wana jamboForums,
Mwanzoni mwa miaka ya 1990 Raisi Mwinyi aliunda Tume ya kuchunguza utendaji kazi wa Idara za Ushuru wa Forodha na Kodi ya Mapato.
Tume hiyo ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Nimejaribu google search nimeona mjumbe mwingine alikuwa Juma Volta Mwapachu. I wish ningeipata tume nzima.
Mapendekezo ya Tume yalikuwa kuvunjwa kwa hizo Idara mbili na kuundwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wafanyakazi wote walilazimika kuomba kazi upya.
Kamishna Mkuu wa kwanza Melkzedeck Sanare[rip] aliteuliwa na Raisi Mwinyi. Marehemu Sanare[mwenyeji wa arusha] alitokea ATC akiwa GM. Bodi ya Wakurugenzi ilizinduliwa na Raisi Mkapa na Waziri wa Fedha Prof.Simon Mbilinyi. Mwenyekiti wa Bodi alikuwa Dr.Benno Ndulu.
Bodi ya Wakurugenzi wa ATC inakuwa na wajumbe 10. Mwenyekiti huteuliwa na Raisi, na wako wajumbe wengine 5 wanaoingia kutokana na nyadhifa zao serikalini na TRA. Waziri wa fedha huteua wajumbe wanne. Sasa kabla hatujaanza kuwalaumu wakina Mramba ni vizuri tukalizingatia hilo.
Tanzania tumekuwa na Tume nyingi tu zilizoundwa na Maraisi mbalimbali. Imekuwa kama utamaduni kuzipa Tume hizo majina ya wenyeviti wake. Mifano michache ni, Tume ya Edward Ayila,Tume ya Jaji Nyalali,Tume ya Warioba,Tume ya Jaji Kipenka n.k. I dont think one has to read too much into the name "Tume ya Edwin Mtei."