Katika mambo yote uliyoandika hoja ya msingi ni moja tu kwa nini Tanzania hatutoboi kimataifa?
Na si lazima taifa liwe na uhusiano wa karibu na Marekani au wanachama wa NATO ili liwe na uchumi mzuri.
Tanzania ni taifa lisilofungamana na upande wowote linaweza kuwa na ushirika na taifa lolote duniani iwe ni China au Marekani
Inawezekana hiyo point ya kwa nini Tanzania haitoboi ndiyo ya msingi, lakini hizo point zote zina umuhimu.
Mfano, huwezi kuongelea Ruto kupata state visit Marekani bila kuongelea business culture ya Kenya iliyomtengeneza Ruto, the Hustler in Chief. Inayoweka watu wa kumu inform Ruto nini cha kufanya, .
Huwezi kuongelea business culture ya Kenya bila colonial influence ya Waingereza na siasa zilizofuatia uhuru za Kenya ambazo hazijapitia distractions za Ujamaa.
Angalia mashirika makubwa ya kimataifa yaliyo na ofisi Nairobi, halafu angalia mashirika ya hivyo yaliyo na Ofisi Dar/Dodoma. Utaona Wakenya wametuzidi sana hapo.
Tanzania tumeshindwa hata kumu accommodate Benjamin Fernandez, wa NALA, aliyepata ahadi mpaka za rais Samia kusaidiwa, akaishia kuzinguliwa na kwenda kufungua ofisi Nairobi.
Kutofungamana na upande wowote kwenyewe tunakufanya kisiasa bila kuzingatia uchumi.
Kenya rais wao Ruto anaongoza kampeni ya kimataifa ya nchi za Afrika kujinasua kutoka kwenye US dollar dependency, ukimuangalia kwa juujuu unaweza kuona anapinga American hegemony. Lakini hapo hapo Ruto ndiye amekuwa rais wa kwanza wa Africa kupata State Visit US tangu 2008, anaingia kwenye alliance na US mpaka amepewa hadhi ya first sub-Saharan Africa non-NATO ally wa US.
Kajua kuuma na kupuliza anapata faida kwa kuibana US na kwa kuungana kupiga deal na US. Ruto mwenyewe kasema yeye si anti US, anawapigania Wakenya tu.
Tanzania Rais Samia kaonekana mwanamke, watu wakampa deal aongoze mazungumzo ya Africa kupewa hela za climate change (carbon credit and climate justice), wakifikiri huyu mwanamke anaweza kuchukua attention ya dunia. Samia kaenda Misri hajajiandaa kabisa, yani kashindwa kusimamia hiyo hoja si tu kimataifa, karudi Tanzania mpaka kwenye press conference hoja hajaipa kipaumbele. Sasa sijui ndiyo wamepiga deal na Rostam wakaona waifiche isijulikane sana?
Yani Wazambia ambao hawakupewa pande la kuongoza hii ajenda wamejipanga vizuri, wamechukua mabilioni ya US dollar, sisi tuliopeea kuongoza ajenda hatujapata kitu.
Kifupi wanasiasa wa Tanzania ni washamba, hawaijui dunia, hawajui lobbying, hawajui wanataka nini, hawajui siasa za kimataifa, wamezoea kukimbizana na Waswahili wetu japo ndani tukija kwenye geopolitics wanapwaya sana.