Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona thread nyingi sana za kusisitiza Lowasa ahamie ukawa. Hivi akihama, anahamia peke yake? Mnajua rafiki zake lowasa waliokuwa wanamchangia? Huyu abaki huko huko au aende ACT. Kwenda ukawa itakuwa ni sawa na kutia doa kwenye nguo nyeupe..
wala watu chadema hawajakataa lowassa kuhamia,ila ni kama mwanachama.ni ujinga kufikiri ukawa inaweza kuamka tu usingizini na kumpa lowassa kuwa mgombea kupitia ukawa!!mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga lowassa asichaguliwe ccm sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa ukawa. Angepitishwa lowassa ukawa ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata slaa alivyokatwa ccm alihamia chadema.
Nawaomba chadema na ukawa msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.
Kama lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya ukawa mtauona mtikisiko wa hii nchi.ukawa watabeba kila kitu kuanzia ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa richmond naamini akiwa chadema atakua huru kusema.
Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe ccm madarakani nyuma ya lowassa kuna watu wengi sana.narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.
kama kweli ni mwanachama wa chadema,basi nadhani unafuata mkumbo tu,hujui falsafa ya chadema na kipi chadema inasimamia.mkuu hutompigia wewe lowassa akija ukawa na kugombea urais lakini sisi tutampigia tena kwa ushawish na nguvu zote, karibu sana lowassa ukawa ujisafishe tukupe mikoba.
Masikin nchi yangu haina wapinzan bali waganga njaa...a.k.a waroho wa madaraka
Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.
Nawaomba CHADEMA na UKAWA msipoteze hii turufu huyu mtu bado yupo vinywani mwa watu wengi.Bado ana influency kubwa kwenye media ambacho ni kitu muhimu wanaomkataa asipokelewe hawaijui siasa.
Kama Lowassa akipokelewa akapeperusha bendera ya UKAWA mtauona mtikisiko wa hii nchi.UKAWA watabeba kila kitu kuanzia Ubunge hadi urais. Lowassa anatakiwa atoke hadharani aeleze uhusika wake wa Richmond naamini akiwa CHADEMA atakua huru kusema.
Ni bora ushirikiane hata na shetani ili mradi uitoe CCM madarakani nyuma ya Lowassa kuna watu wengi sana.Narudia tena kwa wanachadema wenzangu siasa haina rafiki wala adui wa kudumu.
Kama lengo kushika dola shirikiana hata na shetani umalize mchezo, kama lengo ni kupinga ufisadi tutabaki hivi hivi tunapinga ufisadi huku tukiwa wapinzani, vita ni vita tu.
Ritz bana!
Niliisha shauri.
I agree
Lowassa ingia chadema/ukawa
Magamba in action.
Kwa kuwa tunajua nchi yetu tunayo TISS ambayo moja ya jukumu lake kubwa ni kuhakikisha kuwa Sisiemu inatawala daima.
Inaelekea hii hoja ambayo imeibuka kwa nguvu sana katika siku 2 hizi humu JF kabla Ukawa hawajamtaja mgombea wao itakuwa ime-originate kutoka huko.
Hivi inawezekanaje Chadema ambayo imejipambanua na agenda yao kuu ya kupambana na ufisadi wa CCM kwa nguvu zote sasa impokee mtu kutoka CCM ambaye anafahamika kama fisadi papa?
Hivi inawezekanaje mtu ambaye hata Chama chake mwenyewe kilimuita kuwa ni fisadi papa na chama hicho kikampa jukumu Nape ambaye alizunguka nchi nzima kuwatangazia wananchi kuwa mafisadi papa watatu (akiwemo Lowassa) wamepewa siku 90 na chama chao ili wajivue gamba sasa ndiyo Chadema kimpokee kama shujaa wao anayetakiwa kuwapeleka Ikulu?
Kwa hiyo huku kupigiwa debe kupita kiasi humu JF siku 2 hizi ili Chadema impokee fisadi Lowassa kwenye chama chao ni mpango madhubuti ulioandaliwa na Sisiemu kupitia kitengo 'chao' cha usalama wa Sisiemu.
Huyo jamaa mahali pekee panapomfaa kama kweli atataka kuondoka CCM si pengine bali ni kwenda kwenye chama cha 'swaiba' wake, chama cha AKTI.
Ndugu Wananchi,
Mimi kama mdau wa siasa na mzalendo kwa nchi yangu naomba nitoe ushauri ufuatao kwa UKAWA pamoja na Lowassa. Najua kuna watu inaweza ikawa ngumu sana kuelewa point yangu, lakini wenye ufahamu na mambo ya siasa na mapinduzi wataona point yangu.
Naomba nimalizie kwa kusema kwamba hii ndio nafasi pekee ya CCM kuondolewa madarakani. Na njia pekee ni kupitia kwa Lowassa na UKAWA. Chadema na UKawa kubalini huu ushauri na hakika watanzania tuko nyuma yenu, kwani tunaamini kwamba uchumi wa Tanzania utabailika kwa mfumo ulio nje ya CCM na CHADEMA na UKAWA wanaweza kutumia nafasi hii sasa ya kumkubali Lowassa ili tupate mabadiliko.
UKAWA mnatakiwa kuwa makini, acheneni na propaganda za watu wengi hapa JF na mkubaliane na hali halisi. Wakati ndio huu na mkiuachia basi watanzania wasahau mabadiliko kwa kipindi kirefu sana.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA.
Ahsanteni.
Ni mimi Mpenda nchi.
kumbe ukawa hawana mgombea!Mimi ni mmoja wa watu niliyekuwa nikipinga Lowassa asichaguliwe CCM sababu ni moja tu alikuwa threat kubwa kwa UKAWA. Angepitishwa Lowassa UKAWA ingebaki historia siasa haina rafiki wa kudumu wala adui hata Slaa alivyokatwa CCM alihamia CHADEMA.