Ukichunguza kwa umakini ndoa ni Shimo la mateso matupu

Ukichunguza kwa umakini ndoa ni Shimo la mateso matupu

Ili ndoa iwe tamu basi mmoja awe bwege. Wanaume wengi ndoa zinakua shubiri kwao pale mke anakataa kuwa bwege

Wanawake ndoa zinakua chungu

1. mume akikosa pesa
2.akiwa karibu sana na ndugu zake
3 etc
 
Vitabu vyote vya kiimani vimekemea uzinz, uzinz ni source ya hali ngumu ya kimaisha na ndo mana wengi wetu maisha yetu hohehae kwsbb ya uzinz, NDOA ni muhim
 
Najua wengi wataonibishia lakini tukatae tukubali ndoa ndio chanzo kikuu cha matatizo ya binadamu, matatizo kama vile magojwa ya moyo, stress, afya ya akili, kisukali n.k, mengi yamewapata binadamu wengi baada ya kuingia kwenye ndoa.

Hebu fikiria watu mpoo ndani ya ndoa lakini;

1. Ugomvi haushi ndani ya nyumba.

2. Unyumba mnanyimana.

3. Wanaume wengine wanachelewa kurudi nyumbani kisa wanawaogopa wake.

4. Kesi za kuchepuka haziishi.

5. Dharau, kejeli.

Sasa hii ndoa au mateso?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Matatizo uliyoyataja yapo hata kama haupo kwenye ndoa,
Kama unaingia kwenye ndoa kuepuka stress,utqkuwa unachemka,
Zipo stress za pesa,za ajira,boss mkali,
Stress za magonjwa.stress za familia l,ndugu,
Tatizo kubwa watu wanaingia kwenye ndoa bila kujua lengo la ndoa,kwenye ndoa hautafuti mtu mkamilifu,unatafuta mwenza mkamilishane mapungufu yenu,
Usiingie kwenye ndoa bila kujua tofauti ya kuwa mme,mke,baba,mama,
Unaoa harafu Bado unataka uishi kama boyfriend,girlfriend,au uendelee kuishi kama msela wa gheto,
 
Binafsi ndoa imenidisappointments sana, bahati mbaya tena ndoa za kikristo ambazo no return kwa kweli tunakutana na changamoto kubwa sana.
Lakini kwaajili ya uzazi na malezi kwa maslahi ya taifa leo na kesho acha ndoa ziendelee maana kwa ujumla maisha ya mwanadamu ni mateso tu na ndoa ni sehemu moja wapo ya mateso ya binadamu.

Kwa sisi wa kristo tumeambiwa kila mtu abebe msalaba wake kuekekea kalvari ya mbinguni.
Kosa kubwa lingine ni mtu kukubali ndoa ni mateso na akakubali kuishi hivyo kwa kuamini hivyo atateseka mara 2 zaidi ya awali
 
Ukifanya ngono na mtu kabla ya kumchunguza huwezi ona tabia zake mbaya.
Hakuna binadamu anaebadilika tabia hizo ndizo tabia zake ulikuwa kipofu sababu ulikuwa na nyege nae zimeisha SAsa upofu umeondoka.
Watu wa mila na dini kupinga ngono kabla ya ndoa awakuwa wajinga. Lengo ni kuzuia kuunganisha nafsi ukiunganisha nafsi na mtu huwezi yaona mabaya yake.
Kwenye ndoa ni miezi 3 tu nyege uisha then unamuona wa kawaida tu, hapo kinachobakia kushika ndoa ni tabia na kuendana pekee.
Kumbe hapa napo pana darasa, komment hii imenifunza usiruhusu hisia/nyege ziongoze maamuzi yako.
 
Najua wengi wataonibishia lakini tukatae tukubali ndoa ndio chanzo kikuu cha matatizo ya binadamu, matatizo kama vile magojwa ya moyo, stress, afya ya akili, kisukali n.k, mengi yamewapata binadamu wengi baada ya kuingia kwenye ndoa.

Hebu fikiria watu mpoo ndani ya ndoa lakini;

1. Ugomvi haushi ndani ya nyumba.

2. Unyumba mnanyimana.

3. Wanaume wengine wanachelewa kurudi nyumbani kisa wanawaogopa wake.

4. Kesi za kuchepuka haziishi.

5. Dharau, kejeli.

Sasa hii ndoa au mateso?

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Mara nyingi nyinyi mnaoandika hivi ni watoto wa mitaani. Ndoa zenye amani zipo nyingi tu. Msiwe mnaandika ushuzi ushuzi bila takwimu.
 
Ndoa inaundwa na watu wawili na lazma muwe mmejuana inside out.

Hakikisha mwanamke wako anayajua madhaifu yako na wewe unayajua yake kisha ndio mfanye maamuzi sasa ya kuoana. Ikiwa hutayajua madhaifu ya mwenza wako basi ujue ndoa yenu ikimaliza miezi 6 bila mgogoro Mungu anawapigania.

Shida nayoiona wengi huwa tunagubikwa na fantasies na kusahau kuwa ndoa ni uhalisia. Ndoa sio maigizo hivyo kila mtu lazma awe real na mwenzake.
 
Kosa kubwa lingine ni mtu kukubali ndoa ni mateso na akakubali kuishi hivyo kwa kuamini hivyo atateseka mara 2 zaidi ya awali
Nakubaliana nawe, mtu akiweza kuiset akili na ufahamu wake hata kama yupo jela ataona kawaida tu maadamu anaishi.
Ila siku zote juwa mwanadamu na pengine viumbe vyote vinapigania uhai na uhuru.
 
Back
Top Bottom