Ila maisha yanabadilika sana. Hivi inakuwaje mtu kutwa anashabikia mauaji yanayotokea sehemu fulani? Ni roho mbaya, uchawi au ujinga?
Yani kabisa unaandika tunataka kichapo sio makelele, hujisikii hata vibaya japo kidogo? Unahisi hawa wanaokufa hawana roho, au hawana ndugu na familia? Wewe umewahi kufiwa mkuu na kupoteza wapendwa wako, ulijisikiaje?
Dunia kwa namna yoyote inabidi iwe sehemu salama ya kuishi, kukaa bonyokwa na kuanza kushabikia mauaji yanayotokea Iran au Israel au Palestina au Ukraine ni ujinga sana, unahisi hayakuhusu sio? Tambua mambo yakichachaa huko unakoona hakukuhusu HATA WEWE HAUTAKUWA SALAMA.
Haijalishi anakufa mwarabu, muisilami, muisraeli, mwafrika au baniani ni lazima binadamu tuwe na utu. Ni muhimu tujitofautishe na wanyama japo kwa akili tu