Uke kutoa harufu kali(Vaginal Odor): Chanzo, dalili na tiba zake

Uke kutoa harufu kali(Vaginal Odor): Chanzo, dalili na tiba zake

mwambie asiwe anatumia sabuni yoyote akiwa anaosha papuchi yake ,aoshe tu kwa maji safi na kitambaa kisafi,hlo tatizo litakoma na hutoliona tena
 
GENTAMYCINE

Mwonyeshe jinsi unavyompenda, unavyomjali mpaka ajue kuwa unampenda sana then muulize swali kama wewe una tatizo lolote linalomkwaza?? Akijibu huna na yeye atakuuliza but usimjibu moja kwa moja atajisikia vibaya mpongeze kwanza kwa mengine then mgusie as if si tatizo kubwa au kasoro!! Na umuhakikishie kuwa hilo swala la kunuka linakwisha
 
Last edited by a moderator:
Mkuu huko chini ulienda kuchungulia huko nin! mb@@ ndiyo yenye jukumu la kulalamika
 
Kama kweli anajua unampenda na anaona kwa vitendo halitakuwa tatizo jinsi ya kumwambia.....!
 
GENTAMYCINE,
kwa hadhi yako hasa kwa kupitia zile mada zako za idarani,hukutakiwa kabisa kuleta mada hii JF.ungekuja nayo kwa ID ya dharula au ungeipiga nyundo tu kwa kutafuta ushauri nje ya mtandao wa kijamii.ni ushauri tu mkuu.
clipart-sad-yellow-smiley-3d-512x512-fcb4.png
 
Si umesema ujawahi kumpata mtam kama huyo sasa usimwambie kama ananuka atakuwa sio mtamu tena papuchi yake ikiacha kunuka na utam wake utaishia hapo hapo
 
mimi kuna mmoja nilimwambiaga akanijibu mwanaume aliekuwaga nae hajawahi mwambia kitu kama hicho ina maana yeye alikuwa haiskii hiyo harufu, nikamjib alikuwa hakupendi ndiyo maana hajakwambia angekuwa anakupenda basi angekwambia na tatizo lingeisha. alinielewa na akazingatia usafi
 
Nitaanzaje Mkuu?

Ninacho maanisha ni kuwa kama anajua unampenda tena unamuonesha kwa vitendo hata ukitumia njia yeyote atachukulia una mwambia kwa kuwa wampenda....tatizo lako ni wasi wasi wako pengine unajua ni kiasi gani hakuamini na anaweza kuhisi umepata mwingine na atakuuliza kwanini siku zote hujamsaidia...!
 
mwambie hivii...beib leo vipi huku chini mbona hali si shwari??..... sifanye ndo umeisikia kwa siku hiyo na kuendelea then umshauri mwende hospitali
 
Mkuu fanya vitu vifuatavyo vitakusaidia kufikisha ujumbe:

1. Jaribu kumuliza Je anapenda kutumia pafyumu au mafuta au sabun huko kwa PAPUCHI ili kuongeza manukato (Hapo ujanja kichwan mwako ktk kuwasilisha hilo swali ili lionekane la kawaida sana ila linalohitaj majibu ya uhakika), unaweza jifanya kama unataka kumnunulia hivyo vitu n.k.

2. Aliwahi kusumbuliwa na fangasi wa sehem za siri huko nyuma au hata sana? jibu la hapo litakupa mwanga na urahisi wa kumshaur kumuona daktari bila kujisikia vibaya yeye binafsi.

Note: kama unampenda unaweza kumvaa moja kwa moja ila baada ya maongezi ya muda mrefu kumjenga kasaikolojia asichukulie kama umemchoka.
 
Kuna hii mada nimeitoa sehemu inaweza kukusaidia katika harakat zako za kumsaidia mwenza wako.

COPY AND PASTE


SABABU NA JINSI YA KUZUIA UKE KUTOA HARUFU MBAYA.

Tatizo la uke kutoa harufu mbaya ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi.

Zifuatazo ni sababu na jinsi ya kuzuia tatizo hilo.o

1.BACTERIA VAGNOSIS.
Hili ndio tatizo ma 1,linalosababisha uke kutoa harufu mbaya,Inawezekana ukawa msafi mpaka mwisho lakini ukisumbuliwa na tatizo hili basi lazima uke wako utatoa harufu mbaya.Kila uke una Bacteria ambao wapo naturally kwa ajili ya afya njema ya uke wako lakini kama ikitokea hawa bacteria wakazidi na kuwa wengi kupita kiasi ambacho uke wako unaweza kuhimili ndio hapo hiki kitendo kinaitwa
BACTERIA VAGINOSIS.
Sababu zinazosababisha Bacteria Vaginoais hazijulikani kwa usahihi lakini madaktari wanasema inaweza ikasababishwa na kitendo cha kufanya mapenzi bila kondom especially kama vitu vilivyoingia kwenye uke wako wakati wa kufanya mapenzi vilikuwa vichafu ( vitu kama vidole au mashine ya mwanaume au mara nyingine inatokea naturally bila sababu.



DALILI ZA BACTERIA VAGNOSIS.

*Uke kutoa majimaji mazito ( ute ute ) ama mepesi yenye rangi ya njano au brown yenye harufu mbaya.
*Maumivu kwenye maeneo ya kiuno au nyonga.
* Uke unaweza ukawa unawasha.


2.MAGONJWA YA ZINAA.
Kuna baadhi ya magonjwa ya zinaa yanayosababishwa na ufanyaji wa mapenzi bila kutumia kondom,kama kaswende na kisonono,ukiyapata huwa yanasababisha uke kutoa harufu mbaya kwa sababu dalili zake zinahusiana na kutokwa na maji yenye harufu mbaya.


3.UCHAFU.
Inawezekana pia tatizo la uke kutoa harufu mbaya linasababishwa na uchafu,labda unaoga mara moja tu kwa siku au siku nyingine hata hauogi.Au hauna mazoea ya kufua nguo zako za ndani na ikitokea siku umezifua basi hata hauzisugui zikawa safi.


4.YEAST INFECTION.
Hili pia ni tatizo,lipo kama la Bacteria Vagnosis tofauti yake ni kuwa kwenye Bacteria Vagnosis waliokuwa wamezidi ni Bacteria lakini huku wanaozidi ni Fungus Candida Albicana.
*Ni wanawake wachache huwa wanapata Bacteria Vagnosis lakini wanawake wengi lazima wapate Yeast Infection japo mara moja katika maisha yao.
*Mara nyingi Yeast Infection hutokea naturally au inaweza kusababishwa na aina ya vyakula au vinywaji unavyokula au kunywa especially kama vimejaa Yeast. ( vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe.n.k)


DALILI ZAKE.
*Uke kuwasha
*Maumivu kama uke unaungua pale unapokuwa unajisaidia haja ndogo.
*Uke kutoa majimaji mazito (ute ute) yenye rangi nyeupe kama jibini.


MAMBO YA KUFANYA ILI KUZUIA UKE USITOE HARUFU MBAYA.
1.OSHA UKE WAKO KWA MAJI SAFI KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA HAJA NDOGO.
Asilimia kubwa ya wanawake hawana mazoea na utaratibu huu.Ni utaratibu muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanamke,unapokuwa unajisaidia haja ndogo lazima utakuwa umechuchumaa,haja ndogo yako imapokuwa inatoka lazima kutakuwa na mabaki kidogo yatarukia na kubakia lips za nje au za ndani za uke wako.Hayo mabaki baada ya muda yatachanganyika na jasho ma kutengeneza harufu mbaya hivyo ni vizuri kuosha uke wako kwa maji safi kila unapomaliza kujisaidia haja ndogo.


2.UKIWA UNAOSHA UKE WAKO,TUMIA MTINDO WA KUPELEKA MKONO KUTOKA MBELE KURUDI NYUMA.
Kuna baadhi ya wanawake tayari wameshazoea kusafisha sehemu zao za siri kwa kupeleka mkono kutoka nyuma kuja mbele.Hui mtindo sio mzuri kiafya kwa kuwa huko nyuma kuna sehemu ya haja kubwa,kumejaa uchafu na bacteria wengi,sasa wakati unajisafisha unapopeleka mkono nyuma unazoa uchafu na ukauleta mkono mbele unaacha hao bacteria na uchafu kwenye uke wako.Na huo ndio mwanzo wa uke wako kutoa harufu mbaya na kupata infections za ajabu ajabu.
*ukitaka kuwa salama,haijalishi kuwa umemaliza kujisaidia haja kubwa,au ndogo au wakati unaoga,ukitaka kusafisha sehemu zako za siri,tumia mtindo wa kupeleka mkono mbele kurudi nyums ili usije kuwaleta bacteria na uchafu wa nyuma,mbele kwenye uke wako.


3.VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA.
Pamba ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana,na sehemu za siri za mwanamke inahitaji flow ya hewa inayopita,nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako zs siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote,nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.


4.USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA.
Kwa jinsi maumbile ya mwanamke yalivyo,umatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.Unapotoka nyumbani kuelekea kazini,chuo,kwenye biashara zakp n.k hakikisha unatoka na nguo ya ndani ya pili ambayo unatakiwa uiweke ndani ya mkoba au kipima joto chako.
Labda ulivaa nguo ya ndani asubuhi ulipokuwa unatoka nyumbani,ikifika ( saa 8 au 9 ) ingia bafuni au chooni,vua nguo yako ya ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima au ukassfisha sehemu zako za siri tu,Nguo
Ukimaliza hapo chukua nguo ya ndani safi uliyotoka nayo nyumbani uivae,hapo sasa unaweza kuendelea na shughuli zako kama kawaida huku uke wako ukiwa msafi bila harufu za ajabu ajabu.


5.PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI AU YEAST.
Unaweza kupunguza pia tatizo hili kwa kuacha au kupunguza kula vyakula vyote vyenye sukari au yeasy kwa wingi.Vyakula hivyo ni kama vile vinavyotengenezwa na hamira,pombe nk.ukizidisha vyakula au vinywaji hivi ina maana utakuwa unazidisha yeast mwilini na wakizidi kwenye uke utapata YEAST INFECTION,mwisho wake uke wako utaanza kutoa harufu mbaya.


6.BADILI PAD'S ZAKO MARA KWA MARA UWAPO KWENYE HEDHI.
Ili kuzuia uke wako usitoe harufu mbaya kipindi ambacho upo kwenye siku zako,inashauriwa kubadili pad mara kwa mara (kila baada ya masaa 4 au 8 ).kubadili pad's mara kwa mara kunasaidia ujisikie upo confortable,inazuia bacteria kujikisanya,inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata infection na mwisho inaondoa uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.


7.NYOA NYWELE ZAKO ZA SEHEMU ZA SIRI MARA KWA MARA.
Nywele zako za sehemu za siri zinapokuwa ndefu,unakuwa umetengeza maficho ya kila aina ya uchafu kuanzia jasho,majimaji yatakayokuwa yanakutoka ukeni ukipata hamu ya kupewa raha na utamu,mabaki ya haja ndogo nk.
*ili kujiepusha na yote hayo ni heri ukawa unazikata nywele zako za sehemu za siri mara kwa mara ili uke wako msafi muda wote.

COPY AND PASTE

Source: https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=1516662415229878&id=1401366480092806
 
Sidhani kama kuna mtu anaweza kukushauri namna nzuri ya kumweleza kwakuwa wewe ndio inamfahamu zaidi yetu sisi.labda tukushauri Dawa.MWAMBIE AOSHEE MAJI YALIOOSHEA MCHELE KWA MUDA WA WIKI MOJA MFULULIZO.
 
Sidhani kama kuna mtu anaweza kukushauri namna nzuri ya kumweleza kwakuwa wewe ndio inamfahamu zaidi yetu sisi.labda tukushauri Dawa.MWAMBIE AOSHEE MAJI YALIOOSHEA MCHELE KWA MUDA WA WIKI MOJA MFULULIZO.

Dah nilishawahi kushangaa sana hii kitu halafu nilikua sijui maana yake kumbi inaondoa harufu huko,

Niliwahi kukutana nayo sehemu moja mdada alikua anapenda kuoga maji yaliooshewa mchele au yale yanayopatikana ktk sufuria la ugali almarufu kama maji ya ukoko.
 
Dah nilishawahi kushangaa sana hii kitu halafu nilikua sijui maana yake kumbi inaondoa harufu huko,

Niliwahi kukutana nayo sehemu moja mdada alikua anapenda kuoga maji yaliooshewa mchele au yale yanayopatikana ktk sufuria la ugali almarufu kama maji ya ukoko.

Hyo ni nzuri wengi hutumia kuogea hasa maji ya ukoko hutoki harufu hata chembe kuanzia ya kikwapa hadi down stairs.
 
mwambie hivii...beib leo vipi huku chini mbona hali si shwari??..... sifanye ndo umeisikia kwa siku hiyo na kuendelea then umshauri mwende hospitali

hiyo kauli ungeambiwa wewe sipangechimbika
 
Hyo ni nzuri wengi hutumia kuogea hasa maji ya ukoko hutoki harufu hata chembe kuanzia ya kikwapa hadi down stairs.

ingekuwa ni hivyo basi maji ya mchele na ukoko yangekuwa yanauzwa dukani kama vipodozi vingine
 
Back
Top Bottom