UKIACHWA NA SINGLE MOTHER UNAMPOTEZA NA HUYO MTOTO WAKE UNAYEMHUDUMIA. NI BIG LOSS.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Jamaa mmoja hapa ananisimulia kwa hasira kuhusu mahusiano yake yalivyo complicated, magumu sana. Mwanamke aliyekuwa anaishi naye ambaye alimkuta single mother wa mtoto mmoja wamegombana na huyo mwanamke amekazana waachane.
2. Sikutaka kujua sababu ya huyo single mother kutaka kumuacha mshikaji. Mimi nikamwambia mshikaji amuache tuu. Kama mwanamke hamtaki asimlazimishe.
3. Jamaa ananiambia, bado anampenda na zaidi amemlea mtoto wa yule mwanamke kwa miaka mitatu na alikuwa anamlipia ada ya shuleni. Anampenda kama binti yake.
4. Nikamwambia lakini sio binti yako. Ulifanya hivyo kwa hiyari yako na hakuna popote ulilazimishwa. Jamaa anahasira.
5. Ninachotaka kusema;
Haukatazwi kuoa au kuwa na single mother. Single mother ni mwanamke kama walivyo wanawake wengine.
Ila jambo la muhimu lazima uwafahamu kinagaubaga, ujue changamoto zao, uangalie matokeo ya kuwa na single mother na mwisho wa stori ikitokea mmeachana nani atakuwa Loser's
6. Single mother ukiachana naye ujue hata mtoto unayemlea umeacchana naye.
Alafu wanawake mbona wakilea watoto wa single father wao wakiachwa hawalalamiki lakini wanaume wanalalamika?
7. Sababu kubwa ni kuwa, Wanawake kitu kama sio chao hasa kuhusu watoto wanakubali ukweli kuwa mtoto ambaye hajamzaa yeye huyo sio mtoto wake. Atamchukulia kama mtoto wake lakini hawezi kumweka sawa kama mtoto aliyemzaa.
8. Hii ni kusema, unapomuoa au kuamua kuishi na single mother ukatekeleza wajibu usiowako wa kumhudumia mtoto wake, hiyo umefanya kama sadaka, kwa hiyari yako. Hakuna sehemu utakuwa na haki juu ya huyo mtoto siku wakitaka kukutenganisha naye.
9. Baba wa kambo ni Baba wa kambo. Huna mamlaka kimwili na kiroho juu ya mtoto asiyewako.
Huwezi kumbariki wala huwezi kumlaani.
10. Ikitokea unagombana na Mkeo, Mtoto huyo anauwezo wa kuingilia na kukubonda haswa na hakuna cha laana wala hawezi jisikia vibaya kukubonda.
Kwa sababu kwa huyo mtoto wewe ni stranger tuu. Mtu wa kupita katika maisha yake.
Kuwa na Mamaake haimaanishi wewe sio Stranger.
Jumatatu njema
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam