Jasusi, watu wamechelewa! tulipata nafasi ya kukataa ukabila huu mada hii ilipoanza lakini kwa vile ilikuwa "yametajwa na majina" ya ukabila wa watu wengine, ukabila wa baadhi ya wanachama wenzetu ukafumbiwa macho! Watu wakatoa pongezi kwa mtu ati "amekata issue" na "amemwaga data". Watu wakasifia na kusema ni wa wakati wa "kumkoma nyani geledi"! Kila tulipojaribu kuonesha upotofu wa mawazo hayo tukaambiwa "kwanini tunawatetea wachagga? tuna maslahi gani na wachagga" Wengine tumeulizwa kama tumechumbia uchaggani (jambo ambalo silithibitishi wala kukanusha)!
Hata sasa kuna ndugu zetu hapa bado wanakubali kuna ukabila. Lakini ukabila wanaozungumzia wao ni wa wachagga kwa vile mtu ambaye hana ukabila kasema hivyo!!! Maneno anayoyasema mwanachama huyo mwenzetu kama yangewekwa kwenye TV yangemfukuzisha kazi kama Imus!! Lakini kwa vile tumeonekana tumeshapepewa na kufukizwa moshi huu wa chuki ya kikabila, baadhi tumeanza kuamini na kuwashuku Wachagga!! Tumeanza TRA, inabidi tuendelee kuwatafuta, twende Hazina, twende Ikulu, twende Benki Kuu, popote tutakapowakuta wachagga tujue ni ukabila umewaweka hapo.
Tangu nilipoweka aliyoyasema mwanachama huyo kwangu hadharani nilitarajia wanachama wengi ambao wamesoma kutokea kulaani na kuyakana mawazo hayo na kuonesha mshikamano na ndugu zetu Wachagga. Anyway watu wanaogopa, kwa sababu wataonekana "wanawapenda wachagga" au "wananufaika na ukabila"!
Maneno ya mwanachama huyo kuhusu wachagga ni ya kichochezi, kibaguzi, na yaliyojaa sumu ya ukabila. Ni maneno ya hatari ambayo licha ya kuwa ana haki ya kuyasema hadharani ili tujue kilichomo ndani yake, hayana nafasi katika Tanzania yetu, hayavumiliki, na hisia zake ni za kupiga vita kwa nguvu moja! Niko tayari kusimama peke yangu kutamka hivyo.
Ninachoomba ni kuwa asichukuliwe hatua yoyote ile hapa JF bali tujue ni kitu gani kinamuongoza na tuwe tayari kugundua sumu yake hiyo anapoandika juu ya Wachagga! Haki yake ya kutoa maoni, isitishiwe kwa namna yoyote ile kwani ni vizuri kujua mtu anasema nini kwani inatuonesha anachofikiri, kuliko mtu atutendee kitu ambacho hatukujua amewahi kufikiri!!