Inaitwa Brutal beer! Jina moja la kibabe sana! Yaani
BIA KATILI
Kama hujawahi kuiona kwa sura unaweza kuogopa sana.. Lakini once unapoiona unaanza kupata mashaka
.Chupa yake ni ndogo halafu kimodo
. Rangi yake ni pink iliyofifia
. Ladha yake ni ya matunda
. Kilevi chake ni asilimia 5%
Kwahiyo sasa ukatili wake unatokana na nini? BEI!
Kimoja kinauzwa Tsh. 5000! Kinanywewa na wadada wa mjini kwa asilimia 99.. Ni kilevi laini sana lakini bei ni katili
Ukatili wake uko kwenye mfuko wa mlipaji.. Michepuko inavipenda sanaššæš! Akija na mashosti wawili wakanywa tano tano tuu ni laki kasoroš
Na vilivyo laini wanaweza kila mmoja akamaliza 10 pekeyakeš„ŗ
View attachment 3540971View attachment 3540972