Ukiangalia jinsi Rais Ruto alivyopokelewa kwa heshima Marekani utashangaa

Tunaweza kutumia muda mwingi kuongelea hili lakini ileweke tena kuwa swala la Haiti ndiyo limesababisha uratibu wa safari hii kwa haraka haraa hivyo.
Kwanza hii siyo "safari ya haraka" kama unavyo sema wewe. Imepangwa muda kitambo sana.
Kama ulivyosema hapo, kwa upande wangu la Haiti halina uzito mkubwa katika ziara hii. Hata hili limekuwepo muda mrefu wa kutosha, lisingehitaji uharaka wa ziara.
Kama yale mazungumzo ya mkataba wa kiuchumi/biashara yangekuwa yamekamilika, labda hapo ningesema hapo ni jambo muhimu zaidi; lakini siyo Haiti.
Inashangaza kidogo jambo linalohusu swala hilo wala haligusiwi katika ziara hii. Naona AGOA mpya imeyazika hayo.
 
Utapeli waliotakiwa kutapeliwa wamarekani walipoushitukia , hata vazi sutico,linakataliwa nchini ikabidi kaundasuti ziaze kuvaliwa

Tazara yenyewe imechoka kuliko mchoko wenyewe
 
Subirini Yanga nayo imealikwa. Mabingwa wa ball wa mara zote Tanzania wanaenda unyamwezini kukaa kwenye kiti cha mzee baba
 
Umejitahidi sana kujieleza, na yote uliyoeleza yanajulikana. Ila bila kusita kabisa nabaki palepale. Ziara ya Ruto haikuwa ya kustukiza hata kidogo; hii imepangwa kiutaratibu tokea mwanzo kwa nia ile ile ya Marekani kuwa na eneo lake katika ukanda huu. Kenya haikuanza jana chini ya Ruto kuwa chini ya 'influence' ya Marekani. Kidogo Mwai Kibaki aliwastua sana wakubwa, alipogeukia Mashariki. Na kutokana na kuingia kwa China, Marekani anaona maslahi yake yanalegalega; kwa hiyo sasa ana'catch up'.
Siyo mara ya kwanza Ruto kuingia Jumba Jeupe tokea ashike madaraka. Mipango hii ilianzia hata kabla Uhuru hajaachia madaraka. Huu ni mpango endelevu, siyo wa kustukiza.
 
Ni kweli kuna uelewa mdogo, lakini watu wote hawawezi kuwa na uelewa mkubwa, ukitaka iwe hivyo na wewe utakuwa na uelewa mdogo. Kuna watu wanajifunza, wengine wadogo, sasa watajuaje mambo bila kujifunza?

Jana niliandika tofauti ya state visit na visits nyingine, nikaitaja hii ziara ya Nyerere, lakini sikuona haja ya kubeza watu.

Zaidi, swali la msingi liko palepale, kwa nini Kenya inashamiri sana kinataifa zaidi ya Tanzania? Kwa nini Kenya imekuwa nchi ya kwanza Afrika kupata State Visit Marekani tangu mwaka 2008, na Tanzania haipati nafasi hizi?

Kuna jibu refu la historia ya Kenya kama koloni proper la Waingereza ambalo halijapitia Ujamaa kama sisi, geopolitics, Wakenya walivyojipanga ku lobby, business culture ya Kenya, masuala ya Kenya kwenda kulinda amani Haiti, siasa za Umagufuli kujifungia zilivyoharibu mahusiano ya kimataifa ya Tanzania, Samia kutojua anataka kufanya nini, Tanzania kuji align zaidi na China, yote haya yanahusika.
 
Mbona rais wa wasafi WCB, diamond platnumz amepokelewa kwa heshima nchini marekani na barani ulaya πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Pdidy alimpokea kwa heshima sana πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…