KERO Tunaofanya biashara ya Saluni hatuna Elimu Kuhusu malipo ya Service Levy

KERO Tunaofanya biashara ya Saluni hatuna Elimu Kuhusu malipo ya Service Levy

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaofanya biashara ya saluni, utaratibu wa kupata leseni ni kulipia kwanza kibali cha BASATA kupitia tovuti yao, kisha kuomba leseni ya biashara kwa Shilingi 40,000 kwa mwaka. Hata hivyo, wafanyabiashara wengi hatufahamu utaratibu wa kulipa service levy kupitia mfumo wa Tausi wa halmashauri.

Wafanyabiashara wengi tunaamini kuwa baada ya kulipa leseni na kodi ya mapato, tumekamilisha wajibu wetu. Halmashauri hazijatoa elimu ya kutosha kuhusu tozo hii.

Maafisa wanapofika kwenye biashara zetu, wakikuta leseni wanatuomba tuwaonyeshe uthibitisho wa kulipa service levy, jambo ambalo wengi wetu hatulielewi. Kama tungepewa elimu ya kutosha, tungeweza kulipa Shilingi 15,000 kila baada ya miezi mitatu na kutimiza wajibu huo.

Kwa mwaka, gharama za leseni ni Shilingi 40,000, kibali cha BASATA Shilingi 20,000 na kodi ya mapato Shilingi 70,000. Ukijumlisha na service levy ya Shilingi 60,000 kwa mwaka, jumla inafikia Shilingi 190,000, kiasi kikubwa kwa mfanyabiashara mdogo.

Naomba halmashauri zitoe elimu kuhusu utaratibu huu ili kuondoa kero zinazoweza kuepukika na mianya ya rushwa. Maafisa wanapewa nafasi ya kupanga service levy itaanza kulipwa lini, pamoja na faini, jambo linaloweza kufanya deni kufikia Shilingi 300,000.

Hali hii inaweza kufungua mianya ya baadhi ya maafisa kuomba rushwa ili kupunguza deni la mfanyabiashara.
 
Back
Top Bottom