mswahili wrote:
MKASA WA FOY KUMBAMBIKIA KESI benny lusege aliyekuwa officer incharge bandarini na kumfukuzisha kazi kwa maksudi kisa yeye ni RRO na alikuwa anapitisha mabomu yake kwa jina la benny lusege hakujua kama lusege kaenda shule kwa maana ya shule.Foy KWA kushirikiana na kittlya na wachagga wenzao wakamtimua kazi benny akaenda kujitetea kwenye bodi na kila ushahidi hatimaye benny akarudishwa kazini lakini wachagga wote wamekuwa na chuki naye hadi kuchoma moto nyumba yake na akapelekwa porini na hii kesi ilifika hadi kwa Meghji.
jamani msitete kitu msichokijua huenda mnazuia haki za watu kwa kujifurahisha akina lusege wametaka kuuliwa TRA KUNA genge la majambazi.
mswahili,
kwanini unaona ni ukabila tu ndiyo unawasukuma hao jamaa kumdhuru mr.lusege? kwanini isiwe RUSHWA au WIZI? je, huyo jamaa angekuwa ni mchaga mwenzao hivi unaamini wangemstahi kama angetakaa kupitisha hayo magendo?
Ogah wrote:
TUSIWE WATU WA KUKURUPUKA TU MIDHALI STUDY IMEFANYIKA TUNASEMA NI SAHIHI. TUMEONA STUDY NYINGI TU AMBAZO NI BOGUS - WHO KNOWS TRA BETTER THAN WALE WANAOFANYA KAZI PALE NA AMBAO WANANYANYASWA NA UKABILA.[red] JE NI STUDY GANI YA UHAKIKA YA WATANZANIA AU WAGENI KUTOKA NJE.[/red] LAZIMA TUWE MAKINI NA HIZI STUDIES.
well said Dua,
Ogah,
kama umefuatilia postings za Dua basi ataona kwamba tayari ana-conclusions zake. study yoyote ile itakayoleta conclusions tofauti yeye ataiponda. Kama ameikataa study hiyo hapo juu, nini kitamzuia kuiponda study nyingine itakayofuatia?
Dua huyo huyo, yalipoletwa majina hapa na Phillemon akazua kisingizio kwamba uko uwezekano kwamba wapo waliobadili majina!!
Mwanakijiji,Philemon,Mkandara,
1.Mwanzo mwa hoja hii tulikubaliana kwamba kuna uwezekano wachaga wako kwa wingi ktk posti kubwakubwa kutokana na ukweli kwamba kabila hilo lilikwenda shule mwanzoni. Hali hiyo unaweza kuiona hata ktk mashirika mengine. Suala hilo lingekuwa TRA tu, basi tungesema kuna ukabila. Suala hilo lipo accross the board.
2.Malalamiko yakageuka kwamba: kama ni suala la wachaga kusoma zaidi mbona hata UMESENJA na UKARANI makabila mengine hayaajiriwi? Philemon akaleta a random list, ndefu kidogo, ambayo inaonyesha kwamba hakuna monopoly ya wachaga at all.
3.Baada ya Phillemon kuleta listi hiyo Mswahili akadai listi hiyo ni ya MAKARANI,MGAMBO, MESENJA,na MADEREVA wa TRA!! Zaidi katika kuichambua listi hiyo Mswahili ameonyesha wote siyo wasomi. Mswahili alipaswa kutetea hoja yake ya awali kwa kutuonyesha kwamba wachaga wamehodhi hata ukarani, na umesenja.
4.Mwanakijiji ameleta copy ya utafiti ambao umefikia conclusion kwamba tatizo la ukabila lipo URA, na siyo TRA. Kwanini watu wameidismiss ripoti hiyo outrightly? Badala yake watu wanataka another independent investigation.
5.Mwanzo wa mada kulikuwa na hata malalamiko kwamba ukabila wa wachaga unakuwa facilitated na mawaziri toka kilimanjaro. Waziri anateua wajumbe wanne kati ya 10 wa board ya TRA. Mwenyekiti huteuliwa na Raisi, na wengine watano huingia kutokana na sheria ya TRA. Ukiangalia wajumbe walioteuliwa na Waziri utaona hakuna ukabila.
6.Management kuu ya TRA imeonyesha a reasonable tribal balance. Hata meneja utumishi na uajiri siyo mchaga, bali ni mpare. Katika suala linalohusisha wapare basi Mswahili hubadilika na kusema kuna "genge la wakilimanjaro." Naelewa kwamba haya makabila ni watani wa jadi, lakini hivi wanaweza kuwa na mkakati wa pamoja kuyakandamiza makabila mengine? Mimi ningemwamini mswahili kama angedai lipo genge lingine independent--"genge la wapare." Hii hoja ya "wakilimanjaro" hainiingii akilini.