Nabaki palepale pa mwanzo, sitetereki hata kidogo. Haiti ni jambo dogo sana. Wakimbizi wengi wakati huu hawatoki Haiti kupitia Mexico.
Nakufahamu wewe ni mtu mwelewa mzuri wa maswala kama haya ya Kenya na Marekani na wengineo. Nitakuacha kwa hili, kwa sababu sijui kwa nini umeamua kuliweka mbele huku makubwa zaidi yakiwa wazi.
Marekani anatafuta mshirika wa kimkakati katika eneo hili. Kenya kalelewa kwa muda mrefu, wakati umefika sasa wa kumweka mahala sahihi kihadhi kimashirikiano. Dunia imebadilika sana kwa ujio wa wababe wapya.
Tunaweza kutumia muda mwingi kuongelea hili lakini ileweke tena kuwa swala la Haiti ndiyo limesababisha uratibu wa safari hii kwa haraka haraa hivyo. Elewa kuwa viongozi wanpokutana, hawafanyi hivyo kwa lengo moja tu, watafanya mambo mengi ila la Haiti ndilo fukuto kubwa lililoharakisha mkutano huo. Labda nitaje mambo matatu ambayo ndiyo yanayoonekana sana kwa nje lakini siyo yaliyosababisha safari hii iratibiwe na kupangwa haraka haraka hivyo.
(a) Kila mtu anelewa kuwa Marekan inapenda sana kuwa na infulence sana kwenye geopolitics na na natural resouyrcxes za Africa. Hilo siyo jambo geni kwani wamekuwa wanalifanyia kazi kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Kwa hiyo Rutto anapokutana na Biden, jambo hilo halikosi kwenye agenda yao.
(b) Matukio kadha yaliyotokea huko Afrika ya Magharibi yalisababisha nchi hizo kuwafukuza askari wa West na kukaribisha askari wa Urusi. Marekani imekuwa na tentacles zake sehemu mbalimbali za Afrika hasa kwenye mazingira ya ughaidi. Hali ya usalama Somalia na kwenye Ghuba ya Aden kwenye Houthis kunaifanya Marekani iwe na Interest sana na eneo la Kenya kwa matumizi ya kijeshi. Kwa hiyo wakati Rutto atakapokutana na Biden, swala la Kenya kushirikiana na USA kijeshi kwa ajili ya usalama wa eno hilo halitakosa kwenye agenda yao.
(c) China imekuwa na influence kubwa sana kwenye bara la Afrika, na Kenya ni mojawapo ya nchi ambazo zimeelemewa sana na China hasa kwa madeni. Wakati Biden alipoawakutranisha viongozi wa Afrika kwenye ile USA-Africa Summit kujaribu kuwashahwishi wapunguze utegemezi wa China, wengi wao walilalamika kuwa hawakuheshimiwa na Marekani. Baada ya hapo, Marekani ikaanza utaratibu mwingine wa kuzifikia nchi za Afrika kwa lengo hilo hilo la kuzishawishi kupunguza utegemezi wa China. Kamala Harris alitembelea nchi kadhaa za Afrika na kumekuwa na viongozi kadhaa wa Marekani wakitembelea Afrika kwa lengo la kukutana one-on one na viongozi Afrika kujadiliana jambo hilo. Kwa hiyo mkutano baina ya Biden na Rutto hautakosa kujadili swala la utegemezi wa China.
Baada ya hayo matato ambayo ni traditional practices kabisa kwenye foreign policies za Marekani, kuna hili hapa ambalo wengi hawalioni na ndilo lenyewe lilimvuta Rutto.
(d) Wakati hali ya Haiti ikizidi kuspiral out of control, Marekani ilitegemea sana polisi wa UN wakiongozwa na Kenya. Hata hivyo, ,mwezi February Mahakama kuu ya kenya ilizuia Polisi wa kenya kupelekwa Haiti bila kuwapo reciprocity, na hali ya Haiti ikazidi kuwa mbaya sana ikisababisha wakimbizi wengi Marekani. Lengo la ziara hii ni kwa Marekani kutoa hiyo reciprocity inayotakiwa na Mahakama kuu ya Kenya ili Polis wa Kenya waingie kutuliza amani haiti bila Marekani kuhusika moja kwa moja. Hili la wakimbizi, ujue kuwa siyo idadi wa wakimbizi wa haiti wanaoisumbua Marekani, bali ni ile ripple effect ya wakimbizi wanaotoka Haiti kupitia Central America. Kwa wakimbizi kumi watakaovuka bahari hadi central America huvuta wakimbizi wengine kutoka central Amefrica na kuwa na Caravan kubwa.
Sasa hili la (d) linaonekana dogo sana kwenye geopolitical policies za Marekani kwa Afrika, lakini kwa bahati mbaya ndilo kubwa lililosababisha ziara hii kuratibiwa haraka haraka hivyo. Biden angependa huu mgogoro wa haiti uishea hata kabla ya September. Hili la wakimbizi, ujue kuwa siyo idadi wa wakimbizi wa Haiti wanaoisumbua Marekani, bali ni ile ripple effect ya wakimbizi wanaotoka Haiti kupitia Central America. Kwa wakimbizi kumi watakaovuka bahari kutoka Haiti hadi central America huvuta wakimbizi wengine wengi kutoka central Amefrica na kuwa na Caravan kubwa kuelekea Marekani.