Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Kama kuna jambo la kipumbavu na la kijinga alilofanya huyu rais wa nchi jirani ni la kujipeleka kwa usa mzima mzima. Yaan kwa watu wenye akili mgando na wenye akili kisoda ndo wanaona kafanya jambo la kusifiwa, matekani huwa hasaidii nchi masikini, bali huzitumia kwa manufaa yake mwenyewe, once ukiwa huna potential kwake tena anakutema kama mua unavyotemwa ukiisha utamu.

Kwani nani kasema Ruto kafuata msaada Marekani?
 
Kwa hiyo kufanyiwa state visit ni kipaumbele? Mbona mna hoja hazina mashiko. Bado mna akili za kitumwa

Maraisi wa mataifa mangapi hawajafanyiwa state visit hapo Marekani yamepungukiwa nini?

Mimi sioni mantiki ya huu ushindani mlioleta
State Visit haiji hivihivi tu. Ukiona State Visit ujue kuna ma deal ya kusainiwa yapo, kuna strategic alliances zinajengwa. Luna business lobbying imefanyika. Hii inakuwa indication ya uwezo wa nchi kufanya deal kubwa na Marekani. Hupati State Visit kwenda kuuza sura tu.

Rais Omar Bongo wa Gabon alitaka kulipa dola za Kimarekani milioni 8 ili apate State Visit kukutana na George W. Bush. Alijua atapiga deals kubwa zaidi ya hiyo hela.

Mbona unaangalia State Visit kama State Visit tu bila ya kuangalia deals na strategic positioning inayofanyika?
 
Inaingia katika mzunguko wa hela Kenya, watalipwa askari wa Kenya, itaenda kwenye projects za capacity building Kenya, etc

Unafikiri Ruto mjinga atoe askari wake bila kupata kitu?
Ingeenda direct kwenye economic infrastructures ingekuwa na tija zaidi ingesupport productive activities
 
State Visit haiji hivihivi tu. Ukiona State Visit ujue kuna ma deal ya kusainiwa yapo, kuna strategic alliances zinajengwa. Luna business lobbying imefanyika. Hii inakuwa indication ya uwezo wa nchi kufanya deal kubwa na Marekani. Hupati State Visit kwenda kuuza sura tu.

Rais Omar Bongo wa Gabon alitaka kulipa dola za Kimarekani milioni 8 ili apate State Visit kukutana na George W. Bush. Alijua atapiga deals kubwa zaidi ya hiyo hela.

Mbona unaangalia State Visit kama State Visit tu bila ya kuangalia deals na strategic positioning inayofanyika?
Unafikiri nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kama Indonesia, Singapore zilihitaji state visit ngapi pale Marekani kufikia hapo zilipo?
 
Ingeenda direct kwenye economic infrastructures ingekuwa na tija zaidi ingesupport productive activities
Huwezi kujua hiyo status ina ma deal yapi yanayotangazwa na yapi yasiyotangazwa sana.

Na hujui ita i springboard Kenya vipi kufanya hayo mengine vizuri zaidi. Dunia nzima imemuangalia Ruto akikata deals katika njia ambayo haijamuangalia Samia.
 
Sijaona hoja yako hapa
 
Sijaona hoja yako hapa
Kenya is becoming a regional leader, commanding respect on the global scene in a way tgat Tanzania is equally waning and becoming less relevant.

Sababu zake nimezitaja hapo juu, moja kubwa ni jwamba viongozi wakuu wa Tanzania ni washamba.

Mtoa mada alitaka kujua kwa nini Ruto anaheshimika sana duniani ukimlinganisha na Samia.

Sababu nyingi nimezitaja hapo juu. Lakini kubwa zaidi ninkwamba viongozinwa Tanzania ni washamba.

Usichoelewa nini?
 
Sababu nyingi nimezitaja hapo juu. Lakini kubwa zaidi ninkwamba viongozinwa Tanzania ni washamba.
Ujanja wa kupewa state visit na kupewa misaada?

Nenda nchi za ASEAN na Latin America uone viongozi wajanja jinsi wanakuza uchumi wa nchi zao kwa kasi na kiteknolojia
 
Kipimo cha raisi anayeheshimika ni nini?
Ni anavyoweza kuongoza global agenda.

Ruto anaongoza agenda against dollar dependency Africa. Ndiyo maana kina Biden wanamuita kwenye ma state visit kupanga naye waende vipi, he is at the table setting the agenda.

Ruto anaongoza ajenda ya kupeleka Polisi wa Kenya Haiti, angalau watu wameona kaanzisha kitu, wanamsaidia kifedha na logistics nyingine.

Ruto anaongoza ajenda ya kuwapeleka Wakenya wasomi dunia nzima wakamate nafasi muhimu watoe fursa kwa wenzao walio nyumbani. Anawapigania watu wake.

Ruto anaifanyia haki dhana ya "kutofungamana na upande wowote", anaifanyia haki dhana ya "diplomasia ya uchumi". Anakula na Wachina, ananawa, anakula na Wamarekani. Anasema yeye anaangalia maslahi ya Wakenya tu.

Samia anaongoza ajenda gani kubwa kwenye nyanja za kimataifa?
 
Ujanja wa kupewa state visit na kupewa misaada?

Nenda nchi za ASEAN na Latin America uone viongozi wajanja jinsi wanakuza uchumi wa nchi zao kwa kasi na kiteknolojia
Hakuna msaada katika geopolitics, kuna strategic moves na partnership tu.

Mtoa mada ametaka kujua kwa nini Ruto anaheshimika kuliko Samia kimataifa, hajataka kumlinganisha Ruto na viongozi wa ASEAN wala Latin America.

You did not understand the basic and core question of the thread.
 
Mtoa mada ametaka kujua kwa nini Ruto anaheshimika kuliko Samia kimataifa, hajataka kumlinganisha Ruto na viongozi wa ASEAN wala Latin America.
Wewe si ndiye uliyeanza kusema Ruto anaheshimika duniani

Na mimi nikakupa mifano ya maraisi wa mataifa mengine duniani

Mbona umepanick tena?
 
Ni anavyoweza kuongoza global agenda.

Ruto anaongoza agenda against dollar dependency Africa. Ndiyo maana kina Biden wanamuita kwenye ma state visit kupanga naye waende vipi, he is at the table setting the agenda.

Ruto anaongoza ajenda ya kupeleka Polisi wa Kenya Haiti, angalau watu wameona kaanzisha kitu, wanamsaidia kifedha na logistics nyingine.

Ruto anaongoza ajenda ya kuwapeleka Wakenya wasomi dunia nzima wakamate nafasi muhimu watoe fursa kwa wenzao walio nyumbani. Anawapigania watu wake.

Ruto anaifanyia haki dhana ya "kutofungamana na upande wowote", anaifanyia haki dhana ya "diplomasia ya uchumi". Anakula na Wachina, ananawa, anakula na Wamarekani. Anasema yeye anaangalia maslahi ya Wakenya tu.

Samia anaongoza ajenda gani kubwa kwenye nyanja za kimataifa?
Kama sababu ni hizo basi hauna hoja za maana za kumheshimisha
 
Wewe si ndiye uliyeanza kusema Ruto anaheshimika duniani

Na mimi nikakupa mifano ya maraisi wa mataifa mengine duniani

Mbona umepanick tena?
Nimekurudisha mwanzo kabisa wa mada mtu kauliza kwa nini Ruto anaheshimika sana duniani kulinganisha na Samia?

Kwani hatuwezi kuangalia dynamics za nguvu ya foreign policy ya Kenya na Tanzania katika kuangalia nani anakuwa na ushawishi zaidi kimataifa?

Unataka kumlinganisha Ruto na rais wa Ufaransa katika ushawishi wa kimataifa?

Unaelewa kanuni ya kwamba unavyolinganisha vitu, linganisha vinavyolinganishika?
 
Kama sababu ni hizo basi hauna hoja za maana za kumheshimisha
Hujaeleza kwa nini sina hoja, hujaeleza Samia anaongoza ajenda gani kubwa ya kimataifa.

Nimekupa mpaka namba za GDP hapa, umekimbia kujadili uchumi kwa namba kulinganisha Kenya na Tanzania.

Watanzania mara nyingi mnakuwa masikini jeuri, mkiambiwa kupiga pesa sema na hawa mabepari mnajitia usela mavi.

Mwisho wa siku tukija kuangalia GDP mnachekesha. Kenya wako wachache zaidi, wana nchi ndogo zaidi, hawana rasilimali kama Tanzania, lakini GDP wanawashinda.

Kwa sababu nyie wabishi sana.

Maneno mengi, uchumi kichekesho.
 
Back
Top Bottom