Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Badala ya wangenunua kipya wamenunua injini mpyaa hivi kuna haja gani ya kujenga reli ya umeme wakati kivuko kipya chatushinda...!!

Twafanya chaguzi daily pesa za kivuko hatunaa!!
Viongoz wetu HAWAJUI KITU GANI HASA WANANCHI WANAHITAJI katika Muda mwafaka.

Ngoja wamalize Uchaguz Jimbo la liwale mwezi ujao

Billion 1 inateketea tena kumrudisha Bungeni mtu ambaye mwez uliopita alijiuzulu ubunge

Shithole leaders
 
Ajali ni mbaya sana_tumepoteza jamaa,rafiki zetu wengi
IMG-20180920-WA0001.jpg
IMG-20180920-WA0000.jpg
 

Attachments

  • IMG-20180920-WA0000.jpg
    IMG-20180920-WA0000.jpg
    130.1 KB · Views: 41
Kupinduka kwa chombo hiki lazima kwa vyovyote ni issue ya stability tu. Na poor stability inaweza kusababiswa na inproper positioning of the cargo au ubora wa chombo chenyewe. N wakati mwingine cargo shifting kwa sababu yeyote ile
 
Poleni sana wote mliokutwa na janga hili pia sisi Watanzania wote tuwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
 
Aljazeera wanaripoti watu 500 kuzama wakati mamlaka zinasema watu 100 hizi data zimekaaje?
 
Badala ya wangenunua kipya wamenunua injini mpyaa hivi kuna haja gani ya kujenga reli ya umeme wakati kivuko kipya chatushinda...!!

Twafanya chaguzi daily pesa za kivuko hatunaa!!
viongozi wa nchi hii" ni akili mgando". ..inastaajabisha sana na kuumiza wallahi" ndugu zetu wanaishi kwenye mazingira yenye miundo mbinu", haba" .. serikali ya ccm " ndio kwanza ipo busy kwakununua" upinzani", mwisho hupelekea chaguzi kurudiwa" huu ni ufujaji wa kodi za wananchi" wakati bado wanauhitaji mkubwa", wa miundombinu bora". ..Yaliyo tokea leo" iwe fundisho" kwa hili zimwi la hili taifa (ccm)..

halafu bila haya" wanatutajia idadi ya watu"6 wakati meli' imezama chini juu
 
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.


====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere

View attachment 872340

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.

Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.

Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.

Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.


View attachment 872299
Wanajeshi na raia wakitoa msaada wa uokoaji​
Pole kwa wana Ukerewe na Mwanza kwa ujumla....Nje ya mada hivi hiki sio kile kivuko ambacho kimezinduliwa juzi juzi na kurushwa live na TBC?
 
Ukifikilia kwa makini utaona kuna umhimu mkubwa wa kurekodi taarifa za abiria wanao wa majini kuliko abiria wa nchi kavu

Gari ikipata ajali ni rahisi kupata idadi ya waliokua wakisafili, lakini ajari za majini hua tunaishia kukisia tu.... Kadhaa wamekufa.

Wale tunao safili gafla gafla bila tarifa kwa ndg zetu tubadikike.
 
So sad! Poleni sana mliofikwa na maafa hayo makubwa.
 
Back
Top Bottom