Mabibo Hostel?Ninapoishi ni karibu na hostel ya chuo flani hapa Dar,
Niseme Tu wazazi mlioko mikoani mnaleta watoto wenu mnawageuza makahaba. Watoto wanatumika sio mchezo. Ikifika jioni Magari yanapack kama yako gereji .
Daaaah
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mabinti wengi sana maturation yao wame ya weka kwenye mapochi ya wanaume.Tena hakuna mkakati wowote kudhibiti hali hii
Nipe namba zake kwa ushauri zaidi najua anapitia kipindi kigumumtoto wa sister kala disco MUHAS kwa ugeni wa maisha ya chuo, sasa atakula alichopandaβ¦
kitoto cha miaka 19 kishatoa mimba mbili ndani ya kipindi cha semesters 4β¦.WTF
Hapana sio ,Mabibo Hostel?
Wanampiga kama ngoma, tatizo wazazi tunawategemea watoto baadala ya mtoto kumtegemea mzazi utakuta mzazi ana muomba pesa mtoto wake ambaye ni mwanafunzi.Hapana sio ,
Ni kingine.
Na ninazifaham hostel nyingi Tu binafsi yaani ikifika Giza ni uasherati Kwa kwenda mbele. Waume za watu wanajazana hapo ....
Kama sasa hivi ni likizo Ila kuna watoto WA kike wako hostel tangu mwezi WA 7 , huwa najiuliza hawa watoto wanakaaje hostel na vyuo vimefungwa hao wazazi wao hawana muda nao ?
Ila nilichogundua wazazi hawana time na watoto wao.
Kingine umasikini umasikini umasikini hawa watoto WAna shida Sana. Mtoto WA kike unakuta Hana hata hela ya Kula na mzazi Hana time nae!
Sababu nyingine ni ulimbukeni. Kuna watoto WA kike ni limbukeni saaaaana. Mtoto anakuja Dar kutoka huko Namtumbo anajifanya anaijua Dar kushinda wazawa. Anataka Viwanja vyote avijue! Anaishia kudondokea Kwa wahuni wanamchakaza Ile mbaya!
Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mkuu umeongea hoja ya msingi sana. Mambo ya kuiga na kujidai kwenda na wakati ni mojawapo ya sababu kubwa zinazochangia ukahaba vyuoni. Tatizo hili haliishii vyuoni tu, bali huendelea mpaka kwenye ndoa. Upumbavu huu umekuwa chanzo cha ndoa nyingi kuyumba au kuvunjika kabisa. Bahati mbaya jamii imelipokea hili kama mahitajio ya wakati kwa mwanamke.Mabinti wengi sana maturation yao wame ya weka kwenye mapochi ya wanaume.
Hamna kitu kinacho waumiza mabinti KUFUATA TRENDS. IPHONE mpya ikitoka anataka kuwa nayo, kiatu cha brand fulani anataka kwa nayo,nguo na mapochi ya brands fulani anataka kuwa nayo na mwisho anataka kuwa na bwana mwenye gari.
Hapo sasa ndipo wanapo umia hizo TRENDS zina hitaji hela na yeye hela hana.Kilichobaki ni kukiuza kipochi manyonya chake kwa wanaume tofauti tofauti ili awe na hela ya kukimbizana na hizo trends.
Kwa kifupi hamna utumwa mbaya kama wa kukimbizana na trends wakati hela huna,siku hizi hata watoto wa kiume wame uingia huu mtego wa kufuata trends na mara nyingi huishia pabaya.
Trends trends trends zina waharibu vijana wa siku hizi.
Kiasili kabisa mwanamke hana uwezo wa kuweka mipaka bali mwanamke huwekewa mipaka. Kitendo cha kumsaidia kwa kuondoa "sheria kandamizi" ni kitendo cha kumwondolea mipaka na hivyo anaweza kufanya lolote pasipo majuto. Hajui kuweka mipaka, halafu hata iliyopo imeondolewa, ndio maana tumefikia kujadili kina mama waendelee na masomo shule za msingi na sekondari. Sasa hakuna mwalimu mzuri wa mapenzi kwa mwanamke kama mwanamke mwenzake. Vitoto vitavurugwa huko mpaka basi, vilifikia umri wa kwenda chuo tayari ni vikahaba vizoefu. Kifupi zinaa imehalalishwaHapa udom ukahaba umefikia kiwango cha kutisha..nadhan sababu ya ukahaba ni freedom, kukutana na new faces nyingi, kukosa mahitaji muhimu na kukosa self control/ assertiveness
Wengi wanakuwa chini ya uangalizi wa wazazi na walezi huku wakielekezwa na kusimamiwa kila kitu, ghafla wanapofika wakati wa kuingia chuo wanakuwa huru, sasa matumizi ya huo uhuru ndio tatizo.Labda ungeelezea wanakuwa wamebanwa kivipi. Pia unadhani wakipewa uhuru toka awali (kuanzia elimu ya msingi) unadhani wanabadilika na kuwa vijana wenye maadili mema?
Maana ya uangalizi kwa mtoto ni kumjengea tabia ya kuyakabili mambo kwa mfumo huo anaolelewa nao hata pale arakapojitemea. Duniani hakuna mzazi mwenye akili timamu atamwacha mwanaye afanye atakavyo. Sasa ba si malezi sio kunyima uhuru bali ni kuelekeza namna ya kuutumia uhuru ulionao.Wengi wanakuwa chini ya uangalizi wa wazazi na walezi huku wakielekezwa na kusimamiwa kila kitu, ghafla wanapofika wakati wa kuingia chuo wanakuwa huru, sasa matumizi ya huo uhuru ndio tatizo.