Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

It always gets better before it gets worse. This is Tanzania
 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mazishi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Mv.Nyerere iliyotokea Septamba 20 huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza yatakuwa ya kitaifa ambapo viongozi wakuu wa kitaifa wanatarajia kushiriki mazishi hayo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe.
Akiongea na ITV Mhandisi Kamwelwe amesema shughuli za mazishi hayo zitagharamiwa na Serikali na kwamba utaratibu kamili wa eneo yatakapofanyika mazishi hayo utatolewa baadaye.

Hata hivyo Mpaka sasa zoezi la uokoaji na uopoaji wa miili ya watu waliokuwa kwenye kivuko cha MV.Nyerere linaendelea ambapo miili 94 ya watu imeopolewa na waliookolewa wakiwa hai wanazidi 40.

Vikosi vya uokoaji mkoa wa Mwanza vimeongezewa nguvu na vikosi vya mkoa wa Mara katika eneo la tukio ili kuongeza kasi ya kuopoa miili ya watu waliopinduka na kivuko hicho.

Aidha uongozi wa wakala wa meli mkoa wa Mwanza umetambua wafanyakazi wa kivuko watano ambao wamepoteza maisha akiwemo nahodha, fundi, Karani, mlinzi na mkuu wa kivuko, Kivuko hicho kilikuwa na wafanyakazi wanane.

Mamia ya wakazi wa Ukerewe wamekusanyika nje ya kituo cha afya cha Bwisya kutambua miili iliyoopolewa kwenye ajali ya kivuko cha MV.Nyerere iliyotokea wakati wakisafiri kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Ukara kwenye gulio.

Mwandishi wetu aliyepiga kambi katika eneo hilo ametueleza kuwa wengi wa walioopolewa hadi sasa ni wanawake.
CCM anzeni kujiandaa kwa jezi na bendera zenu kwani hao walikuwa wapigakura wenu.
 
Ila hii ishu ya kuuana kwa makusudi au sijui nimeseme kuuana na kujiua wenyewe sijui itaisha lini, hata mv bukoba tatizo lilikuwa ni kuzidisha watu, na hii nayo hivyo hivyo, hivi kweli kivuko cha kubeba watu 100 kinabeba watu 400? hakuna ukaguzi kwenye hivyo vituo?
mambo mengine ni magumu sana kulaumiana. mfano unakuta hakuna kitabu kinachoonyesha kuwa tiketi zitauzwa 100 tu. na zikiisha hakuna zingine. mfano tena unakuta hakuna mtu wa kukagua kama kila anaeingia ana tiketi. mfano wa tatu ni pale ambapo hakuna mashine ya kupima uzito mizigo inayoingia. na shida yetu sisi watanzia kinachotuponza ni huruma. mtubanakuambia nisiposafiri leo nitakosa hata pa kulala na sina hela hata ya kula halafu anaonewa huruma anaingia. matokeo yake tunajazana. ila mtu angejua kuwa kosa la kujaza hata mtu mmoja zaidi ni kufukuzwa kazi asingekuwa na huruma.
 
Na waziri wangu uelewe kuwa ni haki ya waliofiwa kujua wapendwa wao walikufaje(tungekuwa tupo kwenye nchi ya kujielewa uchunguzi yakinifu ungefanywa kubaini whats went wrong na nani atawajibika maana ajali its someone FAULTY sio kazi ya Mungu,na je kuna uwezekano wa serikali kushitakiwa kwenye kwenye kesi ya madai au criminal kwa kusababisha hivi vifo au itakuwa ni cold case kama ya MV BUKOBA?
 
mambo mengine ni magumu sana kulaumiana. mfano unakuta hakuna kitabu kinachoonyesha kuwa tiketi zitauzwa 100 tu. na zikiisha hakuna zingine. mfano tena unakuta hakuna mtu wa kukagua kama kila anaeingia ana tiketi. mfano wa tatu ni pale ambapo hakuna mashine ya kupima uzito mizigo inayoingia. na shida yetu sisi watanzia kinachotuponza ni huruma. mtubanakuambia nisiposafiri leo nitakosa hata pa kulala na sina hela hata ya kula halafu anaonewa huruma anaingia. matokeo yake tunajazana. ila mtu angejua kuwa kosa la kujaza hata mtu mmoja zaidi ni kufukuzwa kazi asingekuwa na huruma.

Ndo mana nikahoji hakuna ukaguzi? Mana ukaguzi ukiwepo utazingatia yote hayo uliyosema
 
hatutaki kusikia idadi ya majeneza tunataka kujua chanzo halisi cha ajali na wahusika wajipime
 
Yep! They deserve a state funeral... In the end of the day, every one will go... No one will live forever...
 
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesitisha ziara yake iliyokuwa ikiendelea mkoani Dodoma katika wilaya ya Chemba na kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwafariji na kufuatilia tukio la ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV.Nyerere ambapo mpaka sasa wawtu 125 wameripotiwa kupoteza maisha
 
Jamani mlitaka sfanye nini wakati hakuna vifaa vya kuokolea muda huo?? Na sio kwamba atakuwa alijiamulia tu mwenyewe, hao wazamiaji hawana vifaa vya kufanyia kazi kwenye mwanga itakuwa gizani?? Ni aibu kwa nchi, hatuko tayari kwenye majanga!! Ya nchi kavu tu yanatushinda itakuwa ya majini??
Kusema vifaa na giza ni hoja dhaifu sana.
Muda ajali imetokea haukutosha kwa kamati ya maafa mkoa wa Mwanza au kitaifa kuandaa vilivyohitajika ili kuongeza ufanisi wa zoezi zima la uokozi!?
 
mungu awape faraja ndungu waliopotelewa na ndugu zao kwani nikatika majuz mazito yaliyo wakuta. yakisababishwa na viongoz wanaopenda kukaa maofisin na kuzungumza mambo kisiasa na sio kiutendaji' ukifatilia walishapewa ahad nyingi kwamba kivuko kitatengeneza lakin kwa hili utaona ukaguz wa mara kwa mara utatokea.
 
Back
Top Bottom