Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

JokaKuu wrote:


Dua responded:


Dua,
You are correct in your assertion kwamba mwanafunzi akivukuzwa mlimani basi anakuwa hana shahada. Hilo halihitaji maswali, wala msisitizo hapa.

Pamoja na hayo, ni vizuri for the sake of fairness, ukaeleza kwamba Mbatia alifukuzwa chuo kikuu kwasababu za kisiasa. vilevile ni vizuri ukaeleza kwamba alifukuzwa akiwa karibu na kumaliza[3rd or 4th year] faculty of engineering.

Joka kuu!
Ni ukweli usiopingika kwamba Mbatia ni Form six leaver.....Na kama toka afukuzwe angekuwa na nia ya kusoma angekwisha hitimu kwa kiwango cha Shahada ya kwanza na hata uzamili kama si Uzamivu.
 
DUA.
tumkubalie JOKA KUU kuwa Mbatia ana digrii ili yaishe otherwise atatutoa kwenye mada.
na Mrema anayo tuliiona wote!!!
 
mswahili cleopa david msuya ni mwenyekiti wa bodi ya TIC kanda ya kilimanjaro,juzi makamu wa rais amezindua dodi ya TIC ya mwanza......yale majina mengine nilisema ni mengi mno ,wewe uliza kituo chochote nitakujibu...vipi umeona majina ya watendaji wakuu ,nimekuwekea hapo juu?

noana umeshashindwa hoja sasa unaamua kurudi NSSF...TUNAKUANGALIA TU...unaposema dar mlishindwa kujenga shule kwa sababuhamkupewa pesa unakosea ...shule zote za moshi zilizojengwa baada ya 1967,ni za binafsi na za wananchi ,tena wamechanga kila kata ikawa na sekondari...sasa mswahili mnangoja hadi mjengewe...
hakuna aliyemkaribisha mtu mjini hapa,watu wamekuja toka bara kufanya nkazi mjini hakuna anayeweza kupambana na nguvu ya soko.
 
Mwendapole
View Public Profile
Send a private message to Mwendapole
Send email to Mwendapole
Find all posts by Mwendapole
Add Mwendapole to Your Buddy List

#46 23rd February 2007, 02:22 PM
kidole
Junior Member Join Date: Tue Nov 2006
Posts: 10
Rep Power: 0


kidole

--------------------------------------------------------------------------------

wanajf natumaini mnaendelea vizuri na kutuwakilisha,
tafadhali turudi kwenye mada yetu kuu.
UNYANYASAJI WA WAUNGU WATU.
BAADA YA JITIADA ZA KUKOMBOA LORR LILE ,KESI IKAWA TUMESHITAKIWA KAMA KOSA LA JINAI,NA SI SWALA LA KODI TENA.
KESI ILENDELEA KUSIKILIZWA MPAKA TAREHE 21/05/2001 HUKUMU IKATOKA MNAMO TAREHE 4/02/2002KWAMBA SISI KAMPUNI XXXX PAMOJA NA MKURUGENZI ALIYESHITAKIWA PAMOJA NA LORR HATUKUWA NA HATIA,KWA HIYO MAHAKAMA IMETUACHIA HURU.BAADA YA HUKUMU HIYO KUTOLEWA MWANASHERIA WETU ALIWEZA KUOMBA ORDER YA MALI WALIZOSHIKILIA.NA KUPEWA MNAMO TAREHE 5/03/2002.NA MWANASHERIA WETU ALIWEZA KUTUPATIA KWA AJILI YA KWENDA KUCHUKUA HIYO MALI, CHA KUSHANGA
NILIFIKA OFISINI KWA BWANA MMOJA ANAYEITWA KISAKA AMBAYE NDIYE

ALIKUWA RRO WAKATI HUO,NAYE ALINIAMBIA HILI SWALA LILIKUWA KWENYE OFISI YA (INVESTIGATION)KWA HIYO NIENDE HUKO NA HIYO ORDER YA MAHAKAMA.KWELI NILIWEZA KUFIKA OFISI HIZO NA KUKUTA BWANA MKUBWA RUTIINDA AKIWA OFISINI KWAKE.NILIOMBA RUHUSA KWA KARANI WAKE KWAMBA NAITAJI KUMUONA ,YULE KARANI WAKE ALINIRUHUSU NA NILIWEZA,

KUINGIA OFISI KWA BWANA RUTIINDA ,CHA KUSHANGAA NA CHA KUSIKITIKA NILIPOMWONYESHA ILE ORDER YA MAHAKAMANI NA KUMWAMBIA NIMEKUJA KUCHUKUA HIYO MALI YETU,BWANA HUYU ALIANZA KUFOKA NA KUNIFUKUZA OFISI KWAKE,NILIJARIBU KUMULIZA KWANI HII TAARIFA MWANA SHERIA

WENU AJAKUPA TAARIFA?BWANA HUYU ALIZIDI KUNISUKUMA NIONDOKE OFISI KWAKE,BASI KWA KUWA ALISHAFUNGUA MLANGO NILIAMUA KUONDOKA,
NAOMBA KUWAKILISHA NITAENDELEA KESHO.
 
Mswahili!

What point are you trying to make by re-posting Kidole's posts?
 
Phillimon.

pole na vikao. hapo juu nimekopi kwenye TRA hardcore thread. unaona katajwa KISSAKA mchagga mwenzio niliyekuambia alikuwa regional revenue officer(RRO).

habari ya msuya si TIC acha uongo. KUNA asasi ya maendeleo kilimajaro na cleopa msuya kapewa uenyekiti.

kama huoni tumia mawani.

ukarimu ni jadi ya watu wa mwambao. ukarimu wao umewavutia wengi. kuna maeneo ukienda kuomba maji unapewa halafu unaambiwa utoe pesa, pwani mzee jongo kumpangisha mushi haone taabu. lakini mushi akijenga hawezi kumpangisha shomvi hata lift tu hawapi waswahili.

kama unaenda njia ya iringa-mbeya gari ikiharibika njiani basi inayokuja nyuma unasimama na kujaribu kutoa msaada kwa yule aliyepata shida au kuharibikiwa. lakini njia ya moshi hakuna ubinadamu huo! hiyo ni mifano midogo tu.
kadri unavyokwenda MLIMA ndio unavyozidi kupotea ustaarabu.
 
» Home » Habari za Kitaifa » Msuya akabidhiwa Kibo Breweries
Msuya akabidhiwa Kibo Breweries
By Habari Tanzania | Published 10/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

na Ramadhani Siwayombe, Moshi

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imekifunga kiwanda chake cha bia kilichopo mkoani Kilimanjaro, maarufu kwa jina la Kibo Breweries na kumkabidhi majengo pamoja na mitambo ya kiwanda hicho, Mwenyekiti wa Kilimanjaro Development Forum (KDF), Waziri Mkuu mstaafu, David Cleopa Msuya. Makabidhiano hayo yalifanyika juzi mjini Moshi katika kiwanda hicho kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Craig Mac Dougall na Msuya.

Mac Dougall alisema wameamua kutoa majengo ya kiwanda hicho kwa KDF kutokana na azima yao ya kutaka kushirikiana na jamii katika kuhakikisha wananchi wa Kilimanjaro ambao ni wadau wakuu wa biashara yao wanapata fursa ya kujikwamua kiuchumi kupitia taasisi hiyo ambayo itakuwa kiungo muhimu kati ya kampuni hiyo na wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro. Alisema wametoa majengo hayo ili yatumike kuendesha miradi mbalimbali ambayo itatoa ajira kwa wananchi wa Kilimanjaro, na wao kama kampuni kwa kipindi cha miaka mitatu wataisaidia taasisi hiyo kulipia baadhi ya gharama, ikiwamo umeme, maji na walinzi, ili kuiwezesha taasisi iweze kujiendesha kwa faida katika miradi watakayoanzisha katika kiwanda hicho.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa majengo hayo, Msuya alisema wamefarijika kwa msaada huo, kwani mkoa huo kwa hivi sasa umekuwa ukiyumba kiuchumi kutokana na viwanda vingi kusimamisha uzalishaji, hivyo kupunguza mapato ya mkoa na pia ajira kwa wananchi wa mkoa huo.

Alisema baada ya kugundua upungufu huo ambao umetokana na kupungua kwa uzalishaji wa zao kuu la biashara la kahawa hadi kufikia tani nne kwa mwaka kutoka tani 28, waliamua kuanzisha taasisi hiyo ili kujaribu kusaidiana na serikali kuwasaidia wananchi wa mkoa huo kuboresha uchumi wao.

Akitoa tathmini ya mkoa, Mkuu wa mkoa huo, Mohamed Babu, alisema kutokana na viwanda vingi vilivyokuwapo kusimamisha uzalishaji na kufungwa, ajira 6,0852 zilizokuwapo zimepungua hadi kubaki 441 za wafanyakazi wa kudumu.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Cril Chami, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia, na mke wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Anna Mkapa
 
DAILY NEWS

· The government yesterday threw its weigh behind initiatives by non-governmental entities which seek in earnest to bring about development.

The pledge was made yesterday by thePrime Minister, Mr. Frederick Sumaye, when inaugurating the Board of Governors of the newsly-established Kilimanjaro Development Forum (KDF).

"Any region whichi sets up institutions which are development-oriented, has government symparthy and support. It is something we shuld all be proud of," he told the borad members.

He said the establishement of KDF shows how residents in the region want to participate in the implementation of the National Vision whose focus is on eradication of poverty through sustainable economic development.

The premier called on other regions, leaders and people at large to identify development hitches and take appropriate remedial measures.

Mr. Sumaye said he was optimistic the KDF would become a viable institution. A former PM, Mr. Cleopa Msuya, is the chairman of the forum.

Earlier, Mr. Msuya said the forum would strive to serve as a facilitation agency for investors who want to set up projects in the region.
 
mswahili inaonekana una USONGOnao hao (WATOTO WA SAMAKI)
 
PHILLIMON.

HIYO NI TIC? KWANINI MTU mzima unaishi kwa uzushi tu? nimekwambia Cleopa msuya mwenyekiti wa KDF unabisha tu.
hii ngoma nzito nitakutoa tu kamasi umeleta uongo TRA nimekutoa.
nyamaza kelele zako zitazidi kunifanya niende deep na uchafu wenu TRA.
KUWA MSTARAABU KAMA KINA TENGA WATU MAKINI.
 
mswahili huyu mtu tuna mtegemea bwana ni mtu mkubwa katika jamii jaribu kupunguza kidogo au Anayataka?.
 
phillemon michael
mswahili cleopa david msuya ni mwenyekiti wa bodi ya TIC kanda ya kilimanjaro
Mkuu
mswahili inaonekana una USONGOnao hao (WATOTO WA SAMAKI)

Mswahili amejibu hilo kwa data kutoka sehemu mbili tofauti, sasa mambo ya usongo yanatoka wapi? Au mlitaka anyamaze ili mseme ni muongo? Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Hii ni kuonyesha kwamba Msuya ni Mwenyekiti wa Kilimanjaro Development Forum (KDF). wakati phillemon michael anabisha.
 
MKUU.

joka kuu na phillimon mikael huko nyuma wamekanusha kuwa Mpare na mchagga hawawezi kukaa pamoja kupanga 'mikakati' ya kuisaidia Kilimanjaro wakimananisha TRA hakuna kitu namna hiyo.

nikamwambia msuya ni mwenyekiti wa mkoa na unajua akishika msuya alivyokuwa na upendeleo kwao. wakabisha wakasema ni TIC nimeweka hapa KILIMANAJARO DEVELOPMENT FORUM na ina msuya mama mkapa. chami, salome mbatia na kina ndesamburo, kama hao wanakaa kuweka mkakati wa kimkoa why not TRA?

siwezi kumuumbua PM najua mtu muhimu kwenye jamii ila awe na heshima asifanye watu wajinga.

tukiuliza wanasema wamesoma sana lakini kututafutia wagombea urais wenye digrii wameshindwa na visingizio kibao ooh Mbatia graduate kwani alikaa miaka mitatu UDSM, kwa mpembuzi ukiona mtu yuko mwaka wa tatu kajiingiza kwenye mgomo au vurugu mara nyingi ni yule aliyefeli darasani au anajua ata disco hivyo anatafuta sababu ya kuondokea.

tunarudia tena Mbatia form six si msomaji angekwenda hata Tumaini university au Bukoba UNIVERSITY.
 
KDF point noted,offcourse nimechanganya kwa sababu moja ya malengo ya KDF ni kuongeza nafasi za uwekezaji kilimanjaro...na wamefanikiwa kushawishi kufunguliwa ofisi ya TIC moshi,wiki iliyopita WANA MWANZA pia wamefanikisha kufunguliwa kwa ofisi ya TIC MWANZA ili kuvutia wawekezaji huko...ilifunguliwa na makamu wa rais.....
 
MSWAHILI NA PHILEMON

Acheni ubishi

mwageni data na mjadala utakuwa mtamu kama wote mkiwa mnajadili data

MWAGENI DATA
 
Wanabodi,

Nimefurahi sana kuona kitendo walichokiwafanya mkoa wa Kilimanjaro kuanzisha shirikisho hilo la KDF. Mtakumbuka kuwa niliwahi kusema haya toka Bcstimes kuwa ni muhimu kwa serikali kuanzisha vyombo kama hivi kila mkoa ama kuigawa nchi ktk zones za Kiuchumi...
Tatizo linalonishinda kuelewa sasa hivi ni kwamba yaonyesha kuwa hili swala limeachiwa watu binafsi ama mikoa kufungua hizo forum badala ya serikali kuhakikisha kila Mkoa kama sio jimbo unafanya uchaguzi wa viongozi wao ktk kufungua vyombo hivi.
Tanzania inahitaji vyombo hivi kwa kila hali kuhakikisha kwamba wakulima wa mazao, wafugaji na wavuvi wanapata elimu, haki na misaada mbalimbali inayohusiana na biashara duniani. Kukata kabisa nguvu ya walanguzi wa kati ambao wanafaidika kwa nguvu ya wanyonge!
Umefika wakati wa serikali yetu kutazama nafasi na maslahi ya Tanzania ktk soko la biashara na sio kutazama mazingira ya biashara duniani ili kutafuta nafasi na maslahi ya Tanzania. We can only improve what we have, mbali ya hapo tutakuwa kila siku tukigawa utajiri wetu nje kwa sababu hatujiamini kama tunaweza. Na tunapougawa utajiri wetu nje kinachobaki ni umaskini na sisi hugawana umaskini!
 
DR.who.

mimi simbishi na nimempa Facts nyingi tu. ila Phillimon uongo ni jadi yake na sasa anadai TIC ni KDF JEE Chadema ni CUF? kwa vile malengo yanafanana? vyote ni vyama vya upinzani.

amekwama vibaya, MAJINA aliyotuletea ya washika mapembe nimeyachambua yote,

naanda misamaha ya kodi na ushuru inayotolewa kwa minajili ya kikabila na kwanini Mengi amekwepa kulipa Billion 5 kama kodi na TRA.

NA deni la Mfanyabiashara mzee TANGO Billion 3 kwa TRA amezimwa kwa vile si mchagga.
 
Kwanza nijibu hoja ya Mkandara kwamba serikali ndiyo ianzishe vitu kama KDF mikoani. Kwa maoni yangu, sio vema kuisubiri serikali kuu ifanye karibu kila kitu. Maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe. Wale wanaosubiri serikali wataachwa nyuma sana. Umefika wakati Watanzania watambue kwamba serikali sio baba, wala mama, na wala sio hata mjomba. Jiendeleze, usisubiri serikali ikuendeleze.

Pili, nasikitika sana kuona kwamba Mswahili (na labda hata watu wengine wawili au watatu) wamekazania kuleta chuki dhidi ya Wachaga. Anachoshambulia Mswahili hapa ni Wachaga au ni TRA? Anashambulia TRA kwa kutumia Wachaga au anatumia TRA kushambulia Wachaga?

Kama wasemavyo Wachina, safari ya kilomita mia huanza kwa hatua moja. Inawezekana kuleta chuki kubwa dhidi ya kabila moja kwa kuanza kama alivyoanza Mswahili. Ndiyo lengo lake?

Mimi ni Mchaga. Mswahili unaposhambualia Wachaga hapa unataka nikuunge mkono? Au unataka Wachaga wote tukupinge? Mbona utakuwa umetuanzishia taratibu za kujitete kikabila kwa mara ya kwanza? Sijawahi mimi kubidika kujitetea kwa msingi wa ukabila. Unatarajia makabila yote yakae upande mmoja nawe yashambulie Wachaga? Kwa lengo gani?

Mimi nakushauri Mswahili: Unaweza kushambulia TRA (you may have your frustrations with them) lakini usishambulie Wachaga. Tuachie hali yetu ya kutokuwa na mabishano ya misingi ya kikabila.

Augustine Moshi
 
Mwalimu, hatari unayoona wewe ndiyo ambayo naizungumzia. Lengo la Mswahili si kutafuta suluhisho la watu wa kabila moja kujazana kwenye kitengo kimoja na hivyo kuleta 'picha' ya ukabila. La hasha! lengo lake ni kupandikiza chuki kati ya watu wa bara na watu wa pwani.. anasema "Dar ina wenyewe".. anauliza "Iweje Dar iongozwe na watu wa kutoka bara"... n.k n.k...

Ameng'ang'ania "ukabila" na watu wanamuunga mkono wakati tatizo halisi hawataki kulitaja!! Wanataka tukienda TRA na kupokelewa na Bw. Mushi mawazoni tuwe resentment "mkabila huyu". Siku Bi. Tarimo akija kutaka kukusanya kodi, tuhisi "mkabila huyu". Njia pekee ya kumridhisha ni kutoajiri wachagga kabisa TRA. Tukifanya hivyo ataenda Muhimbili atasema "mbona kuna madaktari wengi wachagga? Muhimbili kuna ukabila"... na hataishia hapo!!

Nawasihi ndugu zangu, tuukatae ukabila huu na kuutambua kwa jina lake!! Najua wengi mna nia nzuri na makusudio mazuri, lakini tatizo mnalolipigia kelele halipo zaidi ya kujaribu kulijenga ili mlipigie kelele!! Wengine wamejificha kwa kivuli cha uzalendo huku wamejifunika mablanketi ya chuki na kisasi wakibeba bendera za ukabila zenye rangi ya "mapenzi ya nchi"!! Hawa tunawakataa, tutaendelea kuwakataa, na tuna sababu ya kuwakataa!!!
 
Back
Top Bottom