luche1
Senior Member
- Jan 18, 2017
- 144
- 107
Polee nduguNishapoteza wajomba zangu wawili [emoji24][emoji24][emoji24]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Polee nduguNishapoteza wajomba zangu wawili [emoji24][emoji24][emoji24]
Sasa n wakati wa mkuu wa mkoa kuachia ngazi kwa kuacha watu kwenye maji kisa giza! Hv hili giza limekuja ghafla?Mimi bado sijamwelewa huyo mkuu wa mkoa....
Anasema tunasitisha uokoaji mpaka kesho asubuhi kwa sababu giza limeingia!!!
Maswali makuu ya kujiuliza.
1/Watu waliopo hai chini ya maji(kama wapo), wataendelea kukaa kwenye maji wakiwa hai mpaka kesho?
2/Nini maana ya dharula, ikiwa unaweza kuhairisha?
3/Wameshindwa kupambana na giza ili uokoaji uendelee?
Hivi ile kauli ya hapa kazi tu ni blah blah ya kuwachota wajinga tu?
Binafsi nimesikia redio moja inaitwa Milele FM ya nchini Kenya inataja kuwa karibia watu 400 ndiyo walikuwa kwenye hicho kivuko japo sijui km ni kweli au LA!Kwahiyo DC amedanganya?!
Ukisikia kuna utata wa idadi ujue walijaza watu na mizigo kupita kiasi.Hivi ugumu wa kujua watu waliokuwemo hata kwa makidirio unatoka wapi!?
Si waangalie vitabu vya risiti au rekodi za risiti za kieletroniki kama zinatumika huko wataweza kukadiria watu walikuwa wangapi
Inaumiza sana ndugu yangu, fikiria mtu amening'inia mahala akisubiria msaada alafu RC anawahi kuoga maji ya moto yaliyo pashwa kwa umeme na bill zinalipwa na huyo aliyeachwa ananyofolewa na samaki huku anajiona. Kwa hoja dhaifu sana eti GIZA??????Kwakweli aibu kubwa kwa serikali ya Tanzania kwamba vikosi vya uokoaji havifanyi kazi usiku kwa sababu ya Giza?
Hivi hii serikali kweli inajari wananchi wake? Hivi mkuu Wa mkoa kama mwanao nae angekua kwenye hivyo meli ungediriki kutamka zoezi la.uokoaji limesitishwa?
Kama watu wanaweza kulowa dagaa usiku Wa manane tena kwa chemli mmeshindwa kuokoa watu?
Dah nimeumia sana namuwaza MTU yule ambae bado yuko hai ndani ya meli anasubiri uokozi
Namuwaza MTU yule ambae yuko hai ila analiwa na samaki akiwa anajiona mzimamzima, Leo ndio umetimia ule msemo Wa PAMBANA NA.HALI YAKO
Mkuu Wa mkoa anaenda zake kulala kashasema zoezi litaendelea kesho ambao bado mpo hai pambaneni na hali zenu
This is Africa😢😢😢😢😢
Mungu tusaidie
Binafsi nimeski
Binafsi nimesikia redio moja inaitwa Milele FM ya nchini Kenya inataja kuwa karibia watu 400 ndiyo walikuwa kwenye hicho kivuko japo sijui km ni kweli au LA!
Andiko hili linazidi kunitonesha sana, Nchini Kenya vyombo vya habari vimeripoti habari hizi haraka sana na kusitisha baadhi ya ratiba zao Mfano MILELE FM ya Kenya, TBC wako bize na kipindi cha miziki cha ZINAZO KIKI, inauma sana RC anaongezea kwa kusitisha zoezi kuwa GIZA limeingia. MTU aliyelelewa kwenye utamaduni wa KITANZANIA unapata wapi ujasiri wa kuingia kitandani ukalala wakati Wanadamu wenzako wawe maiti au hai unajua wako majini? Zaidi we ni kiongizi kwenye dhamana ndani ya mkoa. Kama Mh Rais aliwahi kukiri kuwa huwa anafanaya kazi hadi usiku kucha sasa wewe RC ujasiri huo wa kusitisha kuopoa maiti au watu hai ukaenda kumkumbatia mkeo unatoka wapi.NIMEUMIA SANA
Anaandika Kijana Msomi
Rashid Chilumba
Nimesikia zoezi la uokoaji kwenye ajali ya kivuko Mwanza limesitishwa hadi kesho kutokana na kiza, sasa kesho mtakwenda kuokoa au kuokota Maiti?
Hapo Mwanza kuna kikosi cha Jeshi, boti za doria za polisi, helikopta na vivuko vingine? Hivi kweli vyote hivyo havina taa kubwa za kuwezesha zoezi la uokozi kuendelea usiku kucha? Kama havina tulivinunua vya kazi gani?
Ni aibu kwa viongozi kusema tunaenda kulala eti kuna giza ziwani wakati kuna dazani ya watanzania wenzetu tunaowahudumia wamezama ziwani tena siyo kwa uzembe wao bali kwa ujuba na tabia ya kutokujali maisha ya watu na kutosimamia usalama wao.
Mkuu wa mkoa, RPC, mkuu wa kamandi ya Jeshi la Wananchi, Mkuu wa Bandari Mwanza mnapata wapi ujasiri wa kwenda kulala na kuna watu watoto wao, baba zao, Mama zao wamo majini na hawajui kama watawapata wakiwa hai? Hivi ingelikuwa ni jamaa zenu wa karibu mngepata ujasiri wa kusimamisha zoezi kwa sababu ya kiza?
Katika dunia ya leo seriously kabisa mnasema kiza kinawazuia kuokoa watu? Aiseee.... Kwa hiyo hao waliozama ikiwa kwa bahati bado wapo hai hadi sasa mnategemea Israeli atawangoja ninyi hadi kesho jua litapochomoza? Huu ni uzembe wa hali ya juu mno.
Kweli kabisa mnashindwa kufunga tochi kubwa kama zile za bandari kwenye helikopta moja ya polisi hapo na boti nne tano mkaingia kuwaokoa watanzania wenzetu? Hata ikiwa ni wafu lakini faraja ni kupata japo miili yao hadi kesho samaki, mawimbi ya ziwa nk inaweza kuwa imewapoteza zaidi.
Leo nimeumia sana, makosa yale yake ya Mv Bukoba, Spice Islander, Skagit yamejirudia Mv. Nyerere na watu wanaenda kulala usiku umeingia na vyombo vya habari vinaonesha shilawadu na kutoa dakika kiduchu kwa habari muhimu na msiba mkubwa huo wa taifa.
Na tena mlionywa mara kadhaa kuwa chombo ni kibovu. Mkuu wa bandari ya mwanza bado yupo na wadhifa wake na msimamizi wa Sumatra kanda ya ziwa kesho ataenda pia ofisini.
Mungu awapumzishe waliotangulia na atawalipa waliowasababishia kuzama kwenu kwa uzembe wao.
Cc
Dotto Bulendu
Malisa GJ
Kheri James
Tusaidiane kusema Ndugu zangu. Tunawezaje kwenda kulala na watanzania wenzetu wako majini sasa hivi?