Huu ni ukweli mchungu. Asilimia 90 wako kwenye ndoa ama.mahusiano kama picha tu.Kwenye foleni zao angalia tu ndani ya gari, kama si mmoja wao amelala basi anachati, au wameweka sura mbuzi, nuru ya uso haipo, uchovu mkubwa, kazini stressi, kurudi usiku wa manane, foleni kubwa, haridhishwi kitandani, mtu kwa siku analala masaa 2 tu, kula yenyewe wanakula fast food au junk foods, machipsi yai, wikend hakuna kupumzka, ni kwenda kujirusha kula mapombe na junk foods, matokeo kiriba tumbo na unene uliopindukia, matatizo ya afya mengi kama nguvu za kiume, presha sukari, hapo ndio mtu anaanza tena kubugia madawa kujaza sumu mwilini, hapo sijazungumzia pollution kama air and land polution za huko dar na noise pollution, ni mtu mmoja huyo anayapata haya yote halafu mnasema ni ujanja kwamba mji umechangamka kumbe watu ni nusu maiti zinazotembea.