Source please!
Ila siyo mbaya kama itatokea.
Tunarudia ,wapinzani walipokwenda IKULU hawakuambulia chochote zaidi ya kunywa juisi ya maembe.
Hili nalo neno, neno zito.Safari hii hawataambulia hata juice.
Unadhani mwenye duka siyo mfanya biashara? Kwamba anagawa juice tuu?
Sana sana atawapa kipande cha sababu ya Mshindi wakaoge.
Maana maji ukiyavulia nguo, huna budi kuyaoga.
Simlamu Lipumba kutuma mwakilishi b'se ataendaje dukani uchi wakati tayari keshayavulia maji nguo?
Mkuu unazidi kulikoroga sasa nitakujibu kwa ufupi zaidi. Huwezi kutoka Ontario ukaenda kupiga kura Quebec pasipo wewe kuwa mkazi wa Quebec. Nilikwambia pia ya kwamba huwezi kwenda Quebec au jimbo lolote kugombea uongozi ikiwa wewe sii mkazi wa jimbo hilo wenzatu hawana makabila wala Uzawa isipokuwa ni raia na unaishi wapi.Nkaubaliana na Mag3 hapo juu kuwa Mkandara haeleweki ingawa anashangaa kwanini hatumwelewi.
Mkuu kwanza ukaazi wa Quebec au majimbo mengine sijui unazungumziaje kisiasa.
Unaweza kuhama kutoka Ontari ukaenda Alberta na kupiga kura kama ulivyo na haki ya kuchaguliwa. Ukaazi umewekwa kwasababu za mambo kama health care, haina maana ukienda Quebec unakosa haki kama raia wa Canada.
Nadhani unajaribu sana kutumia mifano ya huko uliko pengine ukidhani hatuna ufahamu huo.
Pili, unajichanganya sana unaposema undugu wetu ni wa karne. Undugu huo upo kwa Kenya, Msumbiji na Malawi kwa uchache. Hatuna muungano lakini tunaishi vema tu bila shaka.
Zanzibar hawapaswi kumwekea Mtanganyika kitambulisho cha ukazi. Wala hawapaswi kutangaza kuwa wao ni TAIFA nje ya hili tulilo nalo. Sasa wametangaza kuwa ni nchi ikiwa na kila kitu.
Hadi hapo mkuu muungano hakuna, unachotetea ni masilahi ya znz tu.
Nikupe mfano wa juzi. ZNZ wamepewa bilioni 15 zaidi mwaka huu kwasababu ya kodi ya wafanyakazi wa muungano wanaoishi Zanzibar. Wafanyakazi hao wanalipwa na Tanganyika kwasababu znz haina mchango na wala haijachangia takribai miaka 20 sasa.
Kwa maneno mengine, fursa za wznz kuishi Tanganyika ni pamoja na ajira za mambo yasiyowahusu. Na bado tunalipa mishahara hadi mawaziri wao wasiotuhusu.
Sasa tunawazawadia pesa za ili kuwatengenezea ajira.
Wale wabunge 81 wanaolipwa na Tanganyika, znz ina mchango gani.
Labda ueleze umma, hivi Mtanganyika anafaidika na nini na muungano huu zaidi ya mzigo wa gharama. Huenda kuna kitu hatuelewi.
Znz hawataki mambo yote yawe ya muungano ndiyo maana wanayanyofoa.
Wanachotaka ni jina ili wakija wadai kwa mgongo wa Tanzania.
Unapolaumu Tanganyika hutendi haki hata kidogo.
Mambo yote unayosema ni ya muungano huko nyuma umesema ni ya kinyemela na kuwaumiza wznz. Leo unasema yote ni ya muungano!
Hapa ndipo naungana na Mag3 kuhoji kama kweli mkuu unamahali pa kusimamia au ni shoot any moving object.
Kama wznz wameondoa mambo mengi, sisi tunasema basi 7 yawe yetu.
Kama hawataki hatuna sababu za kuwazuia, tunawaacha waendelee na mipango ya TAIFA lao.
Kwani mkuu, tukivunja jahazi na kugawana mbao kuna tatizo gani kwa Tanganyika, na pili, kwa znz?
Zanzibar si TAIFA la Tanzania? Period. Ukishafahamu hivyo utaelewa ulichosema hakina ukweli. Znz si taifa la Tanzania ni taifa la znz.Mkuu unazidi kulikoroga sasa nitakujibu kwa ufupi zaidi. Huwezi kutoka Ontario ukaenda kupiga kura Quebec pasipo wewe kuwa mkazi wa Quebec. Nilikwambia pia ya kwamba huwezi kwenda Quebec au jimbo lolote kugombea uongozi ikiwa wewe sii mkazi wa jimbo hilo wenzatu hawana makabila wala Uzawa isipokuwa ni raia na unaishi wapi.
Tena huko kuna record ya kila raia kiasi kwamba hata wanapokuja mlangoni wanajua nyumba hiyo wnaishi raia wangapi na majina yao. wanajua hadi wahamiaji wakazi wasokuwa na right ya kupiga kura huwezi kujipachika ati ukatoka Ontario kwenda kupiga kura Quebec. Tena basi kama hukujiandikisha kupiga kura itabidi uonyeshe vitambulisho vyote kuhakikisha wewe ni raia na mkazi wa nyumba au apartment uloitaja.
Acha hizi habari za kudhani dhani wakati hujui mfumo wa S3 unafanya kazi vipi.
2. Kuna tofauti kubwa sana baina ya MAMBO ya Muungano (NCHI) na Utekelezaji wa ShuGHULI za serikali (SERIKALI). Mambo ya muungano ni kuashiria Je, kuna MAMBO gani vimewaunganisha ili kuunda Taifa moja, kisha SHUGHULI za muungano ni mfumo wa utekelezaji wa shughuli zake hivyo ktk mambo ya Muungano wetu tunaweza kuwa pamoja kwa yote (wizara zote) ila ktk utekelezaji wa shughuli zake kila nchi inawajibika kusimamia mamlaka hayo kwa niaba ya Taifa zima, hivyo kuchangia mfuko wa Taifa kwa kila kodi inayopatikana. Serikali huendeshwa na kodi za watu sio serikali zetu zinazo hodhi na kufanya biashara kupitia migongo ya wananchi na mikataba ya 10%. Unaweza kuniuliza hao viongozi wanafaidika vipi ikiwa wao ndio wameleta wawekezaji na kadhalika! wewe mwananchi machinga unachangia nini!
3. Kama wewe huijui Historia ya nchi hizi basi sina sababu ya kuendelea na mjadala maana sii ajabu unajiuliza hata faida ya mkeo nyumbani ikiwa hana ajira inayoingiza fedha sawa na wewe. Bila shaka atakuwa mzigo kwako na hata watoto wako ni mzigo kama nitafikiria kama wewe..Lakini bahati mbaya fikra zetu hazifanani.
swadakta haya ndio maneno toka kwa mwananchi mwenye nia ya dhati kuitaka katiba Mpya ya JMT.Tuliwaambia ukawa, jambo la muhimu si kueleza ubaya wa muungano au tatizo la muungano.
Kilichotakiwa ni kuifahamu jamii na tatizo la mwanzo kabla ya kuingia katika mada.
Watanzania wengi wanaelewa katiba ni kitabu anachoshika rais akiapa.
Hawana ufahamu katiba inaathiri maisha yao pale pale waliposimama.
Na wala hawaelewi kuwa matatizo wanayoyakabili sehemu kubwa ni ubovu wa katiba.
Mkuu Mkandara, hakuna serikali 2. Huwezi kuwa na SMZ na JMT ambayo znz imo ukasema ni 2. Hapa ni pana kutatiza sana ima kwa kuogopa ukweli au kwa kutofahamu.Mchambuzi,
Dah kumbe ndio hivi mimi sikujua hili.kumbe Ukawa ni Chadema kwa bara sio umoja wa wajumbe, haya sasa mimi nayepingana na UKAWA pia nipo ni kundi la nani la ACT au sio? Mkuu ieleweke nachopinga mimi sio umoja wa UKAWA ila fikra za kuunda serikali 3 wakiacha mambo ya muungano kuwa 7 badala ya mambo yote yawe ya Muungano.
Kama hivi leo tuna mambo 22 ya Muungano na yale ya Bara yanaendeshwa chini ya muundo huu wa seriikali 2 tusiidai Tanganyika kwa miaka 50, Je inashindikana nini kuwa na yote ya Muungano kuziba kabisa midomo yahawa kina Jussa maana wao ndio wanataka kila siku mambo ya muungano tupunguze, nanyi mnaafikiana nao. Leo tuna saba, kesho yatakuwa matano, na kisha mawili na mwisho hakuna kitu hudhani kwamba hawa jamaa hawakuwa na mwisho hadi waone Muungano umekufa!.
Hili ndilo tatizo langu kubwa na UKAWA ktk mapendekezo ya rasimu ya Warioba. Tulichoomba sisi wananchi ni katiba mpya inayokwenda sambamba na transformation ya TAIFA letu Kiuchumi na kisiasa ili kukidhi mahitaji yetu, jambo ambalo lilitakiwa toka mwaka 1993 na sii swala la kero za Muungano wetu maana mamlaka ya utekelezaji shughuli za serikali ni i za serikali, kila jimbo, kila mkoa na kila wilaya wanayo haki ya kupewa mamlaka hayo ndani ya mfumo huu wa Kibepari..muhimu la lazima kwa serikali zote 2 chini ya muundo wowote na haikomei kwa serikali hiz bai huenda hadi kwa Magavana, Mayor na serikali za mitaa wote wanahitaji mamlaka kamili kwa shughuli zao na sii mlolongo wapaper work na ofisi, hii inaoleta Urasimu na ucheleweshaji wa maendeleo.
Mkuu wangu nikwambie nini uweze kuelewa... kwanza nini maana ya Tanganyika kuvaa koti la Muungano?.. maana muhimu ufahamu hili kwanza kabla hujarukia hoja ambazo hazifanani na madai. Acha hizi habari za kusikia wadhungu wanasema -Three different people can witness the same event and each comes up with a different account of how it occurred!.Mkuu Mkandara, hakuna serikali 2. Huwezi kuwa na SMZ na JMT ambayo znz imo. Hapa ni mhalai pana kutatiza sana ima kwa kuogopa ukweli au kwa kutofahamu.
Ukisema JMT tayari umeshaondoa serikali ya pili. Hakuna serikali ya pili ya JMT.
Serikali 2 ni ya Tanganyika na Zanzibar halafu kuna ya JMT
Mkandara, Warioba amesikiliza maoni ya watu. Moja ya malalamiko ya wznz ni Tanganyika kuvaa koti la muungano.
Yaani yalipongezwa mambo hadi 22 hakuna faida kwa Tanganyika, aliyefaidika ni mzanzibar.
Mznz kasema mambo yaliyoongezwa ni kinyemeala na wewe umemuunga mkono. Inashangaza leo unaposema eti mambo yote ni ya muungano. Ni ya muungano vipi wakati wznz unaowatetea hawataki iwe hivyo?
Hafu unasema kuna mambo yameongezwa kinyemela, back and forth, huwezi kuwa na mambo ya muungano halafu ukasema yameongezwa kinyemela.
Ni jambo la kusikitisha kuona Mtanganyika kama wewe upo tayari kuuza utaifa na rasilimali za nchi yako bila hoja za msingi. Huwezi kuwa na ka nchi kama znz kakapanga namna Tanganyika inavyojitawala.
Leo tunapeleka miswada ikatiwe sahihi na BLW la watu 50, wote wakiamini na akili zao zikifiri kwa bidii kabisa mabalozi ndio tatizo la nchi hii. Real! hawa ndio watu wakaupitia miswada yetu! hawa!
Mkuu Mkandara, wznz wanasema wanataka mamlaka kamili. Tulianza na mambo 11 yakafikia 22,wznz hawataki. Leo wewe unakuwaje mznz kuliko wznz wenyewe? hawataki, tunajaribu 7 kama hawataki njia nyeupee
Na mwisho waeleze watu, serikali 2 zinafanyaje kazi kuondoa malalamiko, kwanza kwa znz, na pili kuwajibisha znz iwe na jambo la maana katika maendeleo, kuchangia na kubadili mawazo ya mabalozi 3.
Tueleze nani anasimamia rasilimali za Tanganyika, na kwanini unadhani cha Mtanganyika ni cha wote cha mzanzibar ni chao peke yao. Haki hiyo inatolewa kwa msingi gani.
Hebu eleza umuhimu wa znz kwetu, maana wengine kwa kusikia wenzetu wanashida ya mabalozi 3, tunadhani kifikra tupo katika muungano na watu tofauti kabisa.
Point ya kwanza, ni kweli, lakini kumbuka kuwa Tanganyika ilitoa utaifa wake na kuukabidhi kwa Tanzania, kwa mujibu wa maneno yako mwenyewe.Mkuu Three different people can witness the same event and each comes up with a different account of how it occurred!.
Wanachosema ni kwamba
1. Kwa Kila project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika haihitaji ridhaa ya Wazanzibar japokuwa kwa kila project ya Zanzibar, Zanzibar inahitaji ridhaa ya Tanganyika ( mfano - OIC)
2. Kwa kila mpango wa project ya Tanganyika (mambo yasokuwa ya Muungano) Tanganyika imetumia jina la Tanzania kuvuta mikopo nje, kwa sababu Kimataifa nchi za Tangayika wala Zanzibar haziwezi kuvuta mikopo kwa sababu hazitambuliwi kama ni Taifa. nakuomba ufahamu tu ya kwamba lengo la TAIFA huru kuwa na kiti UN ni kutambuliwa kama TAIFA huru lenye serikali halali na hivyo kufungwa ktk sheria za Kimataifa katika maswala ya mawasiliano, trade, mikopo, na misaada ambayo mashirika ya Kimataifa yanapewa guarantee ya kuaminiwa.
Hivyo basi utakapo kuwa na serikali ya 3, hiyo ya Tanganyika bado nchi hii itahitaji kutumia jina la Tanzania ktk ushirika wake Kimataifa na mashirika ya nje. Na hivyo itaendelea kulivaa koti la Muungano kwa kutumia tena jina la Tanzania ktk mambo yasokuwa ya Muungano (yawe 7, 11 au 22). Hivyo muundo wa serikali 3 bado hautaondoa tatizo hilo bali Tanganyika itakuwa imelivua koti na kuliweka begani (kuondoa kero) ili upepo upite, lakini kama MAMBO YOTE YATAKUWA YA MUUNGANO tutalivua koti hilo -hakuna Utanganyika wala Uzanzibar kimataifa, hivyo kila jambo litahusu pande zote 2 (TANZANIA) na kupata ridhaa ya bunge la JMT.
Hii itasaidia kuondoa mamlaka kamili kwa viongozi wa serikali za Tanganyika (JMT) kuweka mikataba ya Tangayika chini ya meza, tena basi sio kwa Tanganyika ila kwa wao wenyewe kujilimbikiza utajiri kwa kutumia siri ya nchi. Miradi yote itajadiliwa na wizara kwa faida ya Tanzania, itapitishwa na bunge maana hakuna siri ya miradi ya uzalishaji, ushirika wa wabunge wa pande zote 2 (Utawla na Upinzani) watakuwa na nguvu ya kiitikadi kupinga ama kukubaiana na uwekezaji badala ya Uzanzibar na Ubara na mwisho wa siku ktk mapato ya mradi mzima kodi ya mapato (income tax) itawekwa ktk mafungu mawili, moja ya nchi (VAT) na nyingine ya Taifa ndio kusema kama ni asilimi 30, basi 20 ya Taifa na 10 ni ya nchi. Na ktk nchi, kila mkoa au jimbo litafaidika tena kwa asilimia toka ile asilimia 10. Haiwezekani gas itoke Mtwara waachwe watupu na visima vya maji, pasipo guarantee ya mapato ya kodi toka uwekezaji jimboni hapo.
Haya ni mapendekezo yangu ambayo hata nchi za magharibi wanatumia. kama wewe uanvyodai umewahi kufika Ontario, Canada basi bila shaka unaelewa ndani ya kodi ya HST (13%) kuna kodi 2 za PST (5%)ya jimbo na GST (8%) ya Taifa. Hivyo kila jimbo la Canada linapanga PST yake kuvutia uwekezaji sehemu hiyo kulingana na mahitaji yao lakini kodi ya GST imesimama pale pale kwa majimbo yote. Halafu kuna kodi za Mafuta ambazo kila jimbo linapanga kutokana na gharama za uagizaji, usafiri n.k hivyo bei ya mafuta inatofautiana kwa kila jimbo. yet kila Jimbo hadi taifa wanafaidika na uwekezezaji japo mafuta yanatoka Alberta! Na ndio maana Alberta sasa hivi ni jimbo tajiri kuliko majimbo yote Canada na hawana kinyongo ku share pato lake na majimbo mengine ya Canada kwani hata wao wanafaidika na rasirimali toka majimbo mengine ikiwa ni pamoja na nguvu za umeme wa nuklia toka sehemu nyinginezo.
Kwa hiyo Uwe na tanganyika anma laa maadam mambo yasokuw aya muungano yatakuwepo Tanganyika haitaweza kulivua koti kwa sababu Tanganyika sio TAIFA na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa, njia pekee ya kuondokana na adha hii ni kuyafanya mambo yote yawe ya Muungano japo Wazanzibar hawataki na Watanganyika wanataka kujitenga. hatuwezi kukubali kushindwa na hoja za watu wachache wenye nia mbaya na Muungano wetu, njia pekee ya kuwakomoa wote hawa wenye fikra za Ubinafsi na kugawana mbao ni kuyafanya mambo yote yawe ya nmuungano kisha zitungwe sheria mpya za kodi - Tax income act ambayo itawezesha kila jimbo hadi taifa kufaidika na mapato haya.
Najua bado hujanielewa na hutaki kunielewa....
Rasilimali zipi? ebu nambie wewe Mtanganyika unanufaika vipi na hesabu kubwa ya watu wasiolipa kodi? unanufaika vipi na ardhi kubwa inayoizwa kwa wageni? Unanufaika vipi na dhahabu za Geita na Bulyanhulu? hiyo gas ya Mtwara, Uranium ya Iringa na kadhalika! Je, Huyo Mzanzibar ananufaika vipi!.. Badala ya wewe kutazama katiba iliyopo ili ikuwezeshe wewe kufaiodika na rasilimali hizi unaitazama Zanzibar na kutaka ardhi kule ili iweje?.Mkuu Mkandara
Ninaposema Tanzania imevaa koti la Tanganyika nina maana rasilimali za Tanganyika zimegeuzwa kuwa za Tanzania.
Nina maana mzigo wa Tanzania ameubeba Mtanganyika kwa jina la Tanzania. Hilo lipo wazi kwa kile kigezo cha uchumi.
Kuhusu mikopo, waziri wa znz anasema 88% ya deni lao limedhamiwa na Tanzania iliyovaa koti la Tanganyika. In other words kila sh 100, sh 88 amedhamini Mtanganyika kwa jina la Tanzania.
Tuonyeshe mahali katika bajeti ya znz ya bilioni 710 panapoonyeshwa kuwa kuna fungu la kulipa hiyo 88 au 12%
Jibu ni hakuna na deni hilo atalimeza Mtanganyika kwa jina la Tanzania.
Kuhusu Utanganyika, hilo nalo nasema ili kutokuwa na malalamiko na kuwapa wznz nafasi nzuri ya kukopa bila kupitia Tanzania, tunataka S3. Hapo hakutakuwa na malalamiko kwa sababu znz watakwenda Paris na Washington kupata mikopo na misaada yao kwa uhuru. Tanganyika nao watakwenda huko kwa njia zao.
Na mwisho, nimeeleza kuwa kuna deni la ndani na la nje.
Unapoangalia mikopo na misaada, Mkandara unafumba macho kabisa kuangalia ni kiasi gani znz inatumia kwa deni la ndani.
Hebu tueleze kwa znz, bajeti ya ulinzi na usalama, mambo ya ndani, mambo ya nje, elimu ya juu, wizara za muungano, zn inatumia kiasi gani cha bajeti yake.
Pili, znz ikipata huo uwezo wa kukopa na misaada, je suala la Tanzania litahudumiwaje. Nina maana mikopo na misaada ya Tanzania itahudumia Tanzania, je ile ya znz itakuwa na mchango gani kwa Tanzania.
Tena hapa unanisaidia sana. Tulisema ili mzanzibar anufaike ni lazima tuwe na kila jambo la pamoja.Rasilimali zipi? ebu nambie wewe Mtanganyika unanufaika vipi na hesabu kubwa ya watu wasiolipa kodi? unanufaika vipi na ardhi kubwa inayoizwa kwa wageni? Unanufaika vipi na dhahabu za Geita na Bulyanhulu? hiyo gas ya Mtwara, Uranium ya Iringa na kadhalika! Je, Huyo Mzanzibar ananufaika vipi!.. Badala ya wewe kutazama katiba iliyopo ili ikuwezeshe wewe kufaiodika na rasilimali hizi unaitazama Zanzibar na kutaka ardhi kule ili iweje?.
Hakuna kitu Tanganyika, hapa tuna tanzania tu na serikali yake ya JMT ambayo inaendesha mambo ya Tanganyika. Hivyo Tanganyika inapolivaa koti la Muungano ni muhimu ufahamu kinachosemwa hapa kinahusu nini na sii kuvumbua yako..Ni katiba hii ya mwaka 1977 inayotuongoza sote hivyo unapokuja na maswala ya Utanganyika wakati haipo, basi kesho utakuja na maswala ya Usukuma na Ukurya kutuondoa hata sisi Wakerewe wa visiwani tusokuwa na maliasili na rasilimali kama zenu. Acheni hizi habari za kuvaa koti kwa kutazama una nini mfukoni bali tazama fursa zilizopo wewe kama Mtanganyika unakwamishwa vipi?
Kuna haja kubwa sana ya Kutoa elimu ya URAIA maanake naona watu wameanza kughiribiwa na hii Ukawa!
Mkuu nimeisikiliza video hiyo kwa umakini na sielewi unachodai wewe zaidi ya kwamba Mtoa hotuba anaamini ktk serikali 2. Na zaidi ya hapo kaonyesha wazi kwamba serikali hii inaendelea kufanya makosa yale yale ambayo hayawezi kuondoa mapungufu ya Katiba bali kuondokana na kero zilizopo.Mkandara
Video hiyo nimekuonyesha makusudi ili usitumie makabila kuwatisha Watanganyika.
Pili, wznz wenyewe wanasema kila jambo limekubaliwa. Asilimia 21, PAYE, Mikopo na kujitafutia misaada.
Kumbuka mikopo wanapata kwa dhamana ya Tanganyika yenye assets. Mikopo hiyo haionyeshwi italipwaje, tunachojua ni kumbebesha Mtanganyika mzigo.
Tatu, Wazanzibar watakapopata mikopo na misaada Wataitumia vipi katika muungano. Kama ni yao, kwanini hii inayokuja kwa Tanzania ikihudumia wao(Ulinzi na usalama na mambo chungu nzima) ibebwe na Mtanganyika peke yake?
Nne, kwavile Tanganyika imevaa koti, hebu tuanze kuangalia mambo kwa undani zaidi.
Mkandara, naomba unipe bajeti ya Zanzibar ya ulinzi na usalama, na mambo ya ndani ya mwaka 2014/2015 . Hivyo viwili tu.
Halafu tutaendelea