Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi kweli mkuu wa mkoa anasitisha zoezi la uokoaji kisa giza!? Mkoa mzima hakuna uwezo wa kuweka taa ili kuruhusu uokoaji very sad! Hata kutengeneza umeme wa muda ili kumudu mazingira ya wakati huo tumeshindwa!?
Hivi usiku umekuja ghafla sana mpaka kusitisha zoezi?
Kwa hali hii kama kuna siku ajali itatokea saa 19:00 jion na hujui kuongelea basi nimekufa, yaan jua liwake!!!?
Watazania tubadilike kila mmoja kwa nafasi yake.
 
Kuna kila dalili ya uzembe uliyopelekea ajali hii,kuna watu hawata salimika kwa Magu kwenye hili tukio.
 
Mimi bado sijamwelewa huyo mkuu wa mkoa....
Anasema tunasitisha uokoaji mpaka kesho asubuhi kwa sababu giza limeingia!!!

Maswali makuu ya kujiuliza.
1/Watu waliopo hai chini ya maji(kama wapo), wataendelea kukaa kwenye maji wakiwa hai mpaka kesho?
2/Nini maana ya dharula, ikiwa unaweza kuhairisha?
3/Wameshindwa kupambana na giza ili uokoaji uendelee?

Hivi ile kauli ya hapa kazi tu ni blah blah ya kuwachota wajinga tu?
Sasa n wakati wa mkuu wa mkoa kuachia ngazi kwa kuacha watu kwenye maji kisa giza! Hv hili giza limekuja ghafla?
 
RC hata kama umefanya mazuri namna gani hapo Mwanza kwa hili ningeomba Rais aanze na wewe kwanza, kwa busara fupi tu usingetoa kauli hii ya kuwa zoezi limesitishwa Kisa GIZA ungetumia kisingizio kingine ila siyo kitu kidogo kama GIZA kwenye jambo zito, gumu na LA kutisha kuliko jambo lolote duniani UHAI WA MTU hauna mbadala. Naandika kwa uchungu sana, kifo cha maji ni kibaya sana kuliko karibia kifo chochote kwa sababu kabla MTU hajakata roho akiwa majini huwa anahisi km atapata msaada atapona na asipopata haponi na zaidi anakuwa anajua kuwa baada ya muda flani nitakuwa nimekufa( ni uchungu usiyo mithirika) RC kwa kauli yako tu inatosha kuwekwa ndani kwanza, hivi kama Leo nchi ingepatwa VITA ni kweli tungesema vita tusitishe hadi Giza liishe? Hivi lile jeshi LA wanamaji linalo linda bahari kwa chopa huwa linafanya kazi mchana tu, hivi sherehe za Uhuru yale magwaride yote ya wanamaji kumbe yanafanya kazi mchana tu? Au yapo kwa ajili ya maonesho tu? Hivi RC hii kauli umekutoka tu au ndo ukweli? Yaani hii ni fedhea kubwa sana. Hivi mbona uvuvi harama unashughulikiwa hadi Usiku wa manane? . Sina LA kufanya Mungu awape pumziko LA Amani Watanzania wenzangu waliotangulia mbele za haki, zamu yangu ikiwaadia nitawakuta.
 
Hivi ugumu wa kujua watu waliokuwemo hata kwa makidirio unatoka wapi!?

Si waangalie vitabu vya risiti au rekodi za risiti za kieletroniki kama zinatumika huko wataweza kukadiria watu walikuwa wangapi
Ukisikia kuna utata wa idadi ujue walijaza watu na mizigo kupita kiasi.
Ukifuatilia unaweza kuta kuwa kuna gulio mitaa hiyo
 
In
Kwakweli aibu kubwa kwa serikali ya Tanzania kwamba vikosi vya uokoaji havifanyi kazi usiku kwa sababu ya Giza?
Hivi hii serikali kweli inajari wananchi wake? Hivi mkuu Wa mkoa kama mwanao nae angekua kwenye hivyo meli ungediriki kutamka zoezi la.uokoaji limesitishwa?
Kama watu wanaweza kulowa dagaa usiku Wa manane tena kwa chemli mmeshindwa kuokoa watu?

Dah nimeumia sana namuwaza MTU yule ambae bado yuko hai ndani ya meli anasubiri uokozi
Namuwaza MTU yule ambae yuko hai ila analiwa na samaki akiwa anajiona mzimamzima, Leo ndio umetimia ule msemo Wa PAMBANA NA.HALI YAKO

Mkuu Wa mkoa anaenda zake kulala kashasema zoezi litaendelea kesho ambao bado mpo hai pambaneni na hali zenu

This is Africa😢😢😢😢😢

Mungu tusaidie
Inaumiza sana ndugu yangu, fikiria mtu amening'inia mahala akisubiria msaada alafu RC anawahi kuoga maji ya moto yaliyo pashwa kwa umeme na bill zinalipwa na huyo aliyeachwa ananyofolewa na samaki huku anajiona. Kwa hoja dhaifu sana eti GIZA??????
 
Watanzania tujifunze kuwa wastaarabu na kujiweka mbali na maneno ya kejeli kwenye majanga kama haya yanayohusianisha na uhai wa watu!!!!...

Sote tunatambua udhaifu na ubovu wa watawala wetu lakini lugha za kejeli haziwagusi watawala wetu bali wanyonge wenzetu ambao ndio wahanga wa misiba hii na majanga haya!!!

Kuonyesha waliofanya ubadhilifu kwenye matengenezo na kiasi cha hela kilichotumika havina maaana kwa sasa kwa kuwa tayari watu wameshapoteza maisha na hatuwezi kuwarudisha uhai...zaidi ya kuwafariji na sio kuwasimanga....

Walale pema marehemu wote
 
Kivuko cha Kigamboni geti likifunguliwa "Watanganyika" hukimbilia kwenye "Panton" kama kuku waliofunguliwa bandani. Sijui kama huwa wanahesabu idadi ya abiria wanaoingia.

Kuna siku kile kivuko kilijaa kama daladala za Mbagala. Hili lililotokea Ukerewe liwe funzo kwa vivuko vingine vyote Tanzania hususani kivuko cha kwenda kigamboni.
 
NIMEUMIA SANA

Anaandika Kijana Msomi
Rashid Chilumba

Nimesikia zoezi la uokoaji kwenye ajali ya kivuko Mwanza limesitishwa hadi kesho kutokana na kiza, sasa kesho mtakwenda kuokoa au kuokota Maiti?

Hapo Mwanza kuna kikosi cha Jeshi, boti za doria za polisi, helikopta na vivuko vingine? Hivi kweli vyote hivyo havina taa kubwa za kuwezesha zoezi la uokozi kuendelea usiku kucha? Kama havina tulivinunua vya kazi gani?

Ni aibu kwa viongozi kusema tunaenda kulala eti kuna giza ziwani wakati kuna dazani ya watanzania wenzetu tunaowahudumia wamezama ziwani tena siyo kwa uzembe wao bali kwa ujuba na tabia ya kutokujali maisha ya watu na kutosimamia usalama wao.

Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu wa kamandi ya Jeshi la Wananchi, Mkuu wa Bandari Mwanza mnapata wapi ujasiri wa kwenda kulala na kuna watu watoto wao, baba zao, Mama zao wamo majini na hawajui kama watawapata wakiwa hai? Hivi ingelikuwa ni jamaa zenu wa karibu mngepata ujasiri wa kusimamisha zoezi kwa sababu ya kiza?

Katika dunia ya leo seriously kabisa mnasema kiza kinawazuia kuokoa watu? Aiseee.... Kwa hiyo hao waliozama ikiwa kwa bahati bado wapo hai hadi sasa mnategemea Israeli atawangoja ninyi hadi kesho jua litapochomoza? Huu ni uzembe wa hali ya juu mno.

Kweli kabisa mnashindwa kufunga tochi kubwa kama zile za bandari kwenye helikopta moja ya polisi hapo na boti nne tano mkaingia kuwaokoa watanzania wenzetu? Hata ikiwa ni wafu lakini faraja ni kupata japo miili yao hadi kesho samaki, mawimbi ya ziwa nk inaweza kuwa imewapoteza zaidi.

Leo nimeumia sana, makosa yale yake ya Mv Bukoba, Spice Islander, Skagit yamejirudia Mv. Nyerere na watu wanaenda kulala usiku umeingia na vyombo vya habari vinaonesha shilawadu na kutoa dakika kiduchu kwa habari muhimu na msiba mkubwa huo wa taifa.

Na tena mlionywa mara kadhaa kuwa chombo ni kibovu. Mkuu wa bandari ya mwanza bado yupo na wadhifa wake na msimamizi wa Sumatra kanda ya ziwa kesho ataenda pia ofisini.

Mungu awapumzishe waliotangulia na atawalipa waliowasababishia kuzama kwenu kwa uzembe wao.

Cc
Dotto Bulendu
Malisa GJ
Kheri James

Tusaidiane kusema Ndugu zangu. Tunawezaje kwenda kulala na watanzania wenzetu wako majini sasa hivi?
 
.."George Nyamaha, the head of Ukerewe district council, of which the island is a part, said: “There were more than a hundred passengers on board when the ferry sank. It is feared that a significant number have lost their lives.”

However, it was hard to establish the precise number of passengers since the person dispensing tickets had also drowned with the machine recording the data lost.."

-Boat imebeba waay more than its capacity..
-Hawajui idadi ya walioingia..
-Na sababu ni kuwa mkata ticket amezama pamoja na machine ya kukatia, kwa hiyo hakuna data kamili.
 
Akili za viongozi wa awamu hii ni Mungu tu ndiye anayezijua, hivi utasitishaje kuokoa mtu anayetapatapa kujiokoa kwenye maji, mtu ambaye ukichelewa hata kwa dakika moja tu anazama, halafu useme subiri nitakuja kesho asubuhi, inaingia akilini kweli?

Ningekuwa mimi Magufuli wote waliohusika na kusitisha kazi ya kuokoa leo wasingeingia ofisini.

RIP waliotangulia mbele ya haki, ugua pole majeruhi.
220ddaf1-0271-4c4b-ba31-8349e623f018.jpeg
 
NIMEUMIA SANA

Anaandika Kijana Msomi
Rashid Chilumba

Nimesikia zoezi la uokoaji kwenye ajali ya kivuko Mwanza limesitishwa hadi kesho kutokana na kiza, sasa kesho mtakwenda kuokoa au kuokota Maiti?

Hapo Mwanza kuna kikosi cha Jeshi, boti za doria za polisi, helikopta na vivuko vingine? Hivi kweli vyote hivyo havina taa kubwa za kuwezesha zoezi la uokozi kuendelea usiku kucha? Kama havina tulivinunua vya kazi gani?

Ni aibu kwa viongozi kusema tunaenda kulala eti kuna giza ziwani wakati kuna dazani ya watanzania wenzetu tunaowahudumia wamezama ziwani tena siyo kwa uzembe wao bali kwa ujuba na tabia ya kutokujali maisha ya watu na kutosimamia usalama wao.

Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu wa kamandi ya Jeshi la Wananchi, Mkuu wa Bandari Mwanza mnapata wapi ujasiri wa kwenda kulala na kuna watu watoto wao, baba zao, Mama zao wamo majini na hawajui kama watawapata wakiwa hai? Hivi ingelikuwa ni jamaa zenu wa karibu mngepata ujasiri wa kusimamisha zoezi kwa sababu ya kiza?

Katika dunia ya leo seriously kabisa mnasema kiza kinawazuia kuokoa watu? Aiseee.... Kwa hiyo hao waliozama ikiwa kwa bahati bado wapo hai hadi sasa mnategemea Israeli atawangoja ninyi hadi kesho jua litapochomoza? Huu ni uzembe wa hali ya juu mno.

Kweli kabisa mnashindwa kufunga tochi kubwa kama zile za bandari kwenye helikopta moja ya polisi hapo na boti nne tano mkaingia kuwaokoa watanzania wenzetu? Hata ikiwa ni wafu lakini faraja ni kupata japo miili yao hadi kesho samaki, mawimbi ya ziwa nk inaweza kuwa imewapoteza zaidi.

Leo nimeumia sana, makosa yale yake ya Mv Bukoba, Spice Islander, Skagit yamejirudia Mv. Nyerere na watu wanaenda kulala usiku umeingia na vyombo vya habari vinaonesha shilawadu na kutoa dakika kiduchu kwa habari muhimu na msiba mkubwa huo wa taifa.

Na tena mlionywa mara kadhaa kuwa chombo ni kibovu. Mkuu wa bandari ya mwanza bado yupo na wadhifa wake na msimamizi wa Sumatra kanda ya ziwa kesho ataenda pia ofisini.

Mungu awapumzishe waliotangulia na atawalipa waliowasababishia kuzama kwenu kwa uzembe wao.

Cc
Dotto Bulendu
Malisa GJ
Kheri James

Tusaidiane kusema Ndugu zangu. Tunawezaje kwenda kulala na watanzania wenzetu wako majini sasa hivi?
Andiko hili linazidi kunitonesha sana, Nchini Kenya vyombo vya habari vimeripoti habari hizi haraka sana na kusitisha baadhi ya ratiba zao Mfano MILELE FM ya Kenya, TBC wako bize na kipindi cha miziki cha ZINAZO KIKI, inauma sana RC anaongezea kwa kusitisha zoezi kuwa GIZA limeingia. MTU aliyelelewa kwenye utamaduni wa KITANZANIA unapata wapi ujasiri wa kuingia kitandani ukalala wakati Wanadamu wenzako wawe maiti au hai unajua wako majini? Zaidi we ni kiongizi kwenye dhamana ndani ya mkoa. Kama Mh Rais aliwahi kukiri kuwa huwa anafanaya kazi hadi usiku kucha sasa wewe RC ujasiri huo wa kusitisha kuopoa maiti au watu hai ukaenda kumkumbatia mkeo unatoka wapi.
 
Back
Top Bottom