Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

nimeongea na watu wa ukara hii habari ni ya ukweli na hali ni mbaya sana kwani watu walikuwa wanatoka gulioni bugorora na kurudi ukara kisiwani, hivyo meli ilikuwa imeshona sana, waliopatikana ni wachache sana
 
Mnalalamika serikali kutumia pesa kwenye chaguzi za marudio wakati mnaopiga folleni kwenda kupiga kura ni nyinyi nyinyi.
Utakuta li mtu limetoka kutaka kufia campaigns za mwafulani halafu leo anakuja kusema serikali inatumia vibaya hela kwenye chaguzi ambazo hazina maana.

Anyway, Poleni sana wana Ukerewe.
Nani aliyekudanganya kuwa kura ndio zinaamua viongozi??
 
mleta mada picha uliyoweka sio sahihi sio ya tukio husika..hio picha ni tukio la kuzama MV spice kule Zanzibar...cc Mod One
 
KIVUKO CHA MV. NYERERE CHAFUNGWA INJINI MPYA

Na Theresia Mwami - TEMESA
Kivuko cha MV. NYERERE kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, kinafungwa injini mpya tangu kununuliwa kwake na kuanza kutoa huduma mwaka 2004.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bugorola, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu alisema kivuko cha MV. Nyerere kinafungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 ili kuongeza ufanisi wa kivuko katika kutoa huduma kwa wananchi wa Bugorola na Ukara. Dkt. Mgwatu amewaagiza mafundi wanaofunga injini hizo wafanye kazi usiku na mchana ili waweze kukamilisha ufungaji wa injini mapema iwezekanavyo ili kivuko kiendelee kutoa huduma ya usafrishaji wa abiria na mali zao.

Aidha, Dkt. Mgwatu amesema Serikali imedhamiria kuimarisha usafiri wa vivuko katika Ziwa Viktoria kwa kujenga vivuko vipya vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Kigongo, Busisi, Kayenze, Bezi, Chato, Bwina, Bukondo, Senga, Muharamba, Kikumbaitale, Izumacheli na Nkome pamoja na kuvifanyia ukarabati vivuko vya MV. Nyerere, MV. Misungwi, MV. Sengerema na MV. Sabasaba.

Nae meneja wa vivuko TEMESA Mhandisi Hassan Karonda amebainisha kuwa mifumo ya injini ya kivuko cha MV. NYERERE imechoka sana kwa sasa kwa kuwa ni ya muda mrefu. Alisema, injini mbili mpya pamoja na giaboksi zinazofungwa katika kivuko cha MV. Nyerere ni za aina ya Perkins zenye nguvu ya kilowatt 161 kila moja na zinafungwa na mafundi wa TEMESA kwa kushirikiana na wale wa kampuni ya Delta Industrial Equipment Limited. Aliongeza kuwa kazi ya kufunga injini itaenda sambamba na kazi ya kukipaka rangi kivuko hicho na baada ya hapo kivuko kitaendelea kutoa huduma kama hapo awali lakini kwa kasi zaidi.

Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja. TEMESA inasimamia uendeshaji wa vivuko 30 vya serikali vilivyoko kwenye jumla ya vituo 19 Tanzania bara.

kwa habari hii Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Dkt. Mussa Mgwatu na Eng. Hassan Karonda kuwajibi kunawahusu aisee,tena chap kwa haraka.
 
Back
Top Bottom