A
Anonymous
Guest
Kero yangu ni Ofisi ya Kata ya Gongo lamboto iliyopo Pugu Kona, Maafisa Biashara wa Halmashauri wamekuwa wakikamata Wafanyabiashara na wasiokuwa na leseni au wenye leseni lizizoisha na wengine kuhusu kodi ya Service Levy ambayo kwa asilimia 80 watu hawana uelewa kuhusu kodi hiyo.
Baada ya kuwakamata huwafikisha Ofisi ya Kata iliyopo Pugu na kuwaandikia bill kubwa wakidai ni penaty, faini na ada na huwalazimisha kulipa hapohapo ndiyo waruhusiwe kuondoka, ukishindwa kulipa unapelekwa Kituo cha Polisi Stakishari.
Hivi karibuni walifika dukani kwangu wakakuta leseni yangu imeisha muda, nikawaambia hali ya biashara si nzuri najipanga ni renew hawakunielewa wakanichukua na kunipeleka kwenye hizo ofisi, wakaniandikia bili ya Sh 840,000 na kunilazimisha nilipe ndiyo nitoke.
Sikuweza kulipa nikapelekwa Polici Stakishari, nikalala kituoni bila kufunguliwa kesi na kila polisi niliyemuuliza kituo walinijibu hawahusiki.