Ila kwenye hilo suala la nchi, inaonekana ama una uelewa mdogo sana, au huelewi chochote kabisa. Kingdom of Israel imekuwepo hata kabla hata ya ujio wa Yesu Kristo. Impaka mwaka 900BC Israel kingdom ilikuwa moja ikishikilia eneo kubwa la Mashariki ya kati ambalo leo hii hilo eneo ni hilo linaloitwa Israel, Westbank, Gaza, baadhi ya maeneo ya Egypt, Jordan, Lebanon.
Mwaka 500BC, baada ya kifo cha King Solomon, kingdom ya Israel iligawanyika na kuwa Northetn Israel Kingdom na South Judah kingdom. Hizo kingdoms ziliwahi mara nyingi kuvamiwa na kingdoms zinazowazunguka, hasa ile ya Babylone, na mara kadhaa walishindwa vita, na maeneo yao kuchukuliwa, na wao wenyewe kuchukuliwa mateka. Kusema hakujawahi kuwa na nchi ya Israel kabla ya 1948, huo ni ujinga, kutokuelewa historia ya Dunia. Katika historia ya kale, hakuna nchi iliyowahi kuitwa Palestine. Jina la Palestine liliasisiwa na watawala wa Kirumi, wakati wanaitawala Dunia nzima. Wayahudi wengi waliondoka kwenye nchi ya mababu zao, wakati wa wa Ottoman Empire., na wachache waliosalia waliondoka tena wakati wa utawala wa Muingereza. Mpaka mwaka 1948, kulikuwa na wayahudi kama 10,000 tu kwenye hiyo ardhi ya babu zao, wengi wakiwa wamekimbilia kwenye mataifa mengine, na maeneo yao ya kale, sehemu kubwa yakiwa yamechukuliwa na waarabu. Hakujawahi kuwa na kabila la wapalestina, bali ni waarabu na wayahudi. Na kabila la wayahudi lilianza baada ya kugawanyika Israel Kingdom, wale wa Judah kingdom, wakajiita Judahs. Lakini kabla yake wote walijulikana kama Waisrael, yaani wana wa Israel (Yakobo), na kabla yake waliitwa Waebrania, yaani wana wa Ibrahim.