INawezekana wana sifa.....Sema haiingii akilini....
Inakuwaje wenye sifa wanakuwa ni watu anaotoka nao sehemu moja tu?.....Mwesiga, Mtawala na kwa nini nafasi nyingine hajazijaza na kudai waombaji hawakukidhi vigezo?...Kwa nini anawaweka watu aina ya Mshangama na Madadi ambao pamoja na kukaa TFF miaka lolote hakuna lolote walilosaidia...Kwa nini asingeweka sura mpya kama lengo lilikuwa ni kuleta mabadiliko TFF....
Mwenzake Tenga nafasi kama hizi aliwaachia KPMG ama PWC(sina uhakika ni nani hasa) ambao walitangaza nafasi za kazi na kupitia majina ya waombaji ikiwa ni pamoja na kuwafanyia usaili...Na hapa ndipo walipatikana akina David Mwakalebela, Angetile Osiah, Florian Kaijage, Boniface Mgoyo Wambura na Jimmy Kabwe...Sasa yeye Malinzi kitendo cha yeye na TFF yake kutangaza ajira na kuwafanyia usaili na kutangaza waajiriwa wapya kinatia shaka na kulifanya suala la ukabila liwe na nguvu zaidi...Na wengine wanaweza wakasema hata hizo nafasi mbili hazijajazwa kutokana na 'wahaya' wenzake kutojitokeza kuomba kazi hizo....