Inasikitisha sana. Hivi inakuwaje unamfanyia binadamu mwenzako unyama kama huo kisa tu mmetofautiana itikadi? Ni lini watanzania tutafika mahali tuone kuwa kutofautiana itikadi jambo la kawaida tu kama ilivyo utani wa Simba na Yanga.
Na kama hizi taarifa ni sahihi kuwa alishambuliwa kwa kuwa alikuwa CHADEMA na taarifa zipo CHADEMA wilaya mpaka kanda hao viongozi wa Wilaya mpaka Kanda wamewajibika vipi kumsaidia kumpatia matibabu kamanda wao? Kama hawakuwa na uwezo wa kumapatia matibabu je wameshindwa hata kuhamasisha wanachadema walio karibu wamchangie matibabu kamanda mwenzao? Je hawaoni kuwa hii itawavunja moyo makamanda wengine kupambania chama chao?
Ushauri wangu kwa CHADEMA taifa kama mnapita hapa. Fanyeni juu chini tena haraka iwezekanavyo mmpatie matibabu kamanda wenu kwani mambo kama haya yanawavunja moyo makamanda wenu. Maana mtu anafikiria nikapambanie chama halafu nikipata tatizo familia ndio inihudumie na kama familia haina uwezo ndiyo imetoka hiyo.