Ukame wa sasa ni Matokeo ya Ukataji Miti Mil 2.7 ya Selous

Ukame wa sasa ni Matokeo ya Ukataji Miti Mil 2.7 ya Selous

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Magufuli alikuwa hashauriki. Miti 2.7 Milioni ilikatwa kwenye pori la akiba la Selous kupisha ujenzi wa mradi wa umeme wa JNHEP. Idadi hiyo ya miti ikiwekwa ardhini ni sawa na eneo lote la mkoa wa Dar es Salaam
IMG-20221027-WA0002.jpg
 
Kweli JPM alikuwa Jiwe, alikata miti hadi Kenya

Magufuli alikuwa baba haambiliki na taarifa za wataalamu alisema fake wametumwa na mabeberu wanatuonea wivu, madhara yake twaona vuli imekata na miji ka Dar na pwani joto limezidi kupita kiasi huo msitu ulikuwa sehemu ya kupumulia Tanzania, hafu umeme wenyewe bwawa kujaa ni kudra za Mungu.

Kiukweli kukata huo msitu ulikuwa ubinafsi wa kiwango Cha sgr ni hatari kuwa na viongozi wasioambilika na wasiojali vizazi vijavyo.
 
Kwahyo miti milioni 2 tu ndo ilikuwa inaleta mvua Tanzania?
Hizi tabia za kujidai unakosoa mambo ambayo hayana faida hata kwa familia yako hebu acha kwa logic tu ukikata miti 2m ndo iwe chanzo cha ukame.

Mbona hao mabeberu wanaharibu mazingira toka miaka ya 1600 huko leo ww ndo unaona kujenga bwawa kuharibu mazingira mhhh unasikitisha sana
 
Magufuli alikuwa hashauriki. Miti 2.7 Milioni ilikatwa kwenye pori la akiba la Selous kupisha ujenzi wa mradi wa umeme wa JNHEP. Idadi hiyo ya miti ikiwekwa ardhini ni sawa na eneo lote la mkoa wa Dar es Salaam
View attachment 2399516
Sikutegemea kama watu wa mawazo kama haya bado wapo....hii ina maana kuna tatizo kubwa kwenye mfumo wa elimu yetu.
CCM haifai tena kuwepo.
Aibu kubwa hii..!
Pole kijana, sio kosa lako.
 
Kweli JPM alikuwa Jiwe, alikata miti hadi Kenya

Kwa mara ya kwanza katika kizazi chetu hiki ukame mkali kuikumba mikoa ya Ruvuma, Iringa na Njombe; Mbeya, Songwe, Rukwa, na Katavi zijiandae. Msitu wa Selous una direct effect ya hali ya hewa kwa mikoa hiyo.

Unyevu ukipungua Selous ni lazima mikoa hiyo iathirke kutokana na geographical location yao against Selous with respect to direction ya upepo. That's the fact Chief.
 
kwahyo miti milioni 2 tu ndo ilikua inaleta mvua tanzania ?
Hizi tabia za kujidai unakosoa mambo ambayo hayana faida hata kwa familia yako hebu acha kwa logic tu ukikata miti 2m ndo iwe chanzo cha ukame.

Mbona hao mabeberu wanaharibu mazingira toka miaka ya 1600 huko leo ww ndo unaona kujenga bwawa kuharibu mazingira mhhh unasikitisha sana
Hawa ndio walewaleee mkuu vibaraka vya mabeberu wanaosema eti Afrika tupo overpopulated tunazaliana sana wakati dunia nzima sisi ndio tupo wachache kuliko races nyingine
 
Alikuwa na tenda ya kuuza magogo.
Niliwahi kuuliza mtu wa TFS ile miti kwamba magogo yamepewa nani na kama zabuni ilikuwepo, nilichojibiwa ni kuwa kuna mtu amejimilikisha magogo yote, nikauliza ni nani, sikupata jibu.

Hii nchi kuna watu wanapaswa kushtakiwa kwa uhujumu uchumi hata kama wapo futi sita ardhini.
 
Niliwahi kuuliza mtu wa TFS ile miti kwamba magogo yamepewa nani na kama dhabuni ilikuwepo,nilichojibiwa ni kuwa kuna mtu amejimilikisha magogo yote,nikauliza ni nani,sikupata jibu.

Hii nchi kuna watu wanapaswa kushtakiwa kwa uhujumu uchumi hata kama wapo futi sita ardhini.
Miti milioni 2.7 halafu isijulikane ilipokwenda kama kweli ilikatwa, siwezi kuamini huu ujinga.

Ndio maana hawamtaji huyo mtu kwasababu naamini hayupo.
 
Magufuli alikuwa baba haambiliki na taarifa za wataalamu alisema fake wametumwa na mabeberu wanatuonea wivu, madhara yake twaona vuli imekata na miji ka Dar na pwani joto limezidi kupita kiasi huo msitu ulikuwa sehemu ya kupumulia Tanzania, hafu umeme wenyewe bwawa kujaa ni kudra za Mungu. Kiukweli kukata huo msitu ulikuwa ubinafsi wa kiwango Cha sgr ni hatari kuwa na viongozi wasioambilika na wasiojali vizazi vijavyo.
Mito mikubwa Ulaya kama Rhine na Danube ilikauka mwaka huu sababu ya ukame. Ina uhusiano na hiyo miti iliyokatwa Selous?

Jaribuni kufuta ujinga.
 
Magufuli alikuwa hashauriki. Miti 2.7 Milioni ilikatwa kwenye pori la akiba la Selous kupisha ujenzi wa mradi wa umeme wa JNHEP. Idadi hiyo ya miti ikiwekwa ardhini ni sawa na eneo lote la mkoa wa Dar es Salaam
View attachment 2399516
Wewe utakuwa ni wale wanaoamini Mungu hapendi kuleta mvua kwa makosa yetu. Tangu lini Ukame wa East Africa ukasababishwa na Selous? Au huna taarifa kwamba Erthiopia wako hali ngumu kuliko wewe hapa TZ.
 
Back
Top Bottom