Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Rais samia kwanini pamoja na ziara zote huko hapewi kipaumbele kama Ruto?

Ukiangalia jinsi Ruto alivyopokelewa kwa heshima marekani utashangaa

Ruto kapokelewa kwa heshima sana, vyombo vyote vya kimataifa vimempa airtime na headline yeye na Biden

Nashangaa rais Samia yeye hapati kabisa international coverage kabisa, sio alijazeera,sio cnn, sio bbc tutamuona akiwa kwenye ziara zake

Ziara ya Ruto ni funzo kubwa kwa machawa. Yaani sijui ni kwasababu maziara yetu hayana tija ndo maana hata hawashughuliki?...Yaani wetu ni kama wamempuuza hivi.
Marekani wametega simu za viongozi wote wakuu wanawasikiliza wanachoongea marais wote na mambo yao so wanajua which is which!
 
Sababu za kuheshimika Kwa ruto nchini marekani ni zifuatazo 1.william ruto ni rais aliyechaguliwa na wananchi lakini yule mwingine alilithishwa urithi na babu yake.
2.william ruto ana PhD kutoka chuo mahili tofauti na yule ana PhD ucharwa ya kukusanya mafaili.
3 Rais wa Kenya hakuuza ardhi za wamasai na hajawafukuza kwenye ardh Yao ya asili.
 
Ndiyo sababu kubwa.

Mgogoro wa Haiti unaongeza mzigo kwenye wimbi la wakimbizi Marekani, jambo ambalo siyo zuri kipindi hiki cha uchaguzi. Mambo mengine yote ya kidplomasia baina ya USA na Kenya yangeweza kusubiri lakini hili la Haiti hailiwezi kusubiri ndiyo maana safari imepangwa fasta fasta.
Nabaki palepale pa mwanzo, sitetereki hata kidogo. Haiti ni jambo dogo sana. Wakimbizi wengi wakati huu hawatoki Haiti kupitia Mexico.

Nakufahamu wewe ni mtu mwelewa mzuri wa maswala kama haya ya Kenya na Marekani na wengineo. Nitakuacha kwa hili, kwa sababu sijui kwa nini umeamua kuliweka mbele huku makubwa zaidi yakiwa wazi.
Marekani anatafuta mshirika wa kimkakati katika eneo hili. Kenya kalelewa kwa muda mrefu, wakati umefika sasa wa kumweka mahala sahihi kihadhi kimashirikiano. Dunia imebadilika sana kwa ujio wa wababe wapya.
 
Alikuja hapa Clinton kwenye suala la mahakama ya Rwanda (ICTR) Hadi barabara ikapigwa deki, au ulikuwa hujazaliwa Nini?
Kwa hiyo hoja yako ni nini hasa?

Kasome kwanza maana ya state visit halafu ndio tuje tuongee naona uelewa wako ni mdogo sana
 
Raisi mwingine wa Tz ambaye alikuwa anatema yai ni mwanafunzi wake Nyerere wa pale Pugu, Benjamin W. Mkapa
Mkuu,
Kwa sisi wa st. Kayumba inaitaji jitihada maalum
Shule ambazo kiingereza kime Be ""ABOLISHED"" Kama lugha ya kufundishia mwalimu mwenyewe wa ENGLISH Tia maji Tia maji.
Unakuta walimu wanafundisha kwa CODE MIXING
""Maarifa mengi yamefichwa kwenye lugha ya kiingereza"""

hakuna namna tutakwepa kuijua na kui Master hii LUGHA
 
Sio kweli.

Utofauti ni kwamba Kenya ni mshirika muhimu wa marekani pwani ya Afrika mashariki kama ambavyo nyie ni washirika wa China pwani ya Afrika mashariki.

Kama unafikiri marekani hana muda na nchi za kijamaa basi huzifahamu siasa za kimataifa hata kwa uchache.
kasomeni historia ya Tom Mboya ndiyo mutajua uhusiano wa US na Kenya
 
Dogo hiyo ni state visit.

Kenya wala siyo ya kwanza kuwa na hiyo status ya major non-NATO ally hapa Africa

Egypt, Morocco na Tunisia pia zina status hiyo. Na zinagusika vizuri tu
"Dogo..."?
naona kwa akili hiyo tu hata hayo uliyo andika huko chini wewe ni kama chizi tu! Huna unalojuwa.

Hata kusoma huwezi, au kuelewa ni shida! Nimeandika Afrika?

Hao waarabu uliowataja hawafikii "strategic partnership." Hao wanatupiwa tu vi-dollar vya hapa na pale kila mwaka, wanaridhika.
 
Hata kinongo bongo nikikualika nitaandaa mapochopocho ya kutosha. Ukijileta tu mwenyewe utakutana na maji kwenye jagi mezani.
 
Mkuu,
Kwa sisi wa st. Kayumba inaitaji jitihada maalum
Shule ambazo kiingereza kime Be ""ABOLISHED"" Kama lugha ya kufundishia mwalimu mwenyewe wa ENGLISH Tia maji Tia maji.
Unakuta walimu wanafundisha kwa CODE MIXING
""Maarifa mengi yamefichwa kwenye lugha ya kiingereza"""

hakuna namna tutakwepa kuijua na kui Master hii LUGHA
Umesema vyema

Ila Nyerere wa kulaumiwa sana aliamua kuchagua Kiswahili kama lugha ya kufundishia

Wabongo tunafeli sana kutoboa kimataifa kwa sababu ya Kiingereza na hili limeonekana kwenye kiwanda cha muziki na filamu pia
 
"Dogo..."?
naona kwa akili hiyo tu hata hayo uliyo andika huko chini wewe ni kama chizi tu! Huna unalojuwa.

Hata kusoma huwezi, au kuelewa ni shida! Nimeandika Afrika?

Hao waarabu uliowataja hawafikii "strategic partnership." Hao wanatupiwa tu vi-dollar vya hapa na pale kila mwaka, wanaridhika.
Point ni ileile zote ni major non-NATO allies nothing special on Kenya
 
Kwanza nilidhani wewe ni mKenya, kumbe siyo. Ni mTanzania tu asiyejuwa siasa za leo za hawa wakubwa.
Kenya ni 'puppet' state toka zamani. Kibaki kaipoza kidogo kwa kuangalia Mashariki, wakubwa wenye kinyago chao wakastuka, sasa wanakichonga upya.
Unampa ujiko mwingi sana huyo Ruto asio kuwa nao, ni kwa vile tu humjui, ndiyo maana unapapatika kama ulivyoonyesha hapo kwenye andiko lako.
Sikiliza: ukisha andika title ya Dr. mbele ya jina la mhusika; hakuna sababu tena ya kuweka hiyo Ph.D. mbele ya jina lake. Hili tu linaonyesha upungufu kwako, ndiyo maana umejilaza kabisa mbele ya Ruto atembee juu ya mgongo wako.
unasumbuliwa na inferiority mind set
 
Nabaki palepale pa mwanzo, sitetereki hata kidogo. Haiti ni jambo dogo sana. Wakimbizi wengi wakati huu hawatoki Haiti kupitia Mexico.

Nakufahamu wewe ni mtu mwelewa mzuri wa maswala kama haya ya Kenya na Marekani na wengineo. Nitakuacha kwa hili, kwa sababu sijui kwa nini umeamua kuliweka mbele huku makubwa zaidi yakiwa wazi.
Marekani anatafuta mshirika wa kimkakati katika eneo hili. Kenya kalelewa kwa muda mrefu, wakati umefika sasa wa kumweka mahala sahihi kihadhi kimashirikiano. Dunia imebadilika sana kwa ujio wa wababe wapya.
Tunaweza kutumia muda mwingi kuongelea hili lakini ileweke tena kuwa swala la Haiti ndiyo limesababisha uratibu wa safari hii kwa haraka haraa hivyo. Elewa kuwa viongozi wanpokutana, hawafanyi hivyo kwa lengo moja tu, watafanya mambo mengi ila la Haiti ndilo fukuto kubwa lililoharakisha mkutano huo. Labda nitaje mambo matatu ambayo ndiyo yanayoonekana sana kwa nje lakini siyo yaliyosababisha safari hii iratibiwe na kupangwa haraka haraka hivyo.

(a) Kila mtu anelewa kuwa Marekan inapenda sana kuwa na infulence sana kwenye geopolitics na na natural resouyrcxes za Africa. Hilo siyo jambo geni kwani wamekuwa wanalifanyia kazi kwa miaka yote tangu tupate uhuru. Kwa hiyo Rutto anapokutana na Biden, jambo hilo halikosi kwenye agenda yao.

(b) Matukio kadha yaliyotokea huko Afrika ya Magharibi yalisababisha nchi hizo kuwafukuza askari wa West na kukaribisha askari wa Urusi. Marekani imekuwa na tentacles zake sehemu mbalimbali za Afrika hasa kwenye mazingira ya ughaidi. Hali ya usalama Somalia na kwenye Ghuba ya Aden kwenye Houthis kunaifanya Marekani iwe na Interest sana na eneo la Kenya kwa matumizi ya kijeshi. Kwa hiyo wakati Rutto atakapokutana na Biden, swala la Kenya kushirikiana na USA kijeshi kwa ajili ya usalama wa eno hilo halitakosa kwenye agenda yao.

(c) China imekuwa na influence kubwa sana kwenye bara la Afrika, na Kenya ni mojawapo ya nchi ambazo zimeelemewa sana na China hasa kwa madeni. Wakati Biden alipoawakutranisha viongozi wa Afrika kwenye ile USA-Africa Summit kujaribu kuwashahwishi wapunguze utegemezi wa China, wengi wao walilalamika kuwa hawakuheshimiwa na Marekani. Baada ya hapo, Marekani ikaanza utaratibu mwingine wa kuzifikia nchi za Afrika kwa lengo hilo hilo la kuzishawishi kupunguza utegemezi wa China. Kamala Harris alitembelea nchi kadhaa za Afrika na kumekuwa na viongozi kadhaa wa Marekani wakitembelea Afrika kwa lengo la kukutana one-on one na viongozi Afrika kujadiliana jambo hilo. Kwa hiyo mkutano baina ya Biden na Rutto hautakosa kujadili swala la utegemezi wa China.

Baada ya hayo matato ambayo ni traditional practices kabisa kwenye foreign policies za Marekani, kuna hili hapa ambalo wengi hawalioni na ndilo lenyewe lilimvuta Rutto.

(d) Wakati hali ya Haiti ikizidi kuspiral out of control, Marekani ilitegemea sana polisi wa UN wakiongozwa na Kenya. Hata hivyo, ,mwezi February Mahakama kuu ya kenya ilizuia Polisi wa kenya kupelekwa Haiti bila kuwapo reciprocity, na hali ya Haiti ikazidi kuwa mbaya sana ikisababisha wakimbizi wengi Marekani. Lengo la ziara hii ni kwa Marekani kutoa hiyo reciprocity inayotakiwa na Mahakama kuu ya Kenya ili Polis wa Kenya waingie kutuliza amani haiti bila Marekani kuhusika moja kwa moja. Hili la wakimbizi, ujue kuwa siyo idadi wa wakimbizi wa haiti wanaoisumbua Marekani, bali ni ile ripple effect ya wakimbizi wanaotoka Haiti kupitia Central America. Kwa wakimbizi kumi watakaovuka bahari hadi central America huvuta wakimbizi wengine kutoka central Amefrica na kuwa na Caravan kubwa.

Sasa hili la (d) linaonekana dogo sana kwenye geopolitical policies za Marekani kwa Afrika, lakini kwa bahati mbaya ndilo kubwa lililosababisha ziara hii kuratibiwa haraka haraka hivyo. Biden angependa huu mgogoro wa haiti uishea hata kabla ya September. Hili la wakimbizi, ujue kuwa siyo idadi wa wakimbizi wa Haiti wanaoisumbua Marekani, bali ni ile ripple effect ya wakimbizi wanaotoka Haiti kupitia Central America. Kwa wakimbizi kumi watakaovuka bahari kutoka Haiti hadi central America huvuta wakimbizi wengine wengi kutoka central Amefrica na kuwa na Caravan kubwa kuelekea Marekani.
 
Rais samia kwanini pamoja na ziara zote huko hapewi kipaumbele kama Ruto?

Ukiangalia jinsi Ruto alivyopokelewa kwa heshima marekani utashangaa

Ruto kapokelewa kwa heshima sana, vyombo vyote vya kimataifa vimempa airtime na headline yeye na Biden

Nashangaa rais Samia yeye hapati kabisa international coverage kabisa, sio alijazeera,sio cnn, sio bbc tutamuona akiwa kwenye ziara zake

Ziara ya Ruto ni funzo kubwa kwa machawa. Yaani sijui ni kwasababu maziara yetu hayana tija ndo maana hata hawashughuliki?...Yaani wetu ni kama wamempuuza hivi.
Kuna ziara tofauti, kuna state visit, official visit, an official working visit, a working visit, a guest-of-government visit, a private visit.

Hii aliyoifanya Ruto ni state visit (by invitation of the president only).

Hii state visit ndiyo aliyoifanya Ruto. Haipatikani kirahisi. Ndiyo ya kwanza kufanywa na rais wa Kiafrika Marekani tangu mwaka 2008.

Kuna rais wa Gabon, Omar Bongo, alishawahi kuhonga dola milioni nane za Kimarekani apate mualiko kama huu kwa rais George W. Bush.

Wakenya wamejipanga, wame lobby muda nrefu.

Hii aliyofanya Ruto ni state visit.

Rais pekee wa Tanzania aliyefanya state visit Marekani ni Nyerere, miaka ya 1960s wakati rais wa Marekani akiwa John F. Kennedy.
 
unasumbuliwa na inferiority mind set
Umeiona wapi? Ukiwa nayo wewe usidhani wengine nao ni kama wewe.

Kwanza "inferiority mind set" ndio kitu gani? Unadhani ukitupia vineno vya lugha hiyo utaonekana wewe wa maana kuliko ulivyo kiuhallisia? Bwege tu!
 
Ndiyo sababu kubwa.

Mgogoro wa Haiti unaongeza mzigo kwenye wimbi la wakimbizi Marekani, jambo ambalo siyo zuri kipindi hiki cha uchaguzi. Mambo mengine yote ya kidplomasia baina ya USA na Kenya yangeweza kusubiri lakini hili la Haiti hailiwezi kusubiri ndiyo maana safari imepangwa fasta fasta.
Kwaiyo impangwa safari ili kuwapeleka vijana wa kikenya wakafie Haiti?
 
Back
Top Bottom