Kama Edo kaandika haya basi atakuwa amejiunga na akina Pasco wa JF, na akina ARAP SANG wengine kueneza uchochezi wa kidini, kikabila, kikanda na kadhalika. nasema haya kwa sababu kupeana majukumu ili kuendesha taasisi, shirika na mengine kama haya ya umma, hakutakiwe hata kidogo kufuata misingi ya kikabila, kidini,rangi, n.k. Kinachotakiwa kufuatwa ni uwezo binafsi wa mteuliwa kumudu kutimiza majukumu yake aliyopangiwa katika nafasi aliyoteuliwa.
Edo atwambie hawa walioteuliwa hawafai kushika nyazifa hizo kwa kuangalia uwezo wao binafsi wa kufanya kazi? Kama hawawezi basi waondolewe mara moja....nasema waondolewe mara moja ila si kwa uhaya wao bali kwa viwango vyao vya utendaji kazi.
....Tupinge kwa nguvu zote wale wote (akiwemo na EDO) wanaoleta mada, propaganda za kikabila, kidini, nk. hapa nchini na ulimwenguni kwa ujumla.