Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Madhara yake ndio hayo,alafu tunaanza kuilaumu serikali na
Serikali ndio wanamiliki na kuendesha hivyo vivuko wao ndio wanapaswa kulaumiwa,halafu ni aibu hakuna list ya majina /idadi ya wasafiri waliokuwa kwenye kivuko
 
Hicho kivuko ni majuzi tu wame nunuliwa injini mpya zile za zaman zilikua hazina nguvu, maskini ya mungu mwenyezi muangu awa lehemu malehemu wote duh
 
Poleni ndugu na jamaa wote mliopoteza ndugu zenu,mungu yu pamoja nanyi.
 
Hela ya kurudia uchaguzi zingenunua vivuko vizuri kabisa ila hii serikali haitutakii mema wananchi wake. Wanatutoa kafà...ra
 
hebu wataalam mtusaidie, mtu anaweza kukaa majini kwa muda gan kabla ya kuokolewa?

Inategemea yupe kwenye mazingira yapi....kama hajafunikwa na na maji hata masaa sita hadi kumi akiwa mtaalam wa kuogelea na awe na pumzi yamaana
 
Mkuu acha hizo, mbona kigangwala alitembelewa na anadunda
kwani mimi ndiye niliyesema mkuu " hahaa " lakini hata hivyo yatupasa tuweke akiba ya maneno ". .. maana ilichukuwa takribani miezi miwili kwa majuto kuja kufikwa na kifo baada ya kutoka Kuonana na brother jiwe
 
yaani ," inatia kinyaa " in Africa " ukiwa kiongozi tu " basi unakuwa tayari " kuepuka misingi ya utu " na kuuvaa ushetani "
 
Poleni najua hii sirikali ndio chanzo cha yote hayo kwaku nunua vitu bila kukizi mahitaji kamili
 
Kupinduka kwa chombo hiki lazima kwa vyovyote ni issue ya stability tu. Na poor stability inaweza kusababiswa na inproper positioning of the cargo au ubora wa chombo chenyewe. N wakati mwingine cargo shifting kwa sababu yeyote ile
Mkuu umeongea kweli tupu!

Kwa mujibu wa watu walioko kule ambao wamepata maelezo kutoka kwa manusura, inasemekana kivuko mbali ya kuwa na watu wengi, kulikuwa na mizigo mingi hasa mahindi na saruji, na magari makubwa mawili. Inasemekana wakati kinakaribia kufika ng'ambo ilibidi kukata kona ili kwenda kwenye uelekeo sahihi wa kupark. Sasa wakati wa kukata kona hapo ndo mzigo wa upande mmoja ulihamia upande wa pili hivyo balance ikakosekana kika -overturn upside down.

Haya ni maelezo ya awali lakini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…