Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kwa taarifa za jana vifo zaidi ya 200, hope waliowajaza watu kwenye feri watahukumiwa kama wauaji ili iwe fundisho kwa wengine
 
Nawapa pole wafiwa wote na Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi!
Nianze kwa kukataa misemo maarufu ya kusema ni kazi ya Mungu na haina makosa...
Hii ajali inaonekana kuna uzembe wa hali ya juu, uwezo wa kivuko ni kubeba abiria 100 iweje kivuko kibebe watu zaid ya 400?
Hizi ni ajali za kujitakia safety rules hazifuatwi alafu mnasema kazi ya Mungu?
Ni nani alaumiwe?
Vyombo husika vya serikali, Temesa, sumatra, RC, Dc ,waziri wa wizara husika mlikua wapi???
 
PM na mawaziri wote walipwe nusu mshahara mwaka mzima.
Wabunge wote walipwe nusu mshahara mwaka mzima na no sitting allowance.
Wizara ya mambo ya ndani na agency zake zote nusu mshahara mwaka mzima.
Wizara ya ujenzi na uchukuzi na agency zake zote nusu mshahara mwaka mzima.
Ofisi ya waziri mkuu na agency zake kama zipo nusu mshahara mwaka mzima.

Halafu uone kama kuna uzembe utatokea tena na kuua watanzania wasio na hatia.
 
Kipindi tunaelekea kwenye mazishi... Wakuu wa vitengo eti bado wako ofisini.
Kwa uzembe huo TUTASUBIRI SANA
 
Hadi sasa nimekaa hapa najiuliza viongozi wa huko SUMATRA wanasubiri nini kujiuzulu au wanataka kufukuzwa ? Mambo mengine ni suala la uwajibikaji tu siyo moja kwa moja uwe na makosa au la.
Sumatra yeye ni mkaguzi na mdhibiti wa shughuli vyombo vya majini wa kutoa leseni za meli au kivuko.Lakini msimamizi wa shughuli za kila siku za uangalizi wa shughuli za meli na kadhalika si Sumatra bali State Port Control ambae ni Mamlaka ya Bandari TPA labda kama kuna mabadiriko.
Kila Bandari iliochini ya TPA inatakiwa kuwa na Afisa wa Bandari wa kushughulikia maswala ya usalama wa vyombo,mizigo na abiria.
Sumatra atawajibika tu kama alitoa leseni ya chombo kinyume cha utaratibu.
Wengine wanatakiwa kupewa kibano
1.TAMEESA ambe ni operator wa kivuko kwa niaba ya serikali.
2.Mamlaka ya Bandari TPA
3.Police Marine
4.Wizara ya Uchukuzi.
Lakini mara nyingi kuna mkanganyiko wa shughuli za Mamlaka ya Bandari na Sumatra ipo haja ya kurekebisha utata.
Je kazi za Search and Rescue ipo JWTZ au Police Marine au TPA?
 
Screenshot_2018-09-23-08-43-02-1-1-1.png

Wakati rais amenyoa nywele zote kichwani na kunyoa/kuondoa 'O' yake kwa ajili ya kuomboleza msiba huu, eti Waziri mkuu yeye bado anaendelea kupaka Piko lile Afro lake huku wateule wengine kama wakuu wa wilaya na mikoa hakuna hata mmoja anayeiga style ya mkuu katika kuomboleza.
Wao wanachoweza kuiga ni ubabe na kamata kamata sababu vinawafanye waogopeke lakini kunyoa hawaigi kisa wataonekana vituko.
 
225 + 41= 266
Dc ukerewe alisema kilipakia zaidi ya watu 400..

bado wengine takribani watu 134 kwa mujibu wa DC , aisee tumepoteza watu wengi mno[emoji24][emoji24]
 
Just imagine capacity yake ilikuwa watu mia, ina maana kila wakati walikuwa wakiwasilisha mauzo ya 100 lkn wanabeba zaidi ya abiria 300, hii excess ilikuwa inawakilishwa kwa nani? je, mizogo excess ilikuwa inawakilishwa kwa nani? tunapofanya uchunguzi wa hili jambo turudi juma kuuliza walianza kubeba hii excess tangu muda gani na walikuwa wanaiwakilisha kwa nani? iundwe tume kuchunguza kwanza hizi pesa zilikuwa zinaenda kwa nani, na hao watu wakamatwe na wafilisiwe. Mods msiunganishe huu uzi, tuanzie hapa kwa uchunguzi ili wale samaki wakubwa wapatikane.
Tatizo linaanzia hapo,kulikuwa na pesa chafu.Ukipakia zaidi unapata zaidi.Lakini yawezekana pia hiyo pesa chafu ilitumika kuzuia vyombo au watu husika kudhibiti upakiaji wa abiria na mizigo iliokidhiri.
 
Ndo Jana wamepeleka bulldoza la kuivuta nchi Kazi ilitakiwa siku ile ile kuivuta isingelala majini kwenye mita mia tujifunze,ajali ile kwa dunia ya sasa ni uzembe tuwekeze zaidi kwenye rescue team
 
View attachment 875039
Wakati rais amenyoa nyweke zote kichwani na kunyoa/kuondoa 'O' yake kwa ajili ya kuomboleza msiba huu, eti Waziri mkuu yeye bado anaendelea kupaka Piko lile Afro lake huku wateule wengine kama wakuu wa wilaya na mikoa hakuna hata mmoja anayeiga style ya mkuu katika kuomboleza.
Wao wanachoweza kuiga ni ubabe na kamata kamata sababu vinawafanye waigopeke lakini kunyoa haqataki k8sa wataonekana vituko.
Kunyoa ni imani ya MTU wala hakuna uhusiano Na majonzi
 
Tunajali Pesa kwanza usalama baadae we si unaona treni ya mwendokasi na vivuko vya Kigamboni ni majanga tunaishi kimazoea,
 
R.I.P.
Maisha yetu ni mfupi na yamejaa mahangaiko.
Mungu awarehemu wote walikufa kwa ajali hii na wenginewe....
Na wafiwa awape moyo wa uvumilivu... maana ni kujipanganga upya hasa kwa walio acha familia!
 
Ndo Jana wamepeleka bulldoza la kuivuta nchi Kazi ilitakiwa siku ile ile kuivuta isingelala majini kwenye mita mia tujifunze,ajali ile kwa dunia ya sasa ni uzembe tuwekeze zaidi kwenye rescue team
Wangeazima heavy military equipment wala wasingefika huko.....

Bora mwaka huu hawaja drill.....
 
Back
Top Bottom