Kwanza hii siyo "safari ya haraka" kama unavyo sema wewe. Imepangwa muda kitambo sana.Tunaweza kutumia muda mwingi kuongelea hili lakini ileweke tena kuwa swala la Haiti ndiyo limesababisha uratibu wa safari hii kwa haraka haraa hivyo.
Kama ulivyosema hapo, kwa upande wangu la Haiti halina uzito mkubwa katika ziara hii. Hata hili limekuwepo muda mrefu wa kutosha, lisingehitaji uharaka wa ziara.
Kama yale mazungumzo ya mkataba wa kiuchumi/biashara yangekuwa yamekamilika, labda hapo ningesema hapo ni jambo muhimu zaidi; lakini siyo Haiti.
Inashangaza kidogo jambo linalohusu swala hilo wala haligusiwi katika ziara hii. Naona AGOA mpya imeyazika hayo.