Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ndugu wanabodi:
Hivi sisi Watanzania nano katuloga? TBC na vyombo binafsi vimeshindwa kujiunga mubashara kwenye shughuli ya uopoaji maiti lakini hats kupiga nyimbo za maombolezo imeshindikana kweli?

Nimesema shughuli ya uopoaji kwa sababu serikali ingekuwa serious na maisha ya Watanzania wenzetu ingepeleka jenereta jana ili shughuli ya uokoaji iendelee Jana usiku.

Watanzania zaidi ya 126 ni msiba mkubwa wa taifa lakini radio na luninga ya taifa wameshindwa kujiunga mubashara hatua kwa hatua badala yake wanaendelea na mambo yao yasio na maslahi kwa Taifa.

Naamin kwa Wazungu habari ingekuwa ndio hiyo kuwa mubashara muda wote kwa kila kituo cha luninga na redio.Na wasingekubali kusitisha shughuli ya uokoaji eti kisa giza

Tumeshindwa kuthamini uhai wa wenzetu, kweli ngozi nyeusi ni wabinafsi haijapata kutokea
Watanznaia wengi wanajali starehe, burudani, kuliko KUOMBOLEZA na wengine. Nyombo vya habari media zetu zote ni mziki na vupindi visivyo na maana hasa katika wakati akama huu.
 
R.I.P kwa wote waliotuacha. Kuna watu tayari wamesahau kwamba kuna wenzao waliofiwa. Alafu Moderator huu uzi upeleke kwenye jukwa lake, sijaona habari zozote kuhusu Kenya.
 
Watu wengi wamepoteza Maisha,tuko pamoja nao ndg Wa marehemu pia tunatoa pole kwa wafiwa wote
Nalog off
 
Hiyo saf inatoka wap mkuu

Mbona unakua mbumbu na ziro kichwan kias hcho ...

Huwa nafikiria sana hivi una hata mama wewe au mdg

There is no line btn you people and witches
Usijisumbue kumjibu mtu kama huyo, huwa natamani nimjibu ila huwa namjibu tu kimoyo moyo maana nikifikiria namuonea huruma.
 
Hivi, unafahamu kwamba kuna vyanzo vya uhakika vinasema kwamba abiria walokuwamo humo kwenye kivuko ni zaidi ya 200?

Na pia hakuna anaefahamu zaidi ikwamba inawezekena abiria wakawa zaidi ya 400 aana wengi walokuwa wakienda gulioni?

Sasa waziri wa uchukuzi anaingiaje hapo?

Cha msingi ni kwamba kivuko ni kizima na hakikuwa na kasoro yoyote ile kwani hivi karibuni kilipata injiini mbili mpya.

Suala linaanzia kwenye msimaizi wa hicho kivuko ambae anasimamia kwamba ni tiketi ngapi ziuzwe na abiria wangapi waruhusiwe kuingia kwenye kivuko.

Hivyo usimamizi kwamba kivuko kinabeba uzito upi, namba ya abiria, mizigo na korokoro zingine si jukumu la waziri.

Hilo ni jukumu la wasimamizi wa kivuko ambao ndo wanapaswa kuwajibishwa.
Umeongea vizuri sana. mimi nami nimetoa yangu. Basi UCHUNGUZI uanzie hapa na kuendelea.Then kila aliyezembea awe ni nani
awajibishwe.Hiyo ndo maana yangu kuu.
 
Media za TZ zimeshachapwa bakora mpaka zimepoteza uwezo wa kufikiri. Ni sawa na mbwa anayepigwa kila siku anavyokuwa mbwa mjinga mjinga.

Na siyo media tu, angalia hata wanaohusika hawajatangaza taifa liko kwenye msiba na bendera ziwe nusu mlingoti.

Jamani, Nyerere alisema taifa la watu waliotishwa mpaka kuwa magoigoi siyo riziki.
Walau kuanzia asubuhi bendera zingekuwa nusu mlingoti! Sijui nchi hii uongozi wake hasa awamu hii umelogwa na nani!
 
Back
Top Bottom