Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Ndiyo maana Wamarekani wanamuweka karibu Ruto kwa state visit, Tanzania tunaonekana hatuna uzito.
Acha akili za kitumwa. Mataifa mangapi hayajapewa state visit na Marekani.

Yamepungukiwa nini kiuchumi na mangapi yameizidi Kenya

Kumbe kwako taifa kupewa state visit na Marekani ni sifa?
 
Hata kwenye diplomasia za kiuchumi Tz ni kama Kenya tu
Kenya imepata state visit ya kwanza US kwa nchi ya Africa tangu 2008. Imepata status ya first sub saharan non-NATO ally wa US.

Tanzania haijapata state visit kama hii tangu Nyerere alivyomtembelea Kennedy miaka ya 1960s.

Sasa hapo kwenye mahusiano na nchi kubwq kama US unatufananishaje?
 
Acha akili za kitumwa. Mataifa mangapi hayajapewa state visit na Marekani.

Yamepungukiwa nini kiuchumi na mangapi yameizidi Kenya

Kumbe kwako taifa kupewa state visit na Marekani ni sifa?
Hata tukiangalia namba tu, Kenya kaizidi Tanzania kwa GDP licha ya Tanzania kuwa nchi kubwa, ina rasilimali zaidi na ina watu zaidi.

Kwa mwaka 2022 Kenya GDP yao ni USD 113 billion.

Tanzania ni USD 75 billion.

Tanzania GDP yetu ni 66% ya Kenya.

Bado utasema Wakenya hawajatuzidi kiuchumi?
 
Hili linahusinaje na state visit?
 
SA, Nigeria hazina major non-NATO ally status zimepungukiwa nini?
Kwa nini unashindwa kuangalia dynamics za dunia inayokuja na fursa zinazotokana na ushirikiano huu unaishia kuangalia leo?

Nigeria ilikiwa na uchumi mkubwa kabisa Africa, leo South Africa imeipita, huelewi vipi kwamba mbabe wa leo kesho anaweza kupitwa kutokana na watu walio chini yake leo wanavyojipanga leo?
 
SA na Nigeria hawakuhitaji major non-NATO ally status ili kuwa na uchumi mkubwa barani Africa
 
Rais samia kwanini pamoja na ziara zote huko hapewi kipaumbele kama Ruto?

Ukiangalia jinsi Ruto alivyopokelewa kwa heshima marekani utashangaa

Ruto kapokelewa kwa heshima sana, vyombo vyote vya kimataifa vimempa airtime na headline yeye na Biden

Nashangaa rais Samia yeye hapati kabisa international coverage kabisa, sio alijazeera,sio cnn, sio bbc tutamuona akiwa kwenye ziara zake

Ziara ya Ruto ni funzo kubwa kwa machawa. Yaani sijui ni kwasababu maziara yetu hayana tija ndo maana hata hawashughuliki?...Yaani wetu ni kama wamempuuza hivi.
Ukiangalia Kenya Ione Marekani Africa.
Angalia anavyopromote ushoga waziwazi
Pita Facebook Kenya imejikita kupromote
Mapenzi ya jinsia moja
Kwa nini America isimtunuku heshima?
Kenya ni Balozi mzuri wa Marekani Kwa uchafu wowote Marekani wanataka ukubalike Africa.
Muambieni Shangazi akajipendekeze na Yeye Tumpe majukumu
 
Mataifa yaliyopata state visit Marekani yamefaidika na nini?
Rito anajipanga kupiga USD 300 million kwenye deal moja tu kutokana na state visit hii.

Hiyo deal moja tu.

View: https://youtu.be/pmKK6dKih3w?si=cTFlC-fz8Esex7NF
 
Sijazidogosha ila ndio point yangu ilipo. Marekani anahofia kupoteza ushawishi barani Africa

Hiyo state visit ni kutaka kuwashawishi viongozi wengine wa Africa
Sawa.

Sasa imekuwaje Tanzania nchi ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa sana Africa miaka ya Nyerere siku hizi imepoteza ushawishi huo na Kenya ndiyo inachujua ushawishi huo?

Mbona inakuwa kama huelewi hoja ya uzi?
 
Rais samia kwanini pamoja na ziara zote huko hapewi kipaumbele kama Ruto?

Ukiangalia jinsi Ruto alivyopokelewa kwa heshima marekani utashangaa

Ruto kapokelewa kwa heshima sana, vyombo vyote vya kimataifa vimempa airtime na headline yeye na Biden

Nashangaa rais Samia yeye hapati kabisa international coverage kabisa, sio alijazeera,sio cnn, sio bbc tutamuona akiwa kwenye ziara zake

Ziara ya Ruto ni funzo kubwa kwa machawa. Yaani sijui ni kwasababu maziara yetu hayana tija ndo maana hata hawashughuliki?...Yaani wetu ni kama wamempuuza hivi.
Wakenya wanaeleweka ni wabepari, sisi haijulikani.
 
SA na Nigeria hawakuhitaji major non-NATO ally status ili kuwa na uchumi mkubwa barani Africa
Huijui dunia wewe.

Sa imebebwa na Marekani miaka yote ya ubaguzi wa rangi mpaka ubaguzi umeisha.

Nigeria ina mafuta, ina idadi kubwa ya watu, si ajabu kiwa uchumi mkubwa, na bado inaanguka kwenye charts, unaitoleaje mfano?
 
Haikupangwa siku nyingi sana; mwaliko ulikuja mwezi wa pili ikiwa ni muda mfupi sana baada ya Mahakama Kuu ya Kenya kuzuia polisi wa Kenya kwenda Haiti. Hata kama kulikuwa na mipango hiyo ya kumwalika, jambo ambalo Marekani inataka kufanya kwa kiongozi mmoja mmoja wa Afrika, huenda ziara hii ya Rutto isingekuwa mwezi huu.
Basi mkuu, tuliachie hapa. Ziara imekwisha fanyika. Waliyotaka na kukubaliana yamefikiwa.

Tuendelee na mengine, hasa kuona ufanisi wa ushirikiano kati ya mataifa unavyozidi kunoga, na kama kuna litakalotuhusu sisi majirani katika ushirikiano huo. Binafsi hili ndilo la muhimu zaidi kwangu.

Pengine tutayasoma na kuyaelewa mengi zaidi yakijipambanua kadri ya muda utakavyozidi kusonga.

Sijaona lolote katika yaliyosemwa, au ishara ya kipekee inayonifanya nibadilishe mawazo niliyokuwa nayo toka tuanze kujadili hili swala.
 
Sawa.

Sasa imekuwaje Tanzania nchi ambayo ilikuwa na ushawishi mkubwa sana Africa miaka ya Nyerere siku hizi imepoteza ushawishi huo na Kenya ndiyo inachujua ushawishi huo?

Mbona inakuwa kama huelewi hoja ya uzi?
Sasa Kenya ina ushawishi gani Africa so far?

Kenya imetumika kama njia ya Marekani kuyahadaa mataifa mengine ya Africa
 
Huijui dunia wewe.

Sa imebebwa na Marekani miaka yote ya ubaguzi wa rangi mpaka ubaguzi umeisha.

Nigeria ina mafuta, ina idadi kubwa ya watu, si ajabu kiwa uchumi mkubwa, na bado inaanguka kwenye charts, unaitoleaje mfano?
Mkuu tunazungumzia major non-NATO ally status
 
Nairobi is a financial hub, capitalist wote wanapiga deal pale, kwa sasa Kenya imeibuka kama number one in geothemal energy na beberu kaweka pesa yake nyingi sana, na ukiangalia vizuri American corporations kubwa kama Google na microsoft wana ofisi kubwa sana Nairobi, US wanajenga multi billion dollar highway kubwa sana from Mombasa to Nairobi naona wanataka kuwa na some control na bandari ya Mombasa to slow down mchina, bila kusahau wana military base in Lamu, kwa ufupi Kenya kuna pesa nyingi sana ya mabeberu inazunguka, siku hizi sio lazima uende London maana mabeberu wapo Nairobi wanaweza kumaliza shida zako
 
Back
Top Bottom