Ina tegeemea na mtu mwenyew kama huyu LUCY wangu kwa kweli ni 100% wife material
1. Ana moyo wa kushirikiana (Support)
huwa ananipa sana moyo hasa wakati wa changamoto
Ananitia moyo katika malengo ya maisha na michongo yangu binafsi
2. Ni muaminifu sanaaa
• Amenifanya nimuamini kimapenzi, kifedha, kihisia, na kimaisha
• Mpaka sasa hajaniletea usaliti wa aina yoyote iwe ni uongo , au kuficha mambo muhimu hajawahi ni muwazi mno mm ndo namvuruga binti wa watu😖
3. Ana Mchango wa kiakili na kihisia
• Ni mtu anayeweza kunisaidia kufanya maamuzi mazuri ya pamoja kwa ustadi mkubwa sanaa na uelewa wa hali ya juu ambao mm sikuwah kuwaza
• Ana hisia za huruma na uwezo wa kuonyesha mapenzi kwa vitendo bila kujali lolote
4. Mchango wa kifedha 💯 (Hapa ndo hajawahi kuyumba)
• Yani MCHAGA huyu likija suala la pesa n mwepesi sana kutoa hana uchoyo kabisa mpaka nawazag kwani wachaga mnaowasemeea nyie ni wapi? Mbona huyu wangu yuko tofaut mwanzo nilidhani n penzi jipya ila mpka sasa yuko hivyo hivyo hajabadlka chochote tena ndo anazidi ( eeh mungu nipeeeeee😁)
5. Maadili na Adabu
•Hajawahi hata siku moja kunikosea adabu Hata kama mimi ndo nina makosa huwa ananyamaza mm nimalize kuonge halafu baadae ananirekebisha taratbu mpka nakaa kwenye reli🤣🤣 (i love this women)
• Ana maono yanayolingana na yangu kuhusu maisha familia,
• Ananisaidia sana kuweka msingi wa maisha bora ya baadae.
Itoshe kusema nimepata FULL PACKAGE Haya ndo mambo mwanamke anatakiwa kuchangia kwenye mahusiano
Huyu labda aniache mwenyewe ila hapa sibandukii ng’oo nilikotoka wangeniua wale wadada😁 🕊️LUCY🕊️