Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Sababu zinaweza kuwa:
1. Uwezo wa kuwaza nje ya box (zaidi kutoka kwa viongozi)ni mdogo= viongozi wajinga.
2. Uwezo wa waokoaji ktk hali ngumu zozote ni mdogo= wanajeshi dhaifu
3. Uoga wa waokoaji ktk mazingira magumu ya giza=wanajeshi waoga.
4. Viongozi kutojali uhai/maisha ya watu= viongozi kujali business zao.
* hakika viongozi/ watawala wanaohusika na hili inabidi wawajibishwe mara moja kwa kauli za kizembe kama hizo.
 
Labda ingekua kimezamia kwao ndo angeona hali hiyo hawezi kulala
 
Hivi RC, Msimamizi wa bandari Mwanza, RPC, DC, Kiongozi wa Zimamoto leo walipata usingizi kweli? huku roho za Watanzania zikiteketea ziwani? I cant imagine uongozi wa dizaini hii, na utasikia hakuna atakayewajibika.


Mkuu walilala sana, tatizo lao sio wananchi sana bali kipaombele chao ni ccm kutangazwa washindi wa uchaguzi. Ingekuwa ni kupambana ccm itangazwe washindi usiku, hao wote uliowataja wasingeondoka eneo la tukio.
 
kwahyo wewe ulitaka atoe jibu gani kwa mfano?

waokoaji wameingia kwenye kivuko wakajiridhisha hakuna aliye hai.. na zoezi likabadilika kutoka uokoaji kuwa uopoaji

kuendelea na zoezi ilikuwa ni kuhatarisha usalama wa hao waopoaji .. sidhani kama kungekuwa na watu walio hai ndni ya kivuko zoezi lingesitishwa sema tu lisitishwa kwa sababu wanejiridhisha hakuna akiye hai

sema kuna watu mnajifanya mnajua kuongea na kuongoza nchi wakati hata familia ya kuiongoza bado hujaipata..

embu basi sema ulitaka waendelee kutoa maiti hadi usiku wa manane? unajua changamoto za uokoaji majini?
 

Mimi hoja yangu imejikita kwenye usahihi wa kusitisha zoezi siku ya jana kwa sababu ya giza, na nikaeleza kwamba ilikua ni sawa kufanya vile kutokana na njia ambazo zilikua zinatumika. Na ili zoezi lisiendelee "kulala" ni lazima tu "improve the methods" ili ziwe fanisi na salama kwa waokoaji hasa wakati huo wa usiku na tuwaotoe ndugu zetu (hai au la) kule chini. Na mapendekezo uliyoyatoa hapo juu ni ya msingi kabisa ili kufanikisha zoezi zima. Kwa sababu yoyote ile, kwa uzembe au makosa ya mtu yeyote yule, kama njia za uokozi zilizokua zikiendelea kutumika hazikua salama na fanisi hiyo jana usiku, ilikua sahihi kusitisha zoezi lile hadi asubuhi. Suala la kwanini bado tunatumia njia "za kizamani" kufanya uokozi ni suala jingine (with respect to maamuzi ya jana)
 
Asiye sikia la mkuu huvunjika guu hawa wahenga walikuwa magenius.
 
kwani wamekufa watu wangapi hadi sasa kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika? Nimesoma skynews wanasema zaidi ya 200 wanahofiwa kufa.
Ila nilichojifunza
1:Wapinzani wasipuuzwe na wanatakiwa kuwepo ili wasaidie kuonyesha hatari ambazo zisingesemwa vizuri na CCM. Mbunge alionya kuwa haya yatatokea.
2:Nilitegemea Tangu MV BK izame tungekuwa na Disaster management plan ya uhakika humo ziwani. Nashangaa kuona watu wanaokolewa na mitumbwi na sio Boti za uhakika za uokoaji.
3: Kwa jinsi ilivyozama nakubaliana na huyo mkuu kupona mtu pale ni asilimia ndogo, ila excuse ya uchovu sijawahi kuisikia popote duniani.

Tujitahidi kutoa taarifa zenye faraja kwa Umma. Kusema tutaendelea kesho hata dunia inayofuatilia tukio hili inatuona hatujali watu wetu.
Maoni
 
Kwa kauli aliyotoa jana RC nimeamua tu nikae kimya mana sina neno zaidi ya matusi ya nguoni kwa viongozi wote, acha tu maumivu ya kauli hiyo nikae nayo moyoni. Yani miili ya binadamu wnzako unahalalisha iwe chakula cha samaki??
 
mkeo akiwa leba tu hulali sembuse ndugu yako kulaliwa na meli kwenye maji? tuna shida na huu uongozi wa sasa. mtaelewa tu maana muda huwa hauna ghilba.

Mkuu, tatizo linaanzia kwenye uwezo wetu wa kufanya uokozi, si suala la nani amelaliwa na meli kule. Naona kama unajaribu kutuaminisha kwamba kwa siku ya jana kulikua na uwezekano wa kuendelea kufanya uokozi hadi usiku (bila kuathiri usalama wa waokoaji) lakini roho mbaya na kutokujali kwa viongozi ndio wakaamua kusitisha zoezi. Haya yanaweza kuwa si mawazo mema sana mkuu.
 
Hivi vivuko huwa vinajaza mpaka inasikitisha!
Usifikiri hao watu wako kama wewe na kuchukua tahadhari! NO WAY!
Mara nyingine unaona kabisa watu wanafanya mambo na ni completely suicidal act!
Kama wanavyo panda mshikaki kwenye bodaboda au pickup kwa Nyuma!
Mambo mengine huwa yanabadilika kwa wakati wake, lakini kuinyoshea kidole Serikali ni kutafuta LAANA KUTOKA KWA MAMA TANZANIA walahi!
Be realistic kijana mdogo ehhh jamani!
That’s all
 
 
Waliopo eneo la tukio wanasema sio zaid ya 100m
So kilikuwa kimekaribia sana kufika mwisho ?, lakini haya matukio yamekuwa yakijirudia rudia sana, (kumbuka MV bukoba, na kule mto kilombero) mpaka jana saa 2 usiku walikuwa hawajajua ni watu wangapi waikuwemo ndani ya kivuko, yaani wasimamizi wanashindilia watu as if ni mizigo, Tutafakari.
 
Hakuna Cha ajabu katika Awamu hi,

Si munakumbuka hate tetemeko la kagera rais mwenyewe kwa kinywa chake alitamuka kwamba hakuahidi kuketa tetemeko katika ahadi zake

Kwahiyo naamini hata hii ajali hakuiahidi
 
hawa tutawalaumu bure niliwahi kumsikia Mbunge wao akiomba Engine Mbili mpya za kufungwa kwenye hicho kivuko maana zilizopo zinazima Mara kwa Mara na walilipotezea wakati abiria wanalipia ila kuweka mazingira ya usalama wao yapo chini kabisa
kivuko sijaona hata maboya yakielea kwa ajili ya kusaidia abiria waliomwagwa...
 
Ndio kilikuwa kimekaribia kabisa kufika, tayari abiria walikuwa wamejiandaa kuteremka
 
Tushukuru nchi yetu haipatwi na majanga makubwa na ya kutisha kulinganisha na nchi zingine zinazopigwa na mafuriko, matetemeko na vimbunga vya hatari. Bado hatujawa tayari na ukabilianaji wa majanga na uokoaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…