Ukiangalia kichapo kinachotolewa na Israel utagundua Russia ni overrated sana

Hii kitu huwa inanishangaza sana, yaan ukiingia hii thread unakutana na vijana wa hovyo ambao wamegueza vita vinavyosababisha vifo vya mamilioni ya watu kama ushabiki wa michezo

Wengi ni vijana wa juzi ambao hawajui hata baruti inasikikaje.
 
 
Very correct, mleta mada bado hajakuwa ndio maana kashindwa kutofautisha hao wawili
 
Ushajiuliza ni vipi kama Urusi angekuwa anawasaidia washirika wake moja kwa moja pale mashariki ya kati, kama Marekani anavyofanya ni kitu gani kingetokea? Unadhani Israel angekuwa anatamba kama anavyotamba leo?
 
ALPHA, KAJIFUNZE KWANZA KUANDIKA THEN URUDI TENA SIO "MALALIA" NI "MALARIA" OMEGA, ACHA KUSHIKIWA AKILI KUWA MTU HURU MWENYE FIKRA HURU.
😂

Mkuu, umetisha ila unahatari, unatumia jina tukufu kwenye mambo yasiyo na maana
 
Sema ninahisi yaliyoandikwa kwenye Biblia yakawa na ukweli 100%. Kuwa atakayekubariki nitambariki na atakayekulaani nitamlaani. Nadhani Marekani hii siri ameijua muda mrefu sana na ndio maana muda wote ameikumbatia Israel kama mwanae vile. NA HUENDA HII NDIO SIRI KUBWA YA MAFANIKIO YA TAIFA LA MAREKANI kuwa na nguvu kubwa na uchumi kuliko taifa lolote lile duniani.
Angalia Mataifa yenye uadui na ISRAEL uone jinsi yanavyoanguka na kudumaa.

Hata Russia hii siri anaijua na ndio maana huoni akiiletea ISRAEL chokochoko.

Nchi nyingi duniani zenye uhusiano mzuri na ISRAEL zimestawi sana. Hata jirani zetu Rwanda japo ni kanchi kadogo na kanaendeshwa kidikteta lakini ana ustawi mzuri sana na jamii yake ipo vizuri hasa baada ya mauaji ya Kimbari.

Angalia Idi Amini Dada alivyowasaliti ISRAEL mwaka 1978 kwa kuwateka wale wayahudi, huenda ile ndio laana iliyomfanya ashindwe vita na likawa ni anguko lake.

Angalia jinsi Kenya ilivyobarikiwa katika Uchumi na Maendeleo ya nchi, wao miaka yote tangu uhuru wamekuwa na mahusiano mazuri sana na ISRAEL tofauti na sisi tuliovunza uhusiano na ISRAEL kipindi cha Nyerere, japo alipokuja Magufuli alirejesha. Na kipindi chote hicho Maendeleo yetu yalidumaa sana.

Tusishupaze shingo zetu na TUSIUKWEPE UKWELI. Nadhani hata Farao pamoja na kuona matendo makubwa yaliyotokea kwa wayahudi lakini bado alikuwa mgumu kuukubali ukuu wa Mungu wa ISRAEL. Hivi kweli unamkimbiza mtu halafu anafika baharini unajua sasa unamkamata halafu ghafla unaona maji yanajitenga kulia na kushoto na kutengeneza njia ili mtu huyo apite, HALAFU BADO UNAKOMAA KUMFUATA .

WAISLAMU NA WALE WA KRISTO MSIO AMINI KUWA MUNGU WA MBINGUNI ALILIBARIKI LILE TAIFA NA HATA SASA ANALILINDA . TUJITAFAKARI

MIMI NINAAMINI HUENDA HATA KULIWAZIA MABAYA TU LILE TAIFA NI LAANA
 
Ni ajabu kweli nahisi labda wengi humu ni mapolisi na wajeda!
 
Wanaposhambulia Hamas Huwa mpo kimya
 
Ushajiuliza ni vipi kama Urusi angekuwa anawasaidia washirika wake moja kwa moja pale mashariki ya kati, kama Marekani anavyofanya ni kitu gani kingetokea? Unadhani Israel angekuwa anatamba kama anavyotamba leo?
Nan kamzuia Urusi kufanya hivyo ? unahisi alikuwa hafanyi hivyo ? Unahis moto wa Ukraine ni wa kitoto?
 
hivi hujui kuwa bila Israel hakuna Marekani?

hivi hujui advanced technology zote duniani zina mkono wa Myahudi?
 
hivi hujui kuwa bila Israel hakuna Marekani?

hivi hujui advanced technology zote duniani zina mkono wa Myahudi?
Marekani ilikuwepo kabla hata wayahudi hawajaanza kubanikwa na Hitler,na si kweli kuhusu tech zote kuwa na mkono wa myahudi,pili jifunze myahudi ni nani
 
Israel hana kelele ni kipigo tu

Russia kelele Nyingi mara atishie kutumia nyuklia na mambo mengi ..

Tunataka atoe kichapo .

Usimlaumu Russia, sijui ni lini Mtaamini Israel ina favor ya Mungu, yote yanayotokea Israel yapo kwenye Maandiko! Watapigwa mpaka mwisho wa Ulimwengu!
 
Wavuta bangi gani tena wanamiliki ballistic missile au mimi ndio sijui kuhesabu ????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…