

najua wewe una lako mie siwezi kushughulika na wewe. nakuuliza vipi kuhusu mchango wa maiti wa TOBI? kijana aliyefia Brazil? tunajua wewe ni sehemu ya network hiyo ndio maana umekuwa ukitetea uovu TRA. soon tutaweka mtandao wa wauza madawa ya kulevya waliopo nje ya TZ. nitapita kote Holland, uswizi,America ya kusini, marekani, uk, uturuki,brazil tena sao paul, ugiriki na njia ya irani.
suburini zamu yako. hapa huwezi.
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=47
Mzee Mwanakijiji
najua wewe una lako mie siwezi kushughulika na wewe. nakuuliza vipi kuhusu mchango wa maiti wa TOBI? kijana aliyefia Brazil? tunajua wewe ni sehemu ya network hiyo ndio maana umekuwa ukitetea uovu TRA. soon tutaweka mtandao wa wauza madawa ya kulevya waliopo nje ya TZ. nitapita kote Holland, uswizi,America ya kusini, marekani, uk, uturuki,brazil tena sao paul, ugiriki na njia ya irani.
suburini zamu yako. hapa huwezi.wow.... I like your facts.. sasa mimi ni muuza madawa ya kulevya.. haya wenye kumuunga mkono Mswahili jitokezini kawapa fact!!

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=47

Mzee MwanakijijiHivi suala la Tobi na suala la Ukabila vinahusiana vipi? Ni mswahili aliyeleta na wengine wawili kuongezea suala la mimi kusaidia kuchangisha msiba wa Tobi ili kuhoji my credibility or intergrity. Now, kama hilo wangetaka liwe hoja wangeanzisha thread nyingine and let them discuss me if that gives them any pleasure.

Sasa, Mswahili amewasiliana na mimi na kasema hakumaanisha mimi niko kwenye network ya Wauza unga bali mimi ni "network ya wanaotetea uovu TRA". That is a fair allegation.

Sitaki kuwa issue kwani inapoteza muda na mtiririko wa hoja. Sitaki kumfanya mtu hoja hasa yale nisemayo juu yake hayahusiani na hoja za mtu huyo. Itakuwa ni pigo kubwa kama kile hoja zikiwa za moto tunaanza kuhamia kwenye "umesema hivi kwa vile wewe ni mtoto wa fulani", "unasema hivi kwa sababu huna kazi, n.k n.k"

Kama mtu huna hoja, ni bora ukae kimya na uendelee kusoma mada and enjoy it! Sasa, hebu tuachane na "mwanakijiji" na issues ambazo tunazo kibinafsi. Ieleweke kuwa sina kinyongo au beef na mtu yeyote humu tunayepingana kwa hoja. Wapo marafiki humu ambao kwenye suala hili tuko pande mbili tofauti na hilo halipunguzi heshima yangu kwao!

turudi kwenye issue: Kuna ukabila TRA kwa vile kuna watu wa kabila moja wengi?
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=52

Hayo ndio yaliyotokea, sasa unaweza kutuonyesha mahali ambapo Mswahili amesema MKJJ ni muuza unga? Hilo ni swali ambalo MKJJ alimuuliza Mswahili ambalo hakulijibu hapa ukumbini bali kwenye PM yake. Au unataka kuleta agenda zako? Jibu maswali kwenye mada na usitake kutafuta scapegoat.

MKJJ amekubali na maelezo ya Mswahili lakini wewe umekomalia tafsiri yako, tusome hoja na tujibu hoja, hii ni kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Tuondokane na tabia mbaya ambayo inaendekezwa na watu wachache.
 
Mbona mnatuvuruga bana? Sasa ona mmefunika nilichoandika hadi nimesahau nimefikia wapi.

Mi nataka kuongelea masuala mengine bana sasa mnaturejesha kule tulikokukwepa wengine bana? Mi sijui kurudi nyuma; Dua nionyeshe hapa nilichoandika awali ili nipate majibu kwa wale wenye data. Ujue macho yangu yako hapa nataka kupata kujua watu wana mawazo gani juu yale niliyoomba kuelezwa.

Noma kweli
 
Duuh!! Mara ya kwanza nili-give up kusoma hii thread baada ya kurasa 8 hivi. sasa nimejikongoja wee, mpaka nimemaliza. Sababu kubwa niliacha kusoma ni kwasababu niliona, ukweli ni kwamba ukabila upo (sana sana katika nyanja za mambo ya finance/pesa, ambayo ni area sensitive), kwahiyo nikaona hamna haja ya kubishana vitu ambavyo ni logic.
Tatizo linakuja ni watu kutofanya utafiti. mimi niko kempu ya Mswahili katika hii ishu. Ningependa nikubaliane na MKJJ kuhusu 'undugunisation', lakini ishu hii ni zaidi ya undugunisation. Mhe. PM kaja na list ya majina yake, lakini Mswahili alipo-rebutt, basi PM katulia. The fact is, watu wanaogopa kuongelea hii ishu ya 'ukabila' wakiogopa kuitwa 'hutus n tutsi' kiaina, kwahiyo wana-rely kwenye facts za Mswahili na PM, na nisengependa kusema zaidi, ila hapa nakubaliana na Mswahili (not only from his facts, but from my experience and what I know).
Ugawaji wa kazi upo na ulitendeka labda kutokana na legacy ya ukoloni au shortsightness ya Nyerere (au alipigwa bao? siju)? Lakini msisingizie waChagga walisoma zaidi (labda enzi hizo, lakini sio sasa kiasi kwamba watawale idara fulani fulani). Kwahiyo nina uhakika kabisa ukiangalia taasisi mbalimbali lazima utakuta kwamba makabila fulani yamejaa. So I wont waste my time kubishana ukabila haupo. Ndugu yangu PM, mimi msukuma, na nina ugonjwa na dada wa Kilimanjaro. Nategemea nikioa huko na mimi labda nitakuwa waziri wa nchi huko mbeleni hahaaa. Wewe mwenyewe PM, umesema mbona makabila mengine hayalalamiki (Sukuma, Nyamwezi etc). Ukweli ni kwamba watu wenye kisomo wapo, na sio kwamba hatuoni double standards. Sasa mimi naweza kuongea kama msukuma (lakini sina ukabila), najua kabisa Mwanza/Shinyanga (sukumaland) inachangia sana utajiri wa Tanzania, lakini maendeleo yake ni machovu, ukifananisha na mikoa ya kaskazini (na mchango wao katika taifa), na ingetakiwa tuwe-represented fairly katika nyanja muhimu (lakini kwa qualifications za mtu). Najua zamani kulikuwa na lobbysts wa nguvu sana (kina Bomani etc) na walisikilizwa sana, na kila mkoa ina lobbyst wao kwa interest zao kuvuta maendeleo (ndio mambo ya KDF hayo). Kwavile wewe ni Chadema, basi, mkileta mfumo wa majimbo, mbona mikoa ya kanda ya ziwa itawapiga bao? Sasa hii ni mfano mdogo wa kuonyesha ukabila upo katika National level mambo ya maendeleo. Mimi sio mkabila, mimi ni mtanzania, na chances are....nitaoa kabila nyingine (kama nilivyokwambia dada zenu nawapenda hahaaaaa).

Argument yangu sio kwamba kabila zingine zipewe posts undeservedly ili kupunguza kabila fulani, lakini katika mambo ya Finance TZ, pananuka fyuuu and we know it. Labda next stage, mmwulize Mswahili aende idara nyingine, kwani TRA ameshinda. Na nina uhakika akienda idara nyingine, atakutana na kabila fulani limetanda. Nasema haya kama mTanzania na kwa faida ya Tanzania, denying a problem exits is quite ignorant and potentially deadly. In the words of sijui nani........'Viongozi tupo na tumejaa teleee!!!'.
Wakati mkitafakari kutatua hili tatizo, kuna EAC inakuja. Hivi hii ishu si italeta matatizo makubwa zaidi?
 
mwanakijiji wrote:
Worm, Chuo Kikuu Dar, Wahaya wako wengi huko! tumeambiwa Jeshini wapo Wanyakyusa wengi... we have decided to break a principle and that principle will keep breaking us up!! Tukimaliza hayo matatu tuangalie Wapare wako wengi wapi...Wasukuma, n.k....

Mwanakijiji,
hata kwenye riadha naona ni Wambulu na Barabaig ndiyo wamejaa huko. Kulikoni Tanzania? Je, hapo napo tuseme kuna ukabila ktk "biashara" ya kutimua mbio. Binafsi siamini kama kuna ukabila hapo.

Mimi naamini tatizo halihitaji majibu rahisi-rahisi. Wako wanaopinga, lakini kuna gap kubwa ktk masuala ya elimu baina ya mikoa mbalimbali tanzania. Suala la uchumi nalo linachangia sana.

majuzi nimetumiwa e-mail which is a joke about how couple from different tribes in tanzania propose sex. kitu cha kushangaza tunaambiwa the Hayas would propose in ENGLISH.

Wengine wanaweza kuona ile ni kama kejeli kwa kabila la wahaya. Binafsi naona hawa wenzetu wako ahead of the game. Mhaya anaona fahari sana kuzungumza "Kiswahili cha ulimwengu"--ENGLISH. Zaidi, hiyo inaonyesha kwamba wahaya ni jamii inayoona fahari na kutilia mkazo elimu.

Ziko jamii ambako heshima ya mtu hutokana na idadi ya wanawake aliyooa. Katika jamii ya Kihaya heshima ya mtu hutokana na ngazi ya elimu aliyofikia["nshomire mpaka P-H-D".] Unaweza kudai elimu imekuwa kama utamaduni wa hawa jamaa. Hata mashuleni utaona jinsi wanavyojisumbua kusoma.

Huu mjadala ungekuwa na maana zaidi kama ungejikita ktk kutafuta mbinu za kuamsha mwamko wa elimu Tanzania nzima. Nategemea wachagiaji wataipokea changamoto hiyo.
 
Jamani huwezi kuongoza nchi kwa hisia tu na huwezi kumridhisha kila mtu. Ni kweli wakati mwingine lazima uangalie mtazamo wa jumla wa watu kwani siyo watu wote wanaweza kuelewa nini kinaendelea. Kuna wakati JK alipofanya uteuzi na nafasi zote alizotangaza zilikuwa ni Waislamu, mimi nilikuwa wa kwanza kusema Rais asiwape watu sababu ya kuzungumzia udini. Kwa sababu watu wakianza minon'gono hii ni hatari kwa nchi na kwa jamii husika. Kuanzia wakati huo amefanya vizuri sana kwani kila anapotangaza majina zaidi ya matatu basi anachanganya watu na hivyo amezima mazungumzo ya udini.

Hili suala la ukabila nako liko vile vile. TRA ilipofanyiwa mabadiliko mwaka 1996 toka Idara ya Mapato na kuwa Mamlaka ya Mapato wafanyakazi wote walifukuzwa! na wakatakiwa kuomba kazi upya. Walipoomba kazi upya wafanyakazi 1200 hawakukubaliwa (sina uhakika wachagga walikuwa wangapi, ila kwa vile TRA kuna ukabila, basi sidhani kuna mchagga hata mmoja aliyeachwa!). Kati ya hao 1200, 656 walitoka kitengo cha Forodha (Customs). Wale waliokubaliwa walipewa probation ya mwaka mmoja na baada ya mwaka mmoja wengine 240 wakafukuzwa (sidhani kama kulikuwa na Mchagga hata mmoja). Hivi sasa kuna wafanyakazi karibu 3500 hivi na idadi yao haiwezi kupita 3600 kwa mujibu wa utaratibu na kanuni walizojiwekea.

TRA ina utaratibu wa kutaka wafanyakazi wake wote watangaze mali zao kila mwaka na pindi mali hizo zinapobadilika. Endapo madai yanatolewa dhidi ya mfanyakazi wa TRA yahusuyo ufisadi, uchunguzi hufanyika na uzito wa ushahidi ukionekana basi mfanyakazi hufukuzwa! Of course, kama ilivyo kwenye vitengo vingine ni vigumu sana kuonesha ushahidi uliodhahiri na usiopingika kuwa mtu fulani ni mla rushwa!

Na kuna utaratibu wa kuwazungusha (rotate) wale wanaoshika nafasi nyeti (jinsi gani hili limetekelezwa tangu 1996 sina uhakika) Wengi wafanyakazi wa ngazi za juu huajiriwa kwa kipindi cha miaka mitatu mitatu.

Swali ambalo hatuna budi kulijibu ni jinsi gani "genge kutoka Kilimanjaro" limeweza kujinufaisha pasipo uhalali kupitia TRA? Je, kuna njama ya kuliibia Taifa kwa watu wa kabila moja kufanya kazi mahali pamoja na hivyo kuweza kula njama, bila hata kujali kama watu hao wanatoka koo tofauti au vikabila tofauti ndani ya kabila hilo kubwa?

Haitoshi peke yake kuonesha kuwa wingi wa watu wa kabila moja ni chanzo cha ukabila bila kuonesha ukabila huo. Nikiwakuta wazungu wengi wanafanya kazi kwenye kitengo au kampuni fulani siwezi mara moja kuhitimisha kuwa wote ni wabaguzi pasipo vitendo vya kibaguzi!

Mswahili: Hivi kati ya wafanyakazi wote walioachishwa kazi TRA baada ya mabadiliko ya 1996 kuna Mchagga hata mmoja na ni asilimia ngapi ya Wachagga walioachwa ukilinganisha na waliobaki? Endapo utaweza kuonesha kuwa wengi waliochwa kwenye mabadiliko ya 1996 walikuwa ni watu wa makabila mengine huo ndio utakuwa ushahidi wa kwanza ambao unaweza kunifanya niangalie tena suala hili kama lina ukabila.

- Baada ya mabadiliko hayo yote je kuna mfanyakazi yeyote Mchagga kuanzia makao makuu na mikoani ambaye aliachishwa kazi na nafasi yake kujazwa na mtu ambaye si Mchagga. Ni wachagga wangapi ambao wamefukuzwa kazi mpaka sasa ukilinganisha na watu wa makabila mengine na ratio yao TRA.


Ukijibu maswali yangu haya with specifics kama ulizozitoa ulipotoa tuhuma unaweza kunishawishi nikubali kuwa kuna ukabila TRA. Tafadhali usinitume ati kama mwandishi niende kufanya uchunguzi au kuzungumza na watu wa TRA, wakati wewe ndio mwenye data, wengine wanaweza wasiwe wazi. Please nimwagie data!!
 
Nice people....

jokaKuu here we go! Changamoto yako muhimu kuzingatiwa katika kila anayechangia kwenye hii thread. In reality hiki chote tunachokiita 'ukabila' kimekuja tokana na 'Elimu'.

Ebana umegusa kwenye kidonda, tatizo naanza kusinzia hapa dah!
 
Mada hii imekuwa kama communication satellite iliyoexplode angani na kubaki vipande vidogo vidogo vikielea bila kurudisha signal yoyote duniani.
 
Kichuguu

Usiwe na wasi wasi tunajaribu kufanya some repairs wakati inaanguka.

jokakuu

1. Tunao wafanyakazi wa TRA na mmojawapo ni Mmanda ambaye aliripotiwa akisema maneno haya wakati wa issue ya ukabila ilipoanza June 2006: Mmanda alisema kuhusu swala hilo tusishangae TRA twende jeshini kwanza. alikuwa ana maana gani? huyu yuko jikoni anasema maneno hayo sisi ni watu ambao hatujui mambo ya pale.

2. Uliongelea James Mbatia ambaye aliajiriwa TRA bila cheti, cheti alichokuwa nacho ni cha Form VI je aliajiriwa katika mazingira gani? Alisomea Engineering kutokana na habari uliyotuletea, ilikuwaje TRA wamwajiri?
 
Mwana kijiji.
Mbona bwana unachagua mpaka watu wakuhoji.
Watu wengine mbona ulikuwa ukiwahoji leo unaogopa kuwahoji wachaga wa TRA.
Sasa wachaga wamekuwa wanaogopewa?
 
Back
Top Bottom