Elections 2015 UKAWA na Lowassa unganeni mchukue nchi, wakati ndio huu, mkipuuzia huu ushauri basi tena!

Hivi UKAWA hakuna mtu anaetosha kuwa rais mpaka kuingia katika hali ya kutaka kukodi mtu.
Kweli upinzani haujajipanga kuchukua nchi
 
Naona thread nyingi sana za kusisitiza Lowasa ahamie ukawa. Hivi akihama, anahamia peke yake? Mnajua rafiki zake lowasa waliokuwa wanamchangia? Huyu abaki huko huko au aende ACT. Kwenda ukawa itakuwa ni sawa na kutia doa kwenye nguo nyeupe..

ACT haipokei wahujumu uchumi.....kabla ya uchaguzi wa CCM, CDM wote mlikuwa mnashadadia Lowasa akikatwa anaenda ACT leo hii imedhihirika wazi lengo la viongozi wenu.....sasa wanafiki na wasaliti halisi wa watanzania wanaanza kuonekana upenuni kabisa.
 
Tusisahau ndo hawahawa waliyokuwa wanapiga debe ACT ijiunge ikawa. Wanaangaikaga sana. Poleni
 
wala watu chadema hawajakataa lowassa kuhamia,ila ni kama mwanachama.ni ujinga kufikiri ukawa inaweza kuamka tu usingizini na kumpa lowassa kuwa mgombea kupitia ukawa!!
 
mkuu hutompigia wewe lowassa akija ukawa na kugombea urais lakini sisi tutampigia tena kwa ushawish na nguvu zote, karibu sana lowassa ukawa ujisafishe tukupe mikoba.
kama kweli ni mwanachama wa chadema,basi nadhani unafuata mkumbo tu,hujui falsafa ya chadema na kipi chadema inasimamia.
 
Ficra inabidi zibadilike kwa haraka tufanye maamuzi ya kuchukua nchi . Kubalini Low as a aje tupasue anga .
 
sisi kina gogo la shamba baada ya kufikiri sana tunaungana na wananchi wanaopendekeza Lowasa akaribishwe UKAWA na ikiwezekana apewe nafasi ya kugombea Urais maana lengo ni kuiondoa ccm madarakani mengine yote yatafuata baada ya ccm kuondoka madarakani nina imani kwa alipofikia Lowasa anaweza kubadilika na akawa rais mzuri sana kwani atakuwa amezunguukwa na watu wenye nia njema na nchi yetu
 

UKAWA wakimchukua lile kosa la kuanza kampeni mapema litakuwa limefutika? Huu ni mtego mwingine, wakimchukua ataondolewa kwa na TUME YA UCHAGUZI kwa kosa la kuanza kampeni kabla ya muda uliowekwa kisheria. Safari zake zote za kutafuta wadhamini ilikuwa ni mikutano ya wazi kwa maana ya kampeni
 
Macho na masikio ya watanzania wanasubiri kwa hamu kubwa kutangazwa rasmi mgombea uraisi kupitia #UKAWA rasmi kesho .
UKAWA NDO TUMAINI JIPYA KWA WATANZANIA WOTE.mkuu Pasco umeshapitia humu safari ya matumaini bado inaendelea?
Niliisha shauri.
Baada tuu ya jina la Lowassa kukatwa kwenye 5 bora, nilipandisha uzi huu, Kukatwa Kwa Lowassa, Jee Ndio Mwisho wa Ile Safari, Au..., nikishauri ahame CCM safari iendelee, huku nikitaraji atakayepita ni Membe!.

Lakini baada ya kupitishwa Magufuli, nilifanya about turn na kumshauri sasa atulie tuu, kwa sababu Magufuli ni jembe zaidi ya Lowassa!. Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali yaishe, vunja kambi na kujisalimisha!.


Pasco
 

MYSTERY,
Sikubaiani na wewe kwamba EL ametoswa huko CCM kwa sababu ya ufisadi. Tujikumbushe ni skendo ngapi za ufisadi zimeigubika nchi bila EL kuwepo kwenye system? Escrow kwani EL alikuwepo? Ndege ya Rais? uingizwaji wa sukari kfisadi? Ukaguziw wa magari nje ya nchi kabla ya kuingizwa nchini?

Tukisema CCM imejisafisha kwa kumtosa EL hizi ni ghiriba kwani system nzima ndani ya CCM imeoza. EL akaribishwe ukawa awaeleze watz uhusika wake kwenye Richmond kasha akieleweka atumike kama siraha ya maangamizi kuiondoa CCM madarakan
 

Very objective!. Tatizo la UKAWA ni kukosekana kwa watu wenye uelewa wa level hii!

Pasco
 
Ushauri mzuri saaaaaana ulotoa maana hakuna njia nyingine ya kuwatoa CCM zaid ya kuongeza nguvu ya Lowassa
 
Lowassa ni backup nzuri kwa ukawa, uongozi ni mfumo siyo rais! Fikra zenu sasa zilenge kuondoa mfumo mmoja na kuweka mfumo mwingine kama USA na siyo kujikita tu kwenye agender ya urais.
 
kumbe ukawa hawana mgombea!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…