Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Inasemekana kivuko cha watu 100 kilikuwa na watu zaidi ya 400,hakuna takwimu sahihi kwa chombo nyeti kinachobeba maisha ya watu.
Waafrika bado tuna safari ndefu sana
Basi hii ajali itakuwa imemeza watu wengi sana tutegemee msiba mzito sana
 
Hivi boti za doria za polisi na JWTZ hazina taa, mbona zina tochi kubwa kwa juu zenye uwezo wa kumlika zaidi ya mita 200.

Hizo boti zipo ni juzi tu tulitangaziwa kuwa serikali imenunua boti za doria za kisasa na kupelekwa ziwa Vitoria na zanzibar.
Upuuzi tu unaandika wewe walahi!
Vikao vya kahawa vinakufaa sana walahi
 
Akili za viongozi wa awamu hii ni Mungu tu ndiye anayezijua, hivi utasitishaje kuokoa mtu anayetapatapa kujiokoa kwenye maji, mtu ambaye ukichelewa hata kwa dakika moja tu anazama, halafu useme subiri nitakuja kesho asubuhi, inaingia akilini kweli?

Ningekuwa mimi Magufuli wote waliohusika na kusitisha kazi ya kuokoa leo wasingeingia ofisini.

RIP waliotangulia mbele ya haki, ugua pole majeruhi.

View attachment 872858
Hii kauli imeleta kichefuchefu sana, atumbuliwe huyo mkuu wa mkoa
 
Siku zote Upinzani ndiyo unatetea Mambo ya Msingi, lakini wa CCM na Wingi wao hawana faida yoyote.
 
Labda wangebaki ili kufurahisha watu kuwa bado wanaendelea na zoezi la uokoaji. Hivi kivuko kilichozama chote toka muda huo ndani ya maji, kuna mategemeo ya kumtoa mtu akiwa bado anapumua baada ya masaa takriban kumi?
Uokoaji ni fani pia, siasa ziwekwe kando. Na baada ya masaa kadhaa kupita, halikuwa zoezi la uokoaji tena. Maiti haiokolewi.
 
Ajali nyingi ni maksudi,mungu azilaze roho za marehem mahali Peponia peponi ameni
 
Samahani kwa kusema hivi ila ninadhani kwa namna fulani waokozi walikua sahihi kusitisha zoezi kwenye mazingira yafuatayo:-

Kama teknolojia na njia zetu za uokozi si fanisi kwa wakati wa usiku, hivyo kuendelea na uokozi inakua si salama kwanza kwa waokoaji wenyewe na pia mafanikio yake ni madogo mno, ni afadhali kusitisha zoezi hadi kutakapokucha.

Hakuna anayenufaika na vifo vya ndugu zetu, sitaki kuamini kwamba zoezi lilisitisishwa "JUST FOR LEISURE", kwa sasa bado hatuna uwezo mkubwa sana wa kufanya uokozi wakati wa usiku, na isingekua habari njema leo hii kusikia kwamba tumefanikiwa kuokoa wawili na tumepoteza waokozi nane.

Mwenyezi Mungu atupe nguvu na roho ya ustahimilivu watanzania katika kipindi hiki kigumu. Amen
Nikukumbushe tu 90% ya wavuvi wanaingia ziwan usiku na kutekeleza shughuli zao usiku,,,na tecnologia ya kuzuia Giza mkuu inakua tatizo?.. Boti za kuwasaka wavuvi haramu zipo kibao na zinafanya kazi 24HRS ,,ila za kuokoa watu ambao na hakika baadhi walikua hai hazipo
 
....

Tungechukua tahadhari kabla kuzuia matatizo kama haya.
1. Inasemekana kivuko kimefanyiwa ukarabati miezi kama miwili iliyopita kwa kuwekewa injini mpya za thamani ya milioni 190 ( kama sijakosea).
2.Tahadhari nadhani ambayo haijazingatiwa itakuwa ni uwezo halisi wa kivuko kubeba mzigo na mzigo halisi uliobebwa. Hata hivyo kuhusu uwezo wa kivuko unaweza kutupa elimu maana kwa jinsi ulivyokokotoa uwezo wa vivuko unaweza kutusaidia kivuko hiki kilikuwa na uwezo kiasi gani. Kwani kwenye pointi hii ulikazia kabisa kuwa " haiwezekani"!
3.Pia kitendo cha kutojua idadi kamili ya abiria haikubaliki wakati siku hizi naona wanatoza nauli na kutoa tiketi za electronic. Lazima kumbukumbu ziwepo vinginevyo kuna udanganyifu mkubwa unafanyika.
4.Kuna uwezekano wa kuwa labda ni majanga ya asili, kwani kipindi hiki kumekuwa na upepo wenye kasi kubwa na wa kushtukiza. Hata hivyo(kama ajali hii imetokana na upepo) hii inaonyesha yawezekana hakuna ushirikiano wa kutosha kati Mamlaka ya hali ya hewa na wamiliki wa vivuko(TEMESA) ama wamiliki na makapteni wanapuuzia taarifa wanazopewa na wataalamu wa hali ya hewa.
6. Nimakosa kuingiza masuala ya kisiasa tena ambayo hayana ushahidi kwenye masuala ya majanga kama haya. Vinginevyo, ieleweke kuwa unakusudia kuhujumu utawala sa serikali ya sasa kwa kuigombanisha na wananchi kwa malengo " maalumu". Kama huna lengo hilo jitahidi kukwepa kutumia maneno yanayoweza kuashiria hilo.
===
Inauma sana taifa kupoteza watu wake kwa namna hii.
 
20180921_065239.jpg
20180921_065239.jpg


BBC asubuhi hii.
 
Binafsi nimeski
Binafsi nimesikia redio moja inaitwa Milele FM ya nchini Kenya inataja kuwa karibia watu 400 ndiyo walikuwa kwenye hicho kivuko japo sijui km ni kweli au LA!
Inawezekana...Meli zote zinakuwa na mstari wa usalama.ambao maji hayatakiwi yauguse huo mstari...maji yakiugusa inamaanisha uzito umezidi.. Tatizo ni stability.,,Meli ilikata kona vibaya/ ghafla hivyo mizigo ikahamia upande mmoja, ikakosa balance ikapinduka...
 
Akili za viongozi wa awamu hii ni Mungu tu ndiye anayezijua, hivi utasitishaje kuokoa mtu anayetapatapa kujiokoa kwenye maji, mtu ambaye ukichelewa hata kwa dakika moja tu anazama, halafu useme subiri nitakuja kesho asubuhi, inaingia akilini kweli?

Ningekuwa mimi Magufuli wote waliohusika na kusitisha kazi ya kuokoa leo wasingeingia ofisini.

RIP waliotangulia mbele ya haki, ugua pole majeruhi.

View attachment 872858
Hivi wale mapolisi na wanàjeshi wenye nguvu nyingi za kudhibiti mikutano ya chadema, wizi wa kura na kusherehekea ushindi wa ccm hawana hata Helikopita za kuokoa watu wakati wa majanga??

Mbona siwaoni wakitumia intelijensia yao kwenye hili??
 
Back
Top Bottom